DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
kweli alikuwa gaidi kwa uchunguzi ulio ona vip hujatuambia bastola alitoa wapi
pia ailkuwa anaishi kwa siri
kama aliishishi kwa siri ujumbe wa chama fulani aliuupataje? mbona picha na clip zake ziko mitandaoni huo usiri ni upi si mlisema mkazi wa upanga? au ok ngoja tuamini tulio wapa zamana
Tumepigwa parefu mkuu
 
Hilo halina Ubishi.
Hamza alikuwa Gaidi namba 2.
ndio maana karibia wafuasi wote wa Chadema walimtangaza Hamza kama shujaa wao, inathibitisha kuwa Chadema wanaunga mkono kwa 100% vitendo vya kigaidi.
ndio maana hata kuthibitisha kesi ya Mbowe itakuwa kazi nyepesi sana.
huenda Hamza alitumwa na kumtumikia Gaidi namba 1.
 
Kumbe tunaweza tu kuchunguza kwa muda mfupi hata siku 10 sasa yale mambo ya kesi mwaka mzima uchunguzi unaendelea yanatoka wapi?? Huyu bado kafa lakini wamejuwa yote hayo nawapa hongera lakini mengine mbona mashahidi wapo wazima lakini kila leo uchunguzi haujakamilika. Kazi nchi hii...
Huu uchunguzi umekamilika mapema kwa sababu muhusika hayupo, hawana wa kumtesa mahabusu.

Kama angekuwa hai, uchunguzi ungechukua muda mrefu huku magari ya magereza yangeendelea kuharibika ili asifikishwe mahakamani
 
Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM ngazi ya wilaya, Hamza (R. I. P) bado naamini umekufa na siri nzito sana kuhusu kitu kati ya wewe na Jeshi la polisi.
Narudia kutazama ile video clip, kwa hekima anaitazama daladala iliyojaa raia abiria wenye hofu kubwa. Anaiacha, anakwenda katikati ya barabara anaanza kuongoza magari yapite haraka. Anachagua kushughurika na askari tu!

Magaidi Duniani wa kujitoa muhanga wasinge acha ile daladala vile maana njia pekee kwao kutuma ujumbe kwa Serikali huwa ni kuua innocent souls ili mamlaka zipakazwe tope la lawama.

Kesi ya Zombe na wenzake, Tume ya polisi ilikuja na matokeo kwamba wale wafanya biashara walikuwa MAJAMBAZI. Baada ya kelele nyingi ikaundwa Tume Huru ya majaji ikabaini hawakuwa MAJAMBAZI.

Polisi yajichunguza!
Tuliyajua matokeo yake kabla ya uchunguzi kukamilika
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Mambo ya aibu kabisa haya. Yaani jeshi lenye intelijensia ya viashiria vya uvunjifu wa amani kwenye mikutano ya vyama vya siasa. Wana shindwaje kuwajua magaidi hadi wanapo ua polisi?
Halafu sasa wana bishana na marehemu.
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Ndio uawe police? hebu kuweni wakweli kidogo. Kuna shida mahali. Kufunika funuka kombe mwanaharamu apite kwa mambo muhimu kama haya sii mazuri.
 
Kazi kweli kweli huku tunatumia garama kubwa kutangaza vivutio vya utalii, hapo hapo tuna tangaza Nchi ina ugaidi
 
Tanzania ina asili ya kukandamiza waislamu, sishangazwi kuona serekali ikiwa na hamu ya kuwa na ugaidi. Maelezo ya mpelelezi yana kasoro na yana huge gap, ameshindwa kutueleza kitu kinaitwa motive ya Hamza.

Magaidi wote duniani wana motivation na mara zote ni za kisiasa, kiuchumi n.k. Sijafahamu chochote na kiengereza uchwara cha mpelelezi wetu.
 
Huu ubambikaji mpaka kwa maiti isiyoweza kujitetea unashangaza Sana. Wameamua wenyewe kwa vinywa vyao kuuleta ugaidi Tanzania ambao kimsingi haukuwepo.

Makofi kwa DCI
 
Back
Top Bottom