DC Sabaya abadili matumizi ya fedha ya mfuko wa Jimbo la Mbowe

Mwaka wa fedha huwa unaishia may? great thinkers tusaidie
Mbwiga mwaka wa fedha unaisha June lakini ukumbuke 2020 bunge linavunjwa mwezi June hivyo mambo yote ya procurement yatakamilishwa may 2020.

Swali lingine manka?
 
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!
Sio jukumu lake. Ni mambo ya utawala bora tu ambayo naona "hujayaelewa".
Mpelekeni mahakamani, msiishie tu kuandika humu mitandaoni. Hili tabia ya hawa viongozi kutokufuata sheria inapata nguvu maana hawapelekwi mahakamani.
Nafikiri upinzani unahaja ya kujijengea uwezo kwenye eneo hili. Watu washenzi wapelekwe mahakamani. Na mwakani fujo zitaongezeka sana hivyo wajipange.
 
Yawezekana wewe ni Muha!
Wao wanasifa za ubishi tuu, mmoja anaweza kubishana na behewa zima la 3rd class tokea Tabora hadi Kigoma yeye akisema kama Rais wa Kenya ni Kenyatta basi Rais wa Zambia ni Zambiatta. Na hadi Kigoma anafika hajashawishika tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
20191229_132026.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC) mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, Lengai Ole Sabaya, amezuia Sh. 42 milioni za mfuko wa Jimbo la Hai na kuagiza kati ya fedha hizo Sh. 7 milioni ziende kujenga choo cha walimu wa shule ya msingi Mijongweni iliyopo kata ya Mnadani wilayani humo.

Fedha hizo za mfuko wa Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge wake, Freeman Mbowe kupitia tiketi ya Chadema, zilikuwa zigawanywe kwa kila kijiji ambapo katika mgawanyo huo, kila kijiji kingepewa Sh. 500,000.

Hata hivyo, Sabaya amesema leo Jumamosi Desemba 28,2019 kuwa ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, Yohana Sintoo, kutoa Sh. 7 milioni na kuzipeleka katika shule hiyo na amemtaka awe amezikabidhi Jumatatu bila kukosa.

"Nimemuagiza DED (Mkurugenzi) atoe Sh7 milioni kati ya Sh42 milioni za mfuko wa Jimbo nilizozizuia ziende kutatua changamoto ya choo kwenye hiyo shule na amenihakikishia zitaenda Jumatatu," amesema Sabaya.

Shule hiyo haina choo cha walimu kwa miaka 10 sasa na walimu wamekuwa wakijisaidia katika choo cha Zahanati iliyopo jirani na shule jambo ambalo Sabaya amesema halikubaliki na ndio maana ameelekeza sehemu ya fedha za mfuko wa Jimbo ziende huko.

Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Hai kupitia kwa mkurugenzi wake Sintoo imekabidhi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya kuanzisha mchakato huo na ndipo Sabaya alipoingilia kati ili choo hicho kijengwe na kukamilika Januari 2020.

Jitihada za kumpata Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kuzungumzia uamuzi huo wa Sabaya zinaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ndogo anahangaika na mtu aliyekwisha kumdharau tangu siku ya kwanza anfika Hai.
 
Taratibu za FEDHA hizo pengine hazijafuatwa. Lkn matumizi ni sahihi. Laki 5 kwa kila kijiji zisingefanya kitu.
 
Sasa kila Kijiji laki tano..zingefanya kazi gani..au kuonga ulabu?
Kazi nyingi za vijijini ni za kujitolea kwa wananchi kutumia nguvu zao, kwa hiyo hizo fedha zingeweza kuwasaidia wananchi kumalizia pale walipoishia au wangeweza kununulia hata chai ya kuwatia nguvu wakati wanaendelea na majukumu yao ya kujitolea katika kazi zao za kujenga taifa.

Si ajabu ukakuta hata hizo milioni saba zilizotolewa kwa ujenzi wa choo hazitafanya kazi hiyo, utakuta sehemu kubwa itafanywa na wananchi na sehemu ndogo sana ndo itamalizwa kwa kutumia hizo fedha na zingine zitawarudia wenyewe wanaojifanya kuzitoa na siku hizi upigaji umebadilika watu hawapigi kama zamani, siku hizi wanapiga kwa kupitia kwa wakandalasi.
 
Kwa nini anachukua fedha za jimbo siatumie hela za mfukoni mwake?.
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC) mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, Lengai Ole Sabaya, amezuia Sh. 42 milioni za mfuko wa Jimbo la Hai na kuagiza kati ya fedha hizo Sh. 7 milioni ziende kujenga choo cha walimu wa shule ya msingi Mijongweni iliyopo kata ya Mnadani wilayani humo.

Fedha hizo za mfuko wa Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge wake, Freeman Mbowe kupitia tiketi ya Chadema, zilikuwa zigawanywe kwa kila kijiji ambapo katika mgawanyo huo, kila kijiji kingepewa Sh. 500,000.

Hata hivyo, Sabaya amesema leo Jumamosi Desemba 28,2019 kuwa ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, Yohana Sintoo, kutoa Sh. 7 milioni na kuzipeleka katika shule hiyo na amemtaka awe amezikabidhi Jumatatu bila kukosa.

"Nimemuagiza DED (Mkurugenzi) atoe Sh7 milioni kati ya Sh42 milioni za mfuko wa Jimbo nilizozizuia ziende kutatua changamoto ya choo kwenye hiyo shule na amenihakikishia zitaenda Jumatatu," amesema Sabaya.

Shule hiyo haina choo cha walimu kwa miaka 10 sasa na walimu wamekuwa wakijisaidia katika choo cha Zahanati iliyopo jirani na shule jambo ambalo Sabaya amesema halikubaliki na ndio maana ameelekeza sehemu ya fedha za mfuko wa Jimbo ziende huko.

Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Hai kupitia kwa mkurugenzi wake Sintoo imekabidhi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya kuanzisha mchakato huo na ndipo Sabaya alipoingilia kati ili choo hicho kijengwe na kukamilika Januari 2020.

Jitihada za kumpata Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kuzungumzia uamuzi huo wa Sabaya zinaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipo katika jimbo linaloongizwa na mbunge wa CCM. Shule nyingi hazina vyoo mbona sijasikia DC kubadilisha fedha za mfuko wa mbunge?
Naamini DC Sabaya anataka kumchonganisha Mbowe na wapiga kura wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa kina Ole Sabaya ni aina ya Viongozi wanaoweza ku-survive kwenye Awamu hii ya Tano tu!
Wanaongozwa na mihemuko tu bila kufikiri lolote ktk utendaji wao!
Yeye anadhani kupambana na Mhe.Mbowe (Mbunge) ndiko kutamjenga kiuongozi !
Kuna haja ya viongozi kupewa semina kuhusu majukumu na mamlaka waliyonayo!
Pia vijana hawa sampuli ya huyu Ole Sabaya wajitahidi kujiendeleza kielimu hasa katika nyanja ya Sheria.
Kiongozi mwenye maarifa hawezi ku- vibrate kama huyu kijana ambaye namuona kil.aza na limbukeni sana wa madaraka.
Angalia hata jinsi alivyo- forge kitambulisho kuwa ni Afisa Usalama undercover !
 
Kama amezielekeza kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuna ubaya gani?!
Hazimhusu hizo pesa na mwelekeze atafute fedha kutoka vyanzo vingine! Aache kuivunja taratibu na Sheria zilizoanzisha mifuko ya majimbo kwani atasababisha vurumai zisizo na lazima!
 
Mwenye maamzi na zile fedha ni nani???? Busara ninayoiona mimi ili kuwepo na balance of change mh. Mbowe angeshirikishwa kwenye hilo ili kujenga mtazamo wenye kufanana maana suala la choo ni huduma mhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi sana! Ila pia nionacho hao wawili wana mitazamo na malengo tofauti sana! Ilikuwaje Mfuko huo utoe laki 5 kwa kila kijiji? Laki tano zifanye nini kijijjini? Hiyo ingepelekea viongozi wa vijiji kuzigawana tu maana haziwezi hata kuweka sakafu ya darasa moja!

Mgao wa aina hiyo nauona kama kujitangaza bila malengo ya maana. Bora kuigilia mgao na kuwajengea waalimu choo.
 
Hazimhusu hizo pesa na mwelekeze atafute fedha kutoka vyanzo vingine! Aache kuivunja taratibu na Sheria zilizoanzisha mifuko ya majimbo kwani atasababisha vurumai zisizo na lazima!
Hayo mambo ya hazimhusu ndo yamefanya watu kuziendeshea miradi binafsi na kuwaacha wananchi bila msaada. Ukiona busara iliyotegemewa haitumiki, zuia sheria isiendelee. Sheria inatakiwa iwe na akili.
 
Kweli Mbowe ni kibaka sugu

Back
Top Bottom