DC wa Bariadi adaiwa kushinikiza wananchi kupiga kura ya siri kuwataja wachawi na wenye Fisi

DC wa Bariadi adaiwa kushinikiza wananchi kupiga kura ya siri kuwataja wachawi na wenye Fisi

Kuna mambo hapa nimebaini kutoka kwako;
1. Wewe ni mtu unayeamini mambo ya kishirikina na uchawi, ndiyo maana unaamini watoto wanakufa kwa kurogwa. Kama mtoto kapata malaria kali unampeleka kwa mganga wa kienyeji badala ya Hospitali unategemea nini.
2. Elimu uliyopata haijakusaidia. nilitegemea mwalimu uwe ndo kioo cha jamii na kuielimisha jamii unayokuzunguka
3. kama wewe una zaidi ya miaka 20 huko Bariadi, kwa nini wewe hawajakuloga au hata mke wako na watoto wako hawajauawa na hao wachawi. Maana kama ungekuwa umefanyiwa mambo hayo ungeomba uhamisho siku nyingi
4. kwa kuwa wewe ni mwalimu, tena unayefundisha huko vijijini bila shaka na wewe unalima mazao na unapanda mbegu na kuweka hiyo mizizi uliyoisema ili upate mazao zaidi. kama unafanya hivo basi bado hujaelimika.
Mkuu shida yako nahisi huamini kuwa uchawi upo, ila hata usipo amini hakika uchawi upo.
 
Inakuwaje watu wanafuga fisi, fisi ni hatari sana nasikia hata simba wanawaogopa wakati mwingine, nguvu yao ya kuuma (bite force) ina nguvu kuliko ya simba na chui, akikamata mguu wa binadamu anakula na mifupa yake kama maharage tuu
 
Kwenye utendaji chini kuna mengi wakuu kule chakechake iliibuka ishu ya popo bawa ,wananchi wakawa wanalala nje hospital zikathibitisha watu wameingiliwa ,alichofanya dc aliita waganga wote na alipeleleza wanaodhaniwa wachawi akawaita akasema kwenye kikao kuanzia kesho akilawitiwa mtu mmoja waano natupa jela ,kesho wakalawitiwa wawili akatupa 30 ndan siku ya pili wakaja wenzao wailizia kibabe akawahamishia jela akasema hawatoi hadi popobawa akaome walimwita kisiri wakuhakikishia ,akawatoa na stori hiyo ikaishia hapo.

Kigoma kagunga,walimu walikuwa wanaenda asibuhi wanaamka dalini mara pembeni ya ziwa ,wakawa wanaacha kazi au kukimbia,mkuu wa wilaya alihamiashia walimu wapya 7 akaitisha kikao cha vizee vyote akavichinjia ngombe na pombe ,kisha akawaambia mwalimu yeyote akiripoti tukio kama hilo anaomba wasilaumiane kesho mwalimu mmoja akaamka ziwan ,mkuu wa wilaya alienda na kalandinga akachukua walimu wake akakamata na wake za wazee wale 15 straight jela wakaomba kikao akawaambia wasubiri ziishe siku tatu,wazee walienda hivyo hivyo kumuapia mkuu haitatokea ,wakaenda ziIndika nyumba za walimu wenyewe ,hadi leo walimu wanaishi kwa aman tele tena wazee wanawafata kuuliza kuna lolote mmesumbuliwa .
Haya mambo ya kuongoza jamii za wajinga ngumu sana
 
Siku moja nikiwa shule ya msingi, kiranja mkuu alipelekewa orodha ya wapiga kelele ili aisome mbele ya mwalimu wa zamu ,basi akaanza kusoma majina
Mara akaanza kucheka mwalimu akamuuliza we soma unacheka nn?? Akajibu eti na mie wameniandika
 
Vizuri sana,

Waite na ramba ramba Mbona rahisi tu,

Wacha waumbuke hao waharibifu wa maisha ya watu!

Mtu asiyetaka mwenzie awe na afya njema, awe na kucheki, avae tenge lake wa nini ?!

Uchawi ni adui wa maendeleo.
 
Mpaka Neno la Mungu limeruhusu mchawi kuuawa bila shaka Mwenyezi Mungu anafahamu kuwa uchawi ni mbaya kupita kiasi.


Imeandikwa;

“Asiachwe mwanamke mchawi kuishi “
 
Halafu ubaya wa dhambi ya uchawi huenda Kwa kurithishana toka kizazi hadi kizazi ,

Tofauti na dhambi nyingi hazirithiwi labda iwe coincidence tu.
 
Mtaa-Nyangaka (mjini bariadi) hata mimi nilishangaa Sana, badala ya kusisitiza wananchi waondoe vichaka na kupuluni miti na kukwangua barabara, anaongea Mambo chonganishi, Sasa watu wakianza kukatwa mapanga kwa sababu ya uchawi sijui tena atasemaje?
Huu ni ujinga na hii ni aibu kwa Mamlaka za uteuzi namna wanavyopata Viongozi wake.
 
MADAI
Kutokana na kukithiri kwa matukio ya fisi kuua watoto na watu mbalimbali Bariadi inadaiwa Mkuu wa Wilaya wa eneo hilo aliitisha kikao kwa ajili ya kufanya oparesheni ya kuangamiza fisi hao.

Sambamba na hilo inadaiwa Tarehe 22/04/2022 katika mtaa wa Mangaka aliitisha kikao kwa njia ya Mwano (kupiga yowe ili wananchi wakusanyike) na kuwatuhumu wananchi kuwa baadhi yao ni wachawi na kwamba fisi wao wanajeruhi na kuua watu katika mtaa huo. Alieleza kuwa anataka kuwakamata wachawi wote na kuwashughulikia kwa kuwa wanawatuma fisi wao kwenda kuua na kula watu.




1657980287208.png
 
Back
Top Bottom