DCI Wambura: Uchunguzi umebaini Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga
Natoa ushauri kwa vyombo vya Polisi kwamba viimarishe Intelijensia yao dhidi ya Wanachama wote wa CCM.

We never know huenda kuna magaidi zaidi ndani ya Chama pendwa!
Hata hivo uchunguzi wo wote ambao umefanyika wakati marehemu hayupo una acha maswali.

Kama marehemu alikuwa kwenye mitandao ya vikundi vyenye misimamo ya imani kali,basi huenda angeingia makanisani na kuanza kuua wakristo! Lakini Polisi?
 
Jeshi la Polisi la Tanzania, kwa ujumla halina uwezo wa kufanya uchunguza.

Halijui kuchunguza hata vyanzo vya ajali barabarani, sembuse ugaidi? Jeshi la Tanzania, kila ikitokea ajali barabarani, utasikia kuwa chanzo cha ajali mara ni mwendo kasi au tairi lilipasuka. Upuuzi mtupu! Nani alikuambia kuwa kila ukienda kasi unapata ajali? Hawaendi mbali zaidi ya kuangalia matokeo badala ya kutafuta visababishi.

Kwenye uchunguzi, jeshi la polisi ni zero. Wanapotoa taarifa za uchunguzi, unagundua kabisa kuwa hawa watu hawana mafunzo yoyote kwenye investigation.
 
Kumbe tunaweza tu kuchunguza kwa muda mfupi hata siku 10 sasa yale mambo ya kesi mwaka mzima uchunguzi unaendelea yanatoka wapi?? Huyu bado kafa lakini wamejuwa yote hayo nawapa hongera lakini mengine mbona mashahidi wapo wazima lakini kila leo uchunguzi haujakamilika. Kazi nchi hii...
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
Upuuzi mtupu
 
Polisi ni waongo sana, ile video baada ya Hamza risasi kuisha alinyoosha mikono, kwa askari wenye mafunzo kama ambavyo huwa wanajitapa, wangeweza kumkamata mzima mzima... cha ajabu waliendelea kulenga hewa tena wapo wengi... yaani ni aibu..
Wangemkamata na kumhoji, lakini walikuwa na nia ya wazi kupoteza ushahidi... wakaamua kummaliza

Askari hata shabaha hawana, kaanguka chini bado kwa uoga wakaendelea ku shoot kama hawaamini vile...

Yaani Hamza ukitizama alikuwa highly trained na umakini sana, angekuwa na magazine za kutosha angewalaza sana kwa sababu ya ujinga... lile askari lingine linafikiri sifa kusogea karibu na hatari kiasi kile... yaani ni vituko vitupu...

Hivi hawa polisi wana shida gani
 
Kumbe tunaweza tu kuchunguza kwa muda mfupi hata siku 10 sasa yale mambo ya kesi mwaka mzima uchunguzi unaendelea yanatoka wapi?? Huyu bado kafa lakini wamejuwa yote hayo nawapa hongera lakini mengine mbona mashahidi wapo wazima lakini kila leo uchunguzi haujakamilika. Kazi nchi hii...
😭😭
 
Back
Top Bottom