DC Sabaya abadili matumizi ya fedha ya mfuko wa Jimbo la Mbowe

DC Sabaya abadili matumizi ya fedha ya mfuko wa Jimbo la Mbowe

Hana Malmlaka ya kuingilia Majukumu ya Kamati.
Nafkir yeye angepeleka maombi ya kuhusu hiyo shule kutengenezewa choo. Hayo maombi yaambatane na BOQ ili wajumbe wajiridhishe kiasj Cha Pesa kilichoombwa.
But alivyofanya nj ulimbukeni/Sifa za kijinga.
Hudumia wananch wako huku ukifuata Protocal za kazi husika.
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC) mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, Lengai Ole Sabaya, amezuia Sh. 42 milioni za mfuko wa Jimbo la Hai na kuagiza kati ya fedha hizo Sh. 7 milioni ziende kujenga choo cha walimu wa shule ya msingi Mijongweni iliyopo kata ya Mnadani wilayani humo.

Fedha hizo za mfuko wa Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge wake, Freeman Mbowe kupitia tiketi ya Chadema, zilikuwa zigawanywe kwa kila kijiji ambapo katika mgawanyo huo, kila kijiji kingepewa Sh. 500,000.

Hata hivyo, Sabaya amesema leo Jumamosi Desemba 28,2019 kuwa ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, Yohana Sintoo, kutoa Sh. 7 milioni na kuzipeleka katika shule hiyo na amemtaka awe amezikabidhi Jumatatu bila kukosa.

"Nimemuagiza DED (Mkurugenzi) atoe Sh7 milioni kati ya Sh42 milioni za mfuko wa Jimbo nilizozizuia ziende kutatua changamoto ya choo kwenye hiyo shule na amenihakikishia zitaenda Jumatatu," amesema Sabaya.

Shule hiyo haina choo cha walimu kwa miaka 10 sasa na walimu wamekuwa wakijisaidia katika choo cha Zahanati iliyopo jirani na shule jambo ambalo Sabaya amesema halikubaliki na ndio maana ameelekeza sehemu ya fedha za mfuko wa Jimbo ziende huko.

Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Hai kupitia kwa mkurugenzi wake Sintoo imekabidhi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya kuanzisha mchakato huo na ndipo Sabaya alipoingilia kati ili choo hicho kijengwe na kukamilika Januari 2020.

Jitihada za kumpata Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kuzungumzia uamuzi huo wa Sabaya zinaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama alivyo Baba ndivyo alivyo mwana
 
Utawala huu ni utawala usiofuata sheria kuanzia Bwana yule wa juu na hawa wasaidizi wake!!
 
JK alikuwa na utaratibu wa kuwapa semina kule Ngurdoto haya hatukuyaona. Leo hii ndiyo fashion, anafukuzia nafasi za akina mnyeti, gambo na yule mjinga mmoja wa iringa jina nimesahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo DC kapewa kazi maalum,ana kazi ya kudill na mbowe na anajitahidi kuonyesha kua mbowe hafanyi chochote kwenye Jimbo lake,pia anajitahidi kumwonyesha jiwe kua anachapa kazi" DC wa mwendo kas"
 
Sheria hairuhusu mtu kuingilia mfuko wa jimbo zaidi ya Mbunge ambae ndie mwenyekiti na kmati yake. Hata DED hana mamlaka na hiyo pesa bila kamati ya mfuko wa jimbo kuitolea mamuzi. Shida iliyopo kwa sasa ni haw viongozi wa mwendo kasi kukurupuka bila kufuta sheria.
Huyo ndogo anahangaika na mtu aliyekwisha kumdharau tangu siku ya kwanza anfika Hai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sabaya ni Mtoto wa Mkubwa. Ana nguvu sawa na Baba yake hivyo kuwa na uwezo huo

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyu kijana wa Kimaasai hakika ni chizi,zezeta na pambaf mkubwa…!
Ole Sabaya kila akitokeza kwenye media utasikia kafanya fyongo la aidha KUVUNJA KATIBA au KUKIUKA SHERIA na MAADILI YA VIONGOZI!
Utasikia mara kamsweka mtu remande masaa 24 au 48 bila sababu za msingi zaidi ya ulevi tu wa madaraka na kujimwambafy!
Mara utasikia kaharibu mazao kwenye shamba la Mh. Mbunge Mbowe kwa kisingizio cha mazingira na leo tumesikia anaingilia kugawa fedha za Mfuko wa Jimbo ambazo zina kanuni na sheria yake…!

Kinachosiktisha au kushangaza ni kuona kwamba pamoja na vurugu hizi za hii Maasai hakuna onyo, kemeo au karipio kali kutoka mamlaka za juu yake!

Tafsiri inayoweza kupatikana hapa ni kuwa haya yote anayotenda Bw. Ole Sabaya ni MAELEKEZO TOKA JUU! The main target here is H.E. Aikael MBOWE(MP&CHADEMA Nation Chairperson)!
 
Back
Top Bottom