DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
Natoa ushauri kwa vyombo vya Polisi kwamba viimarishe Intelijensia yao dhidi ya Wanachama wote wa CCM.

We never know huenda kuna magaidi zaidi ndani ya Chama pendwa!
Hata hivo uchunguzi wo wote ambao umefanyika wakati marehemu hayupo una acha maswali.

Kama marehemu alikuwa kwenye mitandao ya vikundi vyenye misimamo ya imani kali,basi huenda angeingia makanisani na kuanza kuua wakristo! Lakini Polisi?
Hao nao wasikwepe ujambazi wao, akina Zombe hata baada ya walioiba zile pesa za BIDCO kujitokeza Bado hawakusikilizwa, Ila wamewaponza ambao hawakukwapua mali za Hamza kuuawa.
 
Huyu chini ya Sirro ni bumunda tu , mana wooote wanaonekana hawana akili hata moja, ugaidi unajifunzia mtandaoni, embu oneni aibu jamani
 
Hao wandishi wa Habari waliluhusiwa kuuliza maswali kwa kamanda?
 
Aisee siwez kubisha sana..lakini kwa Mtanzania tu aliyekulia katika mazingira ya kitajiri hawez kuwa anajua kushika bunduki vile na kujiamini kiasi kile kwa umri ule...palikua na namna..na inawezekana kabisa ametuma salam kwa wenzake..inaweza kuwa mwanzo wa ugaid tanzania au mwisho wa ugaid inategemea tu na vyombo vya usalama vitakavyolimaliza hili
Naomba ndugu usidanganyike na propaganda za IGP Sirro na Wambura!!
Hawa jamaa wanataka kupoteza lengo. The question is: WHY POLICEMEN ???.Kuna madai ya Hamza kudhulumiwa MADINI YAKE YA DHAHABU na mapolisi mbona hili halisemwi??
Kama ni swala la Ughaidi Hamza Angelienda Soko Kuu Kariakoo akajilipua ili auwe wengi na yeye afe!!
Lakini Hamza ALIWA LENGA POLISI !! Hii ina maana kwamba kulikuwa na mgogoro kati ya HAMZA NA MAPOLISI!! Try to think out of the box please!!!
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Mama samia Rais wangu unda tume huru alichosema Dci ni uwongo mtupu! Hivi gaidi anachagua mtu, si angemaliza kwanza raia waliokuwa karibu naye. Wambura ni wazi kabisa na anapaswa kuondoka. Mama unda tume utaona ujangiri na ujambazi waliofanya Polisi
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Mhu!
 
Ushauri wangu mfupi kwa hili jeshi la polisi ni kwamba..Dunia hii na hasa kizazi hiki ni kizazi kilichochangamka sana kiakili...na hii imechangiwa sana na mabadiliko katika Sayansi na Technology hivyo basi njia pekee itakayolisaidia hili Jeshi ni kubadili vigezo vya watu wanaokuwa recruited na kuchukua watu waliofanya vizuri kwenye masomo yao na sio waliofeli.
 
Kama wanaamini na kutoa taarifa kuwa Hamza ni gaidi basi kuna hatari ya uwepo wa sleeper cells Tanzania...

Na kitendo cha 'gaidi' mwenzao kuuawa, kitawaamsha wengine kulipiza kisasi...
 
Gaidi wa kujitoa mhanga,
Halafu anaua polisi tu,
Dah ajabu na kweli,
Kumbe unaweza kujifundisha kutumia banduki kupitia mitandao aisee kweli Teknologia iko advance
 
Back
Top Bottom