DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
Tanzania ina asili ya kukandamiza waislamu, sishangazwi kuona serekali ikiwa na hamu ya kuwa na ugaidi. Maelezo ya mpelelezi yana kasoro na yana huge gap, ameshindwa kutueleza kitu kinaitwa motive ya Hamza.

Magaidi wote duniani wana motivation na mara zote ni za kisiasa, kiuchumi n.k. Sijafahamu chochote na kiengereza uchwara cha mpelelezi wetu.
Ndo hicho kashindwa kutuambia,nini kilimskuma kuchukua hayo maamuzi na zaidi kuwalenga askari polisi tu. Na pia amesema biashara zake zilikuwa ameshaacha zamani,je wamechunguza kwanini ziliisha? Mimi napendekeza chombo cha uchunguzi wa makosa ya jinai kingejitegemea kisiwe ndani ya taasisi nyingine ili kiwe huru.
 
KamaHamza ni gaidi, watu wa karibu naye, nao wakamatwe. Kuna picha tumemwona akiwa na Polepole
 
Jeshi la Polisi la Tanzania, kwa ujumla halina uwezo wa kufanya uchunguza.

Halijui kuchunguza hata vyanzo vya ajali barabarani, sembuse ugaidi? Jeshi la Tanzania, kila ikitokea ajali barabarani, utasikia kuwa chanzo cha ajali mara ni mwendo kasi au tairi lilipasuka. Upuuzi mtupu! Nani alikuambia kuwa kila ukienda kasi unapata ajali? Hawaendi mbali zaidi ya kuangalia matokeo badala ya kutafuta visababishi.

Kwenye uchunguzi, jeshi la polisi ni zero. Wanapotoa taarifa za uchunguzi, unagundua kabisa kuwa hawa watu hawana mafunzo yoyote kwenye investigation.
Wapatie wew mafunzo ya uchunguzi maana unaonekana umebobea ktk eneo hilo mkuu

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Menye darubini za kuona mbali naomba nizikodi kwani nimeamua kupiga kambi Kokobichi, najua Kokobibi panafaa sana kuangalia baharini mahali magaidi wanapoingilia.
 
Safi sana. Sasa ni dhahiri miongoni mwa viongozi wa ccm ni magaidi wa kujitoa mhanga
 
Kuna kazi maalum aliyopewa Hamza na lile kundi lililoratibu kesi ya Ugaidi Kwa Mbowe. Hamza kakosea au kaamua Kwa makusudi kutekeleza tofauti na makubaliano yao. Polisiccm sio wakumuamini hata kidogo.

Tujiulize kwanini tukio lile linalosenwa na Polisi ni la kigaidi lilifanyikia mbele ya ubalozi wa Ufaransa?? Tujiulize pia kwanini Polisi hao hao wameshindwa kufanya uchunguzi dhidi ya shabulio la Mh Lissu? Wakati ule walisema hawakupewa ushirikiano na Dereva wa Mh Lissu. Je ni nani aliyewapa ushirikiano kwenye tukio la Hamza??

Polisiccm endeleeni kujianika mkishakauka tutawaanua.
Wao ni watuhumiwa alafu wanajichunguza? hatari sn
 
Polisi ni waongo sana, ile video baada ya Hamza risasi kuisha alinyoosha mikono, kwa askari wenye mafunzo kama ambavyo huwa wanajitapa, wangeweza kumkamata mzima mzima... cha ajabu waliendelea kulenga hewa tena wapo wengi... yaani ni aibu..
Wangemkamata na kumhoji, lakini walikuwa na nia ya wazi kupoteza ushahidi... wakaamua kummaliza

Askari hata shabaha hawana, kaanguka chini bado kwa uoga wakaendelea ku shoot kama hawaamini vile...

Yaani Hamza ukitizama alikuwa highly trained na umakini sana, angekuwa na magazine za kutosha angewalaza sana kwa sababu ya ujinga... lile askari lingine linafikiri sifa kusogea karibu na hatari kiasi kile... yaani ni vituko vitupu...

Hivi hawa polisi wana shida gani
Lile lilitaka kuleta mambo ya kwenye Movie, alafu linakimbia limemgeuzia mgongo adui, sijui waliliokota wapi lile li afande
 
kumbe unaweza kujifunza kutumia SMG kwenye mtandao na kulenga shabaa bila mazoezi. mlio wa SMG kama hujauzoea huwezi kusimama. inawezekana sawa gaidi ila sio wa kujifunzia kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom