DC Nickson Simon John awataka watumishi Songwe kujenga utamaduni wa kazi unaotoa matokeo

DC Nickson Simon John awataka watumishi Songwe kujenga utamaduni wa kazi unaotoa matokeo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Nickson Simon John, Oktoba 8, 2026 alifanya kikao na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe katika Ukumbi wa Sambila, akisisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kiutendaji unaozingatia matokeo na mahitaji ya Wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho, Nickson amesema mafanikio yataamuliwa na utamaduni wa kiutendaji unaojengwa ndani ya taasisi, akiwataka Watumishi kufanya kazi kwa pamoja na kujenga mazingira yanayowezesha utekelezaji wenye matokeo.
DC NICKSON AWATAKA WATUMISHI SONGWE KUJENGA UTAMADUNI WA KAZI UNAOTOA MATOKEOMkuu wa Wilaya y...webp
DC NICKSON AWATAKA WATUMISHI SONGWE KUJENGA UTAMADUNI WA KAZI UNAOTOA MATOKEOMkuu wa Wilaya y...webp
Aidha, amewataka Watumishi kufikiri kimkakati na kuhakikisha wanaifanya Serikali kuwa taasisi inayokwenda na wakati, yenye uwezo wa kutambua changamoto, kuzitafutia majibu na kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya Wananchi.

Nickson pia amesisitiza umuhimu wa kuwa na uongozi unaolenga kuleta suluhu kwa matatizo ya Wananchi, akiwataka Watumishi kutumia nafasi zao, maarifa na rasilimali zilizopo katika kutatua changamoto na kuhakikisha kazi za Serikali zinakuwa na matokeo yanayoonekana kwa Wananchi.
DC NICKSON AWATAKA WATUMISHI SONGWE KUJENGA UTAMADUNI WA KAZI UNAOTOA MATOKEOMkuu wa Wilaya y...webp

DC NICKSON AWATAKA WATUMISHI SONGWE KUJENGA UTAMADUNI WA KAZI UNAOTOA MATOKEOMkuu wa Wilaya y...webp
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, Bwana Godfrey Kawacha, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, CPA Cecilia Kavishe.
 
Back
Top Bottom