DC Simalenga analengwa na nani? Tuhuma dhidi yake za kumpiga mwanafunzi zinatia mashaka sana

DC Simalenga analengwa na nani? Tuhuma dhidi yake za kumpiga mwanafunzi zinatia mashaka sana

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Siamini na nitakuwa wa mwisho kuamini kioja hiki kwamba DC amemnasa kofi mwanafunzi mpk akajeruhiwa.

Yaani kofi limejeruhi kiasi kwamba nusu ya uso wa mwanafunzi umebandikwa pamba? Tangu lini kofi likajeruhi kama panga??

Nimeangalia mara 5 clip ya "anayedaiwa kuwa mwanafunzi aliyejeruhiwa". Kwa kuwa nilisomea Cuba nimebaini yafuatayo yanaweza kuwa kweli;-

(a) Anayedaiwa kuwa mwanafunzi wala siyo mwanafunzi. Ni mhuni fulani tu toka mtaani. Namna anavyoongea hana soni.

(b) Anayedaiwa kujeruhiwa hana jeraha ndiyo maana hasikii maumivu yoyote. Ukiangalia ukubwa wa pamba iliyobandikwa usoni unaweza kukadiria ukubwa wa jeraha na wingi wa maumivu. Lakini vyote hivyo havionekani kwa huyo "mwanafunzi". Kwahiyo huyo msichana kwa hisia zangu hana jeraha. Kama unabisha mwambieni aondoe hiyo pamba usoni.

(c) Kuna magazeti 4 yameandika habari hii kinazi sana kurasa za mbele. Hii inaashiria magazeti haya yamenunulowa na anayemlenga Simalenga.

Chochote kinawezekana awamu hii. Uhuni wa kusagiana kunguni na kupakaziana ili watu wapoteze nafasi zao unarudi kwa kasi Sana (kama enzi za mzee Kikwete).

DC Simalenga kwa 80%analengwa na wabaya wake. Kama mnabisha pamba itolewe usoni kwa huyo mtoto ili tuone jereha lake.

IMG-20221207-WA0026.jpg
 
Nakubaliana na point zote za mtoa mada, mara ya kwanza natizama hii Video, nikasema huyu Binti ni Kicheche flani hivi!
Hapo kwenye ukicheche ndy shida ilipoanzia.

Lipo jambo la msingi alilopigwa huyo binti,
Na Sio kama walivyotuaminisha mitandaoni sababu ya kipigo chake.
 
Upatikanaji wa hawa watu ndio tatizo linaaza hapo!

Wengine huchukuliwa mtaani na kupewa U DED tofauti na zamani ilikuwa ni upandaji madaraja.

Sasa kama wahuni wanapewa ofisi za Umma unatarajia nini!
 
Chochote kinawezekana awamu hii. Uhuni wa kusagiana kunguni na kupakaziana ili watu wapoteze nafasi zao unarudi kwa kasi Sana (kama enzi za mzee Kikwete).

DC Simalenga kwa 80%analengwa na wabaya wake. Kama mnabisha pamba itolewe usoni kwa huyo mtoto ili tuone jereha lake.
Mbona umeandika kama wewe ndie simalenga mwenyewe?
Ulichofanya simalenga ni uhuni wa kiwango cha lami, hukafaa kabisa hata kuwa mjumbe wa mtaa!
 
Mbona umeandika kama wewe ndie simalenga mwenyewe?
Ulichofanya simalenga ni uhuni wa kiwango cha lami, hukafaa kabisa hata kuwa mjumbe wa mtaa!
Amezikana tuhuma zote mkuu. Mm jnimeyoka kuhojiana naye kabla ya kuandika mada hii
 
Siamini na nitakuwa wa mwisho kuamini kioja hiki kwamba DC amemnasa kofi mwanafunzi mpk akajeruhiwa.

Yaani kofi limejeruhi kiasi kwamba nusu ya uso wa mwanafunzi umebandikwa pamba? Tangu lini kofi likajeruhi kama panga?...
Ni mara ngapi umesikia mtoto amekubali kuumizwa ili asingiziwe mtu mwingine!. Na adanganye kuwa kitendo hicho kimefanyika sehemu ya wazi yenye watu wengi tena uwanjani!.

Jiuze kwanini tunasikia tu watu wanao laani kitendo alichokifanya DC, kwanini hawajitokezi wengine waliokuwepo uwanjani wakasema ukweli tofauti na huo unaosemwa na mtoto huyo aliyeshambuliwa?.
 
Siamini na nitakuwa wa mwisho kuamini kioja hiki kwamba DC amemnasa kofi mwanafunzi mpk akajeruhiwa.

Yaani kofi limejeruhi kiasi kwamba nusu ya uso wa mwanafunzi umebandikwa pamba? Tangu lini kofi likajeruhi kama panga??

Nimeangalia mara 5 clip ya "anayedaiwa kuwa mwanafunzi aliyejeruhiwa". Kwa kuwa nilisomea Cuba nimebaini yafuatayo yanaweza kuwa kweli;-

(a) Anayedaiwa kuwa mwanafunzi wala siyo mwanafunzi. Ni mhuni fulani tu toka mtaani. Namna anavyoongea hana soni na anaonekana ametumika sana kwenye 6 kwa 6.

(b) Anayedaiwa kujeruhiwa hana jeraha ndiyo maana hasikii maumivu yoyote. Ukiangalia ukubwa wa pamba iliyobandikwa usoni unaweza kukadiria ukubwa wa jeraha na wingi wa maumivu. Lkn vyote hivyo havionekani kwa huyo "mwanafunzi". Kwahiyo huyo msichana kwa hisia zangu hana jeraha. Kama unabisha mwambieni aondoe hiyo pamba usoni.

(c) Kuna magazeti 4 yameandika habari hii kinazi sana kurasa za mbele. Hii inaashiria magazeti haya yamenunulowa na anayemlenga Simalenga.

Chochote kinawezekana awamu hii. Uhuni wa kusagiana kunguni na kupakaziana ili watu wapoteze nafasi zao unarudi kwa kasi Sana (kama enzi za mzee Kikwete).

DC Simalenga kwa 80%analengwa na wabaya wake. Kama mnabisha pamba itolewe usoni kwa huyo mtoto ili tuone jereha lake.
Wasaalam Watanzania; Taarifa hii nimeiona. Kama Waziri mwenye dhamana ya Watoto, tayari nimeshatuma kikosi cha maafisa ustawi wa mkoa waniletee taarifa ya tukio hili kisha nitakuwa kwenye nafasi ya kusema chochote kwa utaratibu stahiki. Hivyo, tuvute subira. Ahsanteni. [emoji1241] [emoji1488]
 
Back
Top Bottom