DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
Ukiwa hoi kibiashara huwezi kuwa na bastola?

Ukikubalika sehemu ndio inakuzuia kufanya uhalifu?

Kwa maoni yangu, utetezi wako doesnt hold water.,
 
Naona DCI Manumba hajaeleza kama Hamza aliwahi kusafiri nje ya nchi na kupata mafunzo mbalimbali iwe ya kidini au matumizi ya silaha.
 
Aliwezaje kujenga ofisi ya chama chetu pendwa kwa pesa yake ya mfukoni kama hakuwa na ukwasi.
 
Tuwe wakweli ugaidi hauna chama.

Hivyo uchunguzi uliofanywa na polisi ambao kimsingi ndio wataalamu lazima uheshimiwe.

Kwamba kwa sababu Hamza ni mwanaccm basi hawezi kuwa gaidi hiyo siyo sahihi kabisa.

Tuwaache polisi watimize majukumu yao ya kikatiba.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Watanzania sio wajinga.

Watu wa Chunya huko Makongorosi walikuwa wanamkubali Hamza. Aliahidi kujenga shule, aliajiri watu kibao.
Ahadi hewa? Tuwekee picha za hao watu kibao aliowaajiri uliwaona? ukiambiwa thibitisha mahakamani? tuwekee picha yao wote kibao hapa
 
Hivi polisi wamefanya uchunguzi,,au wame-hypothesize tu...Watuambie affiliated na kundi gani la kigaidi?au wamekuta video ya kikundi gani kwenye simu yake
 
Polisi wajitafakari upya kazi imewashinda alichofanya DCI ni kuchukua umbeya wa mitandaoni na kuurasimisha.
 
Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.
Hapa mleta mada ujapafafanua vizuri nadhani kuna vipande umeviruka. Kweli msemaji katoa maelezo kiurahisi hivi!? Kwa sababu maelezo haya yanaibua maswali lukuki!
 
Nimecheeekaaaaaah daaaaaaah!
Polisi wetu bana, sawa zile STORY za kitu chenye ncha kali hawawezi kuziacha!
Jambazi akafariki akikimbizwa hospital!
Salute

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hao polisi waache propaganda, huyo kaua watu waliompora dhahabu zake alipeleka sokoni, sasa mbona hakuua raia.

Sisi tunaojitambua tunaelewa hivyo na wala hizo propaganda feki za polisi haziwezi kubadilisha mindset zetu.
 
Magaidi wa Tanzania wana sifa tofauti na wa nchi nyingine. Hizo taarifa ingekuwa vizuri wakashare na mataifa mengine kuisadia dunia njia mpya ya kuwa profile magaidi.... Yaani hapa tumewazidi FBI na Scotland Yard. Wambura inabidi kwa hili apewe tuzo la kimataifa. Magaidi wawili TZ wenye vigezo tofauti na magaidi wengine duniani.
Anakuambia eti swala la kudhulumiwa madini sio kweli kwasababu walikumkuta hana madini yoyote eneo la tukio baada ya kumuua 🤣
 
Tunaliomba Jeshi la Polisi pia lifuatilie nyenendo za viongozi wa Chadema na baadhi ya wafuasi wake ambao kimsingi walifurahia sana kitendo cha Gaidi Hamza kuwauwa Askari wetu.
hii inathibitisha kuwa viongozi wa Chadema na baadhi ya wafuasi wao wana kila dalili za kujihusisha na vitendo vya Kigaidi ndio maana walifurahia vitendo vilivyo fanya na Hamza.
ni muhimu sana wafuatiliwe popote pale walipo ktk kila kona ya nchi hii.
tusowafuge wala kuwalea.
nasisitiza tena Jeshi la Polisi kamwe lisivumilie vitendo vya viongozi wa chadema na baadhi ya wafuasi.
Ndugu wa shujaa Hamza warejeshewe dhahabu zilizo porwa na mapolisi, tuanzie hapo.
 
Haya kawaeleze Wanaccm wa Nzega kabla Husein Bhashe hajafanya yake.

Hao mapolisi wanaoua raia ni wasomali??
Umelewa? Hiki ulichoandika kinahusiana nini na comment yangu? Ujinga ni kudhani kila mtu ni shabiki wa mambo ya vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom