Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mimi nimeshangaa sana kuhusu hilo, mimi mwenyewe amenishawishi hadi nimeenda kuutafuta huo mtandaoDCI ameamua kuutaja na mtandao unaotoa mafunzo ya Ugaidi kabisa ili wanaotaka kujifunza na walikuwa hawajui wapate access. Kosa kubwa
Hayupo tena ili hata atoe maelezo huru,tena hivyo maelezo yoyote yanamfaa.Kumbe tunaweza tu kuchunguza kwa muda mfupi hata siku 10 sasa yale mambo ya kesi mwaka mzima uchunguzi unaendelea yanatoka wapi?? Huyu bado kafa lakini wamejuwa yote hayo nawapa hongera lakini mengine mbona mashahidi wapo wazima lakini kila leo uchunguzi haujakamilika. Kazi nchi hii...
Si wabambikiaji walishaanza hata kabla hayo kutokea.Hakuna atakae shangaa kwani ni moja ya dhamira za kubambikia.Tunaliomba Jeshi la Polisi pia lifuatilie nyenendo za viongozi wa Chadema na baadhi ya wafuasi wake ambao kimsingi walifurahia sana kitendo cha Gaidi Hamza kuwauwa Askari wetu.
hii inathibitisha kuwa viongozi wa Chadema na baadhi ya wafuasi wao wana kila dalili za kujihusisha na vitendo vya Kigaidi ndio maana walifurahia vitendo vilivyo fanya na Hamza.
ni muhimu sana wafuatiliwe popote pale walipo ktk kila kona ya nchi hii.
tusowafuge wala kuwalea.
Mimi nimeutafuta ila nimekosa. Wewe umepataje?Hata mimi nimeshangaa sana kuhusu hilo, mimi mwenyewe amenishawishi hadi nimeenda kuutafuta huo mtandao
Sina Mashaka na DCI ila bado najiuliza uliza Gaidi gani anaeua Polisi peke yake, na je wakati anatoa misaada ya kibinadamu mbona hakuitwa gaidiMkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.
Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.
Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.
"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.
Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.
"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.
Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.
"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.
Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.
Chanzo: Mwananchi
Police wanajidanganya wenyewe kwa sababu wananchi wanajua. Wengi husema wanajitekenya na kucheka wenyewe. Wawaulize wakazi wa Chunya na Upanga wapate ukweli.kama ni kweli alikuwa mfanya biashara wa madini kwa uzoefu wangu wengi huwa wanajifunza matumizi ya kutumia silaha sababu ya nature ya kazi yao,pia hawa wenzetu asili ya kisomali wengi wanahobi ya uwindaji
Kwahiyo sasa tuelewe kuwa ndani ya lumumba kuna chuo cha ugaidi?Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.
Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.
Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.
"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.
Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.
"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.
Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.
"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.
Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.
Chanzo: Mwananchi
Ndiyo maana mabalozi wa nchi za nje kila ikitajwa kesi ya mh Mbowe wanajitahidi kuwepo mahakamaniTaarifa hizi zifike kwa mabalozi wote kuwa Tanzania kwasasa ni sehemu hatarishi kwa Ugaidi.
Huyu Kamanda ni muongo tena uongo wake ni wa kiwango cha Tozo za Tanzania, hivi jamani Gaidi gani ambae hataki kuuwa Raia anataka polisi tu??? Tutizame hao IS walvyo wanataka public ya watu ili wajitoe muhanga na kuwauwa watu wengi, Hamza anaonekana katika video hanaa time kabisa na Raia jambo ambalo magaidi hawalifanya hata siku 1, Polisi wasema ukweli kwanini hakuwabali kwamba baadhi yao wamekuwa si waaminifu na kumdhumu huyo hamza? Mazingira yote yanaonesha hamza alikuwa akilipa kisasi kwa polisi na si kwamba gaidi...tafsiri ya gaidi atupe kamanda kisha aseme upumbavu huu tena. Shame!Hawa Polisi si wa kuwaamini kabisa.