DC Simalenga: Yule binti hakupigwa kama inavyosimuliwa, nilimpa warning. Nilitaka kumpiga nikamshika Mkono akaomba Msamaha!

DC Simalenga: Yule binti hakupigwa kama inavyosimuliwa, nilimpa warning. Nilitaka kumpiga nikamshika Mkono akaomba Msamaha!

Shuleni wanafunzi hawachapwi?
Wanachapwa na walimu sio nje ya hapo. Yaani hapo kakiri kuwa alikusudia kutenda kosa akaombwa msamaha na bahati mbaya yeye hajashtuka kuwa amekosea.
Hivi ikiruhusiwa viongozi wachape si itakuwa balaa. Waziri mkuu anamtia kerebu DC, DC anawatia bakora machinga.
Ila mkuu kama wewe waona ni kawaida sitoshangaa maana TZ raia mshazoea mambo kwenda hovyo hata nje ya kanuni na sheria kisa tu ni mazoea
 
Hivi unaruhusiwa kupiga? Tuliosoma Cuba tushaelewa ,wewe simalenga subiri tu report itoke hurudi zako kaole ukaendeleze usanii.
Kuchagua vijana wa hovyo ndio matokeo yake. Sijui alikula maharage ya wapi. Fatuma Karume amwekee mikono apate haki yake huyu mtoto kaumizwa
 
DC akatoa JUKUMU!
akagawa MAJUKUMU, Pole binti lakini huyu binti anaonekana mkaidi LAKINI HAKUSTAHILI KUPIGWA!

Yamkini ALMHOJI DC Kwa ujasiri MBONA unatufukuza WAKATI NA SISI NI WATU!
DC akapaniki kutoheshimika! Ni JAZIBA TU mtoto nasikia katibiwa na wazazi wamepewa kifuta machozi YAMEISHA
Ila huyo binti ni NUNDA kupitia virtual expression, ni vile vinunda vinavyojua kujitetea
 
Kama DC katoa warning kampasua binti jicho,
Je angempiga ?
Binti angekuwa ktk hali gani..


Uetetezi mwingine hovyo kabisa.
Mjinga sana,hata kuongea hajui.......hivi hawa jamaa wanaokotwa kwenye madampo nini? Yaani ni aibu sana
 
Kwa nini alitaka kumpiga na alitaka kumpiga kama nani....!?

Lazima kulikuwa na witness wengi tu, hivyo kama hawatatishwa ukweli utajulikana. Yaani kitendo cha yeye kushika mkono tena mtoto wa kike... Yaani ni kosa kubwa sana.

Hiki kiburi cha Wakuu wa Wilaya toka enzi za JPM inabidi kidhibitiwe. Nakumbuka akina Chalamila waliwahi piga watoto wa watu halafu kuna watu wakawa defend. Sasa haya ndiyo matokeo yake.

Enzi za JK kuna Mkuu wa Wilaya alimtandika viboko mwalimu wa shule ya msingi.... Kikwete alimtimua kazi kesho yake.

Sitashangaa kusikia ana negotiate dau ili atoke salama. Kwa hiyo matokeo ya uchaguzi nafikiri tayari yameshajulikana.
Kiukweli hii tabia iliota mizizi kipindi cha JPM sasa bado wanadhani wapo utawala wa gizani.

Mkuu wa wilaya hana mamlaka ya kumpiga ama kumwadhibu mtu kwa namna yoyote ile.

Anakana kumpiga huku akikiri alitaka kumpiga. Kwa uelewa wa haraka haraka ni kweli alimpiga ndiyo maana binti amevimba jicho.

Achukuliwe hatua stahiki ili iwe fundisho.
 
Wazungu hao unaowasema wa wapi au Buza? Maana kwa mbele ukimpiga mtoto unapewa adhabu kali sana , watoto wa kizungu wanafundishwa hadi kupiga 911 wakipigwa na wazazi.
Acha ujuaji usio kuwa na maana.

Nchi pekee ambayo kuna sheria ya kutopiga mtoto barani Ulaya ni Wingereza tu hakuna nyingine.

Hata Marekani sheria inamruhusu mzazi kumuadhibu mtoto wake pale ana pokosea ila sijajua kwa upande wa shuleni.
 
Back
Top Bottom