DC Sabaya abadili matumizi ya fedha ya mfuko wa Jimbo la Mbowe

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC) mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, Lengai Ole Sabaya, amezuia Sh. 42 milioni za mfuko wa Jimbo la Hai na kuagiza kati ya fedha hizo Sh. 7 milioni ziende kujenga choo cha walimu wa shule ya msingi Mijongweni iliyopo kata ya Mnadani wilayani humo.

Fedha hizo za mfuko wa Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge wake, Freeman Mbowe kupitia tiketi ya Chadema, zilikuwa zigawanywe kwa kila kijiji ambapo katika mgawanyo huo, kila kijiji kingepewa Sh. 500,000.

Hata hivyo, Sabaya amesema leo Jumamosi Desemba 28,2019 kuwa ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, Yohana Sintoo, kutoa Sh. 7 milioni na kuzipeleka katika shule hiyo na amemtaka awe amezikabidhi Jumatatu bila kukosa.

"Nimemuagiza DED (Mkurugenzi) atoe Sh7 milioni kati ya Sh42 milioni za mfuko wa Jimbo nilizozizuia ziende kutatua changamoto ya choo kwenye hiyo shule na amenihakikishia zitaenda Jumatatu," amesema Sabaya.

Shule hiyo haina choo cha walimu kwa miaka 10 sasa na walimu wamekuwa wakijisaidia katika choo cha Zahanati iliyopo jirani na shule jambo ambalo Sabaya amesema halikubaliki na ndio maana ameelekeza sehemu ya fedha za mfuko wa Jimbo ziende huko.

Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Hai kupitia kwa mkurugenzi wake Sintoo imekabidhi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya kuanzisha mchakato huo na ndipo Sabaya alipoingilia kati ili choo hicho kijengwe na kukamilika Januari 2020.

Jitihada za kumpata Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kuzungumzia uamuzi huo wa Sabaya zinaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye maamzi na zile fedha ni nani???? Busara ninayoiona mimi ili kuwepo na balance of change mh. Mbowe angeshirikishwa kwenye hilo ili kujenga mtazamo wenye kufanana maana suala la choo ni huduma mhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ma DED waonywa kutumia fedha za mifuko ya jimbo











Serikali ya Tanzania imetoa onyo kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini kutozitumia fedha za mifuko ya jimbo bila idhini ya mbunge kwani hawana uamuzi na fedha hizo.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatatu Mei 13, 2019 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji.

Katika swali lake, Haji ametaka kujua iwapo kuna baadhi ya wakurugenzi hufanya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo bila kuwashirikisha wabunge hususan Zanzibar, Je, katika hili suala la kusimamia fedha hizi ni la Mbunge au Wakurugenzi.

Akijibu swali hilo, Mwita amesema mwenyekiti wa fedha za mfuko wa jimbo ni mbunge na wajumbe wanajulikana kwa mujibu wa sheria, kanuni na mkurugenzi anapaswa kuheshimu uamuzi wa kamati hiyo ambayo mbunge ndiyo mwenyekiti wake.

Mwita amesema kama mbunge ataridhia fedha hizi kutumika sehemu fulani Mkurugenzi hawezi kuzuia, kama mbunge atakwenda eneo A au B na kusikiliza kero za wananchi na kuahidi kutoa Sh. 500,000 Mkurugenzi hawezi kubadilisha.

Chanzo: Mwananchi
 
Natumai unaendelea vyema na majukumu yako,nimesoma taarifa yako hii hapo chini, nimeshtuka sana.

"DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya amezuia Sh42milioni za mfuko wa Jimbo la Hai linaloongozwa na Freeman Mbowe (Chadema) na kuagiza kati ya fedha hizo, Sh7milioni ziende kujenga choo cha walimu wa shule ya msingi Mijongweni " #MwananchiUpdates

Hii taarifa imenishtua sana ,ila nikagundua tatizo ni sifa za kisiasa na ukosefu wa maarifa katika majukumu yako ,pia kutokuwa na uwelewa na tamaduni ya kufuata na kuheshimu sheria,nadhani viongozi wengi wa umma mmezoeshwa hivyo ,tabia hii itatuumiza na kurudisha maendeleo ya taifa letu nyuma sana,tuheshimu sheria.

Tuache hayo ,haya tuelekezane kidogo ili ujue kuhusu mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo siku nyingine usirudie kutia aibu aliyekuteuwa.

Fedha za mfuko wa kuchochea Maendeleo ya jimbo zinasimamiwa na Sheria Na. 16 ya mwaka 2009 (The Constituencies Development Catalyst Fund Act, Na.16 of 2009) ambayo inamtaka mbunge kuelekeza fedha hizo kwenye miradi inayoibuliwa na wananchi wenyewe katika Jimbo husika.

Kwa mujibu wa Sheria hii kifungu cha 10 a,b,c,na d kimeelezea juu ya kuwepo kwa kamati ya mfuko wa jimbo ambayo imepewa jukumu la usimamizi wa fedha za mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo.

Kamati hiyo inapaswa kuwa na wajumbe saba ambao ni,

#Mbunge mwenyewe kama mwenyekiti .

#Afisa mipango wa Halmshauri au Manispaa ambaye ndiye katibu.

#Madiwani wawili ambao ni wajumbe.

#Afisa watendaji wa kata wawili (WEO) ambao ni wajumbe.

#Na mjumbe mmoja aliyeteuliwa na kamati kutoka katika shirika lisilo la kiserikali (NGO) katika eneo la jimbo hilo.

Ukisoma pia kifungu cha 7 (1) kimeelezea vyema kwamba ugawaji na utoaji wa fedha hizo utaidhinishwa na kati hiyo ya fedha ya maendeleo ya jimbo.

Ukisoma pia kifungu cha 7 (2,3) kimeelezea kwamba taarifa za kupokea fedha hizo na matumizi yake zinapaswa taarifa hizo ziwasilishwe kwa waziri husika wa serikali za mitaa .

Ukisoma kifungu cha 7(4) kinasema kamati hiyo inaweza kuweka vipaumbele wapi fedha hizo ziende.

Sasa mimi nikuulize DC Sabaya ,wewe ni mjumbe wa kamati hiyo ? , Nikuulize DC Sabaya kwani wewe ndiye kamati wa mfuko wa fedha hizo za Jimbo la HAI ? , Nikuulize DC Sabaya hayo mamlaka ya kuzuia fedha za mfuko wa jimbo umeyatoa wapi ? , Nikuulize DC Sabaya sheria ipi umeitumia kuzuia hizo fedha ?

DC hana hayo mamlaka ya kuzuia hizo fedha hata DED (Mkurugenzi)hana hayo mamlaka ya kuzuia hizo fedha.

Ndio maana Boss wenu,Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara tayari alitoa kauli ya serikali Bungeni tar 13/Mei /2019 J.tatu akiwapiga marufuku Ma DED waheshimu fedha hizo wasizigusi bila idhini ya kamati ,Sasa wewe DC Sabaya huelewi nini ? ,Soma kauli ya bosi wako hapo katika Link

" Ma DED waonywa kutumia fedha za mifuko ya jimbo "

Au ndio sifa ili uonekane unapambana na Mbowe ?,Sifa bila maarifa na uelewa utaaibika tuu na kuonekana kituko bure hata kwa aliyekuteuwa.

Fuata sheria ,Fuata sheria tunasheria zetu ziheshimu katika utekelezaji wa majukumu yako,jimbo linachangamoto nyingi ulishindwa kupendekeza kama maoni ili kamati ipeleke fedha huko ,maana fedha hizo sio nyingi kiasi cha kutatua kero zote za jimbo kwa wakati mmoja.

Shukrani nakutakia heri ya mwaka mpya.

Mwanahabari Huru
 
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!
 
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!
Ujinga mtaacha lini? Mbona mwasisi wa chama chenu alionya sana kuhusu kufuata katiba? Hatuwezi kuendesha nchi kwa "busara za viongozi". Nchi iendeshwe na sheria. Kama hana mamlaka ya kisheria ku"zielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii", kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Tuache kuongozwa na ukada, sheria zimetungwa na CCM leo CCM wanaongoza kuzivunja. Mtakuja kulipa siku moja
 
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!
Anazielekeza Kama nani ndani ya Jimbo?.Je sheria inamruhusu kufanya hivyo?.

Au ndio kwenye suala la maendeleo kuvunja sheria inaruhusiwa?.

Je kuna umuhimu wakuwa na sheria na taratibu juu ya fedha hizo, kama mkuu wa wilaya anaamua ziende wapi bila sheria kumruhusu?.

Vipi siku mkuu wa mkoa akianza kuzuia fedha zote za majimbo katika mkoa aliopo,unafaham nini kitatokea?.

Kama suala nikuletee maendeleo hebu jaribuni wana ccm na serikali kubadili sheria ambazo mnahisi nivikwazo kwenu, ili mfanye jambo lolote mnalohitaji bila kuvunja sheria.
 
Kwani lugha ya kushauri na siyo ya kuagiza ingetumika kwa jamii iliyo nje hata kama huko ndani watalazimishana si ingekuwa bora! Kwani choo ni muhimu pia
 
Kwa akili yako unafikili Mbowe ananjaa ya ml.42?anaweza akawafuga ukoo wenu wote pamoja na aliyekutuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…