DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
Hapa tumepigwa! Yani mualifu kajichunguza mwenyewe na tutegemee aje na majibu yakuwa yeye alikosea? Mungu awalaze mahali pema hamza na vijana wa Siro..... Wale jamaa wakujitoa muhanga huwa wanatafuta sehemu sehemu yenye wingi wa watu!' sasa najiuliza huyu gaidi hamza kwann alidili na police tu? Manake hapo kuna jambo lazima na police walikuwa kwenye position yakuweza kupiga miguu ili wasipoteze ushahidi!!! Ila naisi kule kumpiga risasi nyingi nikupoteza ushahidi na kama ujuavyo kosa siku zote linakuwa la marehemu.....!!!!
 
Ile intelijensia ya polisi ya fujo kwenye mikutano ya CHADEMA ilikuwa wapi mpaka Hamza akawa gaidi na huku ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya?
Kama kweli Hamza alikuwa ni Gaidi basi hakuwa Peke yake ndani ya Chama cha Mapinduzi. Haingii akilini kuwa mtu anaweza kujifuza Ugaidi kupitia mitandaoni. Hamza alionekana akitumia silaha ipasavyo. Je na Hilo alijufunzia mitandaoni.
 
kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.
Muda mrefu usio kuwa na muda.....na uchunguzi umefanywa..!!!

Mbna vibarua na m/kiti wa kule mgodini alikiri na kusema aliondoka ata mwezi haujaisha....

Uchunguzi wa bongo ni wa makaratasi...
 
Aisee siwez kubisha sana..lakini kwa mtanzania tu aliyekulia katika mazingira ya kitajiri hawez kuwa anajua kushika bunduki vile na kujiamini kiasi kile kwa umri ule...palikua na namna..na inawezekana kabisa ametuma salam kwa wenzake..inaweza kuwa mwanzo wa ugaid tanzania au mwisho wa ugaid inategemea tu na vyombo vya usalama vitakavyolimaliza hili
watu wana pick hizo tabia kutoka kwa marafiki, vikundi, makundi. haijalish umetoka jamii ya kimaskini au tajiri.ball you need ni exposure tu
 
Polisi yasema Hamza alikuwa gaidi aliyeshawishika pakubwa kwa kupitia kutazama na kusoma mitandao!


Pia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

N.B
Nchi zingine kama Rwanda, Kenya na Mozambique vyombo vyao vya usalama wakitoa taarifa hawapepesi macho husema waziwazi kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa magaidi. Lakini taarifa hii ya DCI Camillius Wambura naona anasita kusema au kutaja uchuguzi wao umebaini nini kuhusu nchi zingine kuhusika na kumbadilisha au kumpa mafunzo ya kigaidi Hamza.
 
Aisee siwez kubisha sana..lakini kwa mtanzania tu aliyekulia katika mazingira ya kitajiri hawez kuwa anajua kushika bunduki vile na kujiamini kiasi kile kwa umri ule...palikua na namna..na inawezekana kabisa ametuma salam kwa wenzake..inaweza kuwa mwanzo wa ugaid tanzania au mwisho wa ugaid inategemea tu na vyombo vya usalama vitakavyolimaliza hili
kama ni kweli alikuwa mfanya biashara wa madini kwa uzoefu wangu wengi huwa wanajifunza matumizi ya kutumia silaha sababu ya nature ya kazi yao,pia hawa wenzetu asili ya kisomali wengi wanahobi ya uwindaji
 
Wasomali kujifundisha silaha ni jambo la kawaida kwao,ni kama utamaduni wao tu,hata kwenye harusi zao hua wanapiga risasi juu,kama Wayemen tu,ni sawa na Mzaramu na ngoma.
 
Back
Top Bottom