DCI Boaz vipi, Mbona amekimbia kesi ya Mbowe?

Wewe ndiye umefanya concise analysis. A well reasoned one! Hata Samia atakuja kujibu maswali, Tena huyo Ni shahidi muhimu maana anagahamu kesi nzima ya ugaidi mpàka Mbowe kufungwa! Itakuwa aeleze Mbowe alifungwa lini kwa kesi ipi
 
Kama ndivyo,ndugu yetu Sirro naye ajipange.
 
Hangaya alijifanya ana akili kuliko mwendazake, mwisho wa kesi hii ndio mwanzo wa anguko la kasi la ccm.
kauli ya umma sio chokochoko.
Hivi mnapozungumzia "umma" huwa mnamaanisha nini aisee, huenda mie sielewi, ni huu umma unaomtukana JPM kila uchao mitandaoni? embu nendeni site mkamtukane ndo mjue nini maana ya umma.
 
nikisikia mwana ukoo kawa ccm naomba kabisa kumfuta jina la ukoo.asije kutuzalia wapuuzi kama ziro na ccm
 
Serikal huwa inapoteza sana tu. Tofauti ni kwamba watuhumiwa watakaa muda mrefu sana hadi serikal ije ikubali kunyanyua mikono juu si leo
No mpaka hapa serikali imehadhirika vya kutosha. Kumbuke wako jela miezi mitano. Ni mingi Sana hii.
 
Mpelelezi hajui hata maana ya Triangulation katika kuidentify estimated location of mobile phone/user .... maajabu ya wapelelezi wa mchongo na serikali inaona bado ni bora kuajiri form four failures.
 
Ukweli ni kwamba baada ya Mbowe juzi kwenda pekee yake ofisi ya jaji pamoja na mawakili wa pande zote ndio hii kesi ilipoenda kumalizwa!!!
Juzi jumapili?
Aisee, kumbe Tz watu wanachapa kazi mpaka jumapili?safi sana
 
Watafungwa kwa Kosa Lipi?
 
Angebanikwa kama wenzetu wanavyombanika samaki nchanga🤔.Nasijui angeokolewa na nani kwenye kubanikwa huko🏃.
 
Ukweli ni kwamba baada ya Mbowe juzi kwenda pekee yake ofisi ya jaji pamoja na mawakili wa pande zote ndio hii kesi ilipoenda kumalizwa!!!

Exactly, kile kitendo cha kwenda kuonana na jaji pembeni nilijua kabisa jaji anakwenda kuweka ukweli wa serikali ambao Zito alitumwa ukafeli. Simply kesi iliisha ile ile jana baada ya serekali kuona aibu ya wazi.
 
Lile tukio la jana la Mh. Mbowe kulalamika kuhusu kunyimwa chakula yeye pamoja na wenzake, jambo likitokea huku Mh. Rais akiwa bado yupo Europe, na tena katika kipindi ambacho balozi mbalimbali za nchi za EU zikionyesha dhahiri kuwa zipo "interested" juu ya kesi hii ya kigaidi.

Pengine hii ndiyo sababu kubwa ambayo imepelekea serikali ikubali mashaidi wa upande wa mashtaka waishie kuwa 13 tu badala ya wale 23 ama 24 ambao walikwisha kuwaandaa. Ushahidi wa Urio na Swila ndiyo ambao ulikuwa muhimu mno katika kujenga msingi wao wa mashitaka.

Kubomolewa kwa misingi hiyo na upande wa mawakili wa utetezi ndiyo imekuwa sababu ya kufanya kidali "po" kwa kuwa endapo DCI Boaz angeletwa kutoa ushahidi ingekuwa fadhaa kubwa kwa upande wa serikali. Kwenye "cross examination" asingeweza kuchomoka katika ku "discharge burden of proof" ili kuwaweka watuhumiwa hatiani.

Mh. Kibatala na timu nzima ya mawakili upande wa utetezi, mnapaswa kupewa kongole nyingi sana. Kwa hakika mmeitendea haki fani ya sheria katika kusimamia kwa weledi mkubwa haki za kisheria.
 
Wamejikuta hawana mashahidi
 
Wamesitisha kesi kabla hawajathibitisha llosa la ugaidi
 
Endapo Kesi hii itamalizwa kwa njia hii, basi Kibatala atakuwa celebrity wa sheria baada ya Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…