DED/DEO Magu watoto wako hatarini Magu Shule ya Msingi

Kaji Bagome

Member
Joined
Nov 5, 2019
Posts
16
Reaction score
22
Ujumbe huu uwafikie Mkurugenzi Mtendaji (DED) Bwn. Lutengano Mwalwiba na Afisa Elimu Msingi (DEO) Bi. Glory Mtui; wote wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya MAGU.

Kuhusu mada iliyobeba ujumbe huu ni kwamba, watoto wanaosoma Magu Shule ya Msingi iliyoko Magu Mjini wako hatarini tangu ujenzi wa jengo jipya la madarasa unaoendelea shuleni hapo.

Hatari hiyo inatokana na watoto kuamriwa na uongozi wa shule hiyo kwenda kuteka maji kutoka kwenye dimbwi ambalo liko umbali wa takriban nusu kilomita kutoka shuleni hapo; maji kwa ajili ya ujenzi nilioutaja, ikiwa ni kumwagilia matofali, jengo na ujenzi kwa ujumla.
Kabla ya kufikia dimbwi hilo, watoto inawabidi wavuke barabara ya lami inayoingia na kutoka hospitali ya wilaya; ambapo kuna magari, pikipiki nyingi na baiskeli; vyombo vyote hivyo vya usafiri huendeshwa kwa kasi, na watoto hao hufanya kazi hiyo ya kuteka maji bila kudindikizwa au kuongozwa na waalimu.

Jana kuna mtoto wa DARASA LA KWANZA (STD I) aligongwa na pikipiki na alipata majeraha makubwa kichwani, alipelekwa hospitali ya wilaya kwa matibabu; akahudumiwa, lakini hali yake ilikuwa mbaya ikabidi apelekwe Bugando Hospital kwa rufaa.

Ni kweli ajali inaweza kutokea mahali popote; lakini kwa mazingira ya ajali iliyomhusisha huyu mtoto kuna uzembe na kutokujali usalama wa watoto kwa hali ya juu sana kwa uongozi wa shule ya Magu, hususan Mwalimu Mkuu.

Magu kuna mtandao wa mabomba na maji yanatoka kwa wingi kila siku, isipokuwa kwa dharula tena kwa nadra sana. Shule ya Magu imeunganishwa na mtandao wa maji ya bomba, lakini shuleni hapo maji hayatoki kwa sababu mita iliibiwa!

Hivi, huko Idara ya Maji Magu mita za maji hakuna? Hata kama mita ya maji inauzwa, Shule haipati capitation grant kila mwezi kwa ajili ya matumizi ikiwemo ukarabati? Huu ni uzembe na kutojali kulikopitiliza kunakofanywa na uongozi wa shule ya msingi Magu.

Mita ya maji inagharimu kiasi gani mpaka usalama wa watoto uhatarishwe kiasi kikubwa hivyo kwa kwenda kuteka maji kwenye dimbwi la maji yaliyotuama kwa umbali ule wakivuka barabara yenye vyombo vya usafiri viendavyo kasi bila kusindikizwa na waalimu?

Maji yaliyotuama kiafya hayafai, hata kama hawayanywi, lakini ni kuwahatarisha watoto maana maji hayo yana uwezekano mkubwa yakawa na vijidudu vinavyosababisha kichocho na magonjwa mengine.

Hatari ya watoto kudumbukia kwenye hilo dimbwi na kupoteza maisha, maana hawana usimamizi wa waalimu. Hatari ya watoto kugongwa na magari, pikipiki au baiskeli kama ilivyotokea jana kwa huyo mtoto wa darasa ka kwanza.

Licha ya ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi, bado wanafunzi wameendelea kuteka maji kutoka kwenye dimbwi hilo, bila uongozi wa shule kujali kwamba mwenendo wao mbovu wa kuendesha mambo umeleta kadhia kubwa na mpaka sasa majaaliwa ya majeruhi hayajulikani.
Kukosekana kwa maji ya bomba hapo shuleni, maana yake ni kwamba hata lile agizo la kunawa mikono kama tahadhari ya corona hapo shuleni halipo!

Vyoo vya shule ya msingi Magu vinatumia maji; je hali ya vyooni hapo shuleni ikoje? Ni vema DED na DEO Msingi Magu mkachukua hatua kali dhidi ya uongozi wa shule hiyo.

Naamini mkifuatilia kwa undani hapo patakuwa na mambo mengi ambayo yatakuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Vipo viashiria vingi sana hapo shuleni ambavyo vinaonesha kwamba uongozi shuleni hapo siyo thabiti kwa sasa.

Rudisheni mita ya maji maji yatoke shuleni, ili kuwaepusha watoto na hatari zinazoweza kuzuilika.

Povu ruksa, maana ukiwaambia watu ukweli wananuna!!
 
Kiujumla wilaya ya magu yte kuna tatizo ktk shule zte za msingi! Watoto watasombaje maji yakumwagilia??? Baadae ktk riport yao utasikia kumwagilia matofari gharama... 340,000

Bado kuna baadhi ya shule hazina madawati, hazina madarasa, nenda s/m kisesa . Watoto wanakimbia kuwahi dawati, viongozi wamekoswa ubunifu, walipozuiliwa kuchangisha wakanuna , hawana mawazo mbadara tena.
 
Dah!! Hataree; hata Kisesa? Mzee amesema anaiongezea wilaya moja Mwanza Jiji; nahisi Kisesa itahamia jiji, labda watoto watapata huduma bora zaidi za kielimu.
Ole wenu Magu DC, Kisesa ikirudi jiji mmekwisha; mtabaki na nini? Busega iliporudi Simiyu mlipata mshtuko; Kisesa ikiondoka mtazimia. Teh, teh, teh, teh......
 
Bora iludi jiji, wilaya ya magu haina jipya ! Imezidiwa na mji ramadi , kisesa hakuna maji, hakuna mipango ya kuipanga, mji unakua kwa kasi , ukitaka kuamini hilo angalia stendi na soko lilipo, utazani hakuna mbunge na madiwani, watendaji kata na veo siwezi kuwalaum!
Bora irudi jiji kwa wajanja kiswaga abaki akiwaswaga wananzengo wake,
Maana ikiwa wilaya itakuwa na jimbo lake pia.
 
Tahadhari imetolewa Magu, wahusika wamelala usingizi. Kule Geita mtoto amefukiwa kifusi
 
Maji ya bomba Magu S/Msingi yameanza kutoka leo!! Ni mpaka madhara yatokee? Mnangwe wee!! Watendaji wa aina ya Mwalimu Mkuu Magu S/Msingi hawafai.
TAHADHARI KABLA YA HATARI ni LAZIMA, no compromise!!
Si ajabu huyo mwalimu ataachwa aendelee tu na ukuu wake kama vile mtoto aliyeumizwa au kulemaa hakuwa na haki ya kulindwa.
Huyo mama alichomewa ofisi na wananchi kule Nyambitilwa alikokuwa mwalimu mkuu ndipo akahamishiwa Magu S/ Msingi.
Hivi DED na DEO Msingi hapo Halmashauri Magu hamwoni incompetence ya huyo madam? Aisee nyie!! Haya, Mungu anawaona.
 
Dah!! Hataree; hata Kisesa? Mzee amesema anaiongezea wilaya moja Mwanza Jiji; nahisi Kisesa itahamia jiji, labda watoto watapata huduma bora zaidi za kielimu.
Ole wenu Magu DC, Kisesa ikirudi jiji mmekwisha; mtabaki na nini? Busega iliporudi Simiyu mlipata mshtuko; Kisesa ikiondoka mtazimia. Teh, teh, teh, teh......
Tatizo wilaya ya magu chanzo cha mapato ni uvuvi, ndio maana wakisikia habari ya kuanzishwa wilaya mpya wanahaha.
 
Maji ya bomba Magu S/Msingi yameanza kutoka leo!! Ni mpaka madhara yatokee? Mnangwe wee!! Watendaji wa aina ya Mwalimu Mkuu Magu S/Msingi hawafai.
TAHADHARI KABLA YA HATARI ni LAZIMA, no compromise!!
Si ajabu huyo mwalimu ataachwa aendelee tu na ukuu wake kama vile mtoto aliyeumizwa au kulemaa hakuwa na haki ya kulindwa.
Huyo mama alichomewa ofisi na wananchi kule Nyambitilwa alikokuwa mwalimu mkuu ndipo akahamishiwa Magu S/ Msingi.
Hivi DED na DEO Msingi hapo Halmashauri Magu hamwoni incompetence ya huyo madam? Aisee nyie!! Haya, Mungu anawaona.
DED, DEO Msingi na watendaji wengine mnaohusika na Idara ya Elimu hapo wilayani Magu; fuatilieni kwa karibu utendaji wa huyo Mwalimu Mkuu Magu S/Msingi mkizingatia historia ya matukio ya ovyo aliyoyafanya shule alizotoka (Nyanguge na Nyambitilwa) kabla hamjamhamishia Magu S/Msingi.
Kwa nini hamwavui madaraka watu wazembe na wenye uwezo hafifu wa kiuongozi kama huyo Mwalimu?
Mbona kuna walimu wengi sana tens wenye Stashahada na Shahada ambao hamwapi madaraka, badala yake mnaendelea kukumbatia walimu wakuu wasiokuwa na sifa, tena wazembe na wakorofi kama huyo?
Mtasema mnasubiri STD VII wamalize mitihani ndio mmwondoe huyo mwalimu!! Kwani sasa hivi anafanya nini cha maana shuleni hapo zaidi ya kuwavuruga waalimu, wanafunzi na wazazi?
Hana ushirikiano na waalimu wake; mizozo isiyoisha kwa sababu ya ubabe na kutokutaka kushauriwa; lugha chafu kwa waalimu na wazazi na kuwanyanyasa wanafunzi.
Mchanga na kokoto kwa ajili ya ujenzi wa hilo jengo jipya vimesombwa na watoto kwa kuokoteza mitaani, hata kuiba kwenye saiti za watu na shule jirani ya Nyalikungu! Hilo jengo mbona limechangiwa fedha na wazazi?
Bado amewabebesha watoto maji mpaka mtoto wa STD I amegongwa na pikipiki akivuka barabara kwenda lamboni na hatujui nini majaaliwa ya mtoto huyo!
BADO mwalimu huyo anadiriki kutamka ndani ya Staff Room kwamba yeye hajali kuandikwa kwenye Facebook; anasema AFADHALI mtoto huyo angekufa kabisa ili aandikwe vizuri!
Jamani! Ninyi mnaona huyu mama ni wa kawaida?
Nijuavyo mimi, akinamama wana huruma kuliko wakinababa; yeye huyu vipi?
Unawezaje kumtakia mtoto asiye na hatia AFADHALI YA KUFA, ili uandikwe vizuri kwenye Facebook?
Hata kuta zina masikio; usitamke jambo baya dhidi ya mtu ukiamini eti hatalisikia! Ni suala la muda tu.
DED na DEO Msingi Magu, mvueni madaraka huyo mama; hafai kuwa Mwalimu Mkuu.
Watoto wa STD VII Magu S/Msingi hawataathirika kimasomo kwa kuondolewa ukuu wa shule huyo mama; mimi naamini, badala yake watoto watanufaika maana waalimu watapata morale ya kufanya kazi vizuri zaidi, maana watapata nafasi ya kupanga mipango yao vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa walivyokabwa koo!
MSIPOJALI MADOGO, NA MAKUBWA MTAACHA. Tchao.
 
HILO JENGO LIMECHANGIWA FEDHA NA WAZAZI (AU NIONGEZE SAUTI?)
WEO Magu Mjini na M/Kiti Kamati ya Shule Bwana Omedi tuelezeni kuhusu pesa za jengo zilizochangwa na wazazi zimekwenda wapi mpaka watoto wanabebeshwa kokoto, mchanga na maji? Au na ninyi mmeshiriki kuzila? Hiiiiii....!! (Kwa sauti ya MZEE) Ole wenu.
 
Umeshindwa kwenda hapo shuleni kuwapa huo ukweli???
Mkuu SACO; mwenye mamlaka ya kumwajibisha Mwalimu Mkuu huyo mkuu wa idara ya elimu (DEO) msingi au Mkurugenzi (DED) mwenyewe.
Jukumu la waathirika ni kutoa taarifa tu kwa mamlaka husika; MUHIMU ni kuwa, taarifa hizo ziwe sahihi na siyo majungu.
 
Umenena vema Hagwila; DED na DEO Msingi Magu, wafanye uchunguzi wa hayo majongolito ya mwalimu huyo ambaye yuko chini yao. Shule ipo, waalimu wapo, wanafunzi wapo na wazazi wapo; ukweli utathibitika tu.
 
Ujumbe huu uwafikie Mkurugenzi Mtendaji (DED) Bwn. Lutengano Mwalwiba na Afisa Elimu Msingi (DEO) Bi. Glory Mtui; wote wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya MAGU.

Kuhusu mada iliyobeba ujumbe huu ni kwamba, watoto wanaosoma Magu Shule ya Msingi iliyoko Magu Mjini wako hatarini tangu ujenzi wa jengo jipya la madarasa unaoendelea shuleni hapo.

Hatari hiyo inatokana na watoto kuamriwa na uongozi wa shule hiyo kwenda kuteka maji kutoka kwenye dimbwi ambalo liko umbali wa takriban nusu kilomita kutoka shuleni hapo; maji kwa ajili ya ujenzi nilioutaja, ikiwa ni kumwagilia matofali, jengo na ujenzi kwa ujumla.
Kabla ya kufikia dimbwi hilo, watoto inawabidi wavuke barabara ya lami inayoingia na kutoka hospitali ya wilaya; ambapo kuna magari, pikipiki nyingi na baiskeli; vyombo vyote hivyo vya usafiri huendeshwa kwa kasi, na watoto hao hufanya kazi hiyo ya kuteka maji bila kudindikizwa au kuongozwa na waalimu.

Jana kuna mtoto wa DARASA LA KWANZA (STD I) aligongwa na pikipiki na alipata majeraha makubwa kichwani, alipelekwa hospitali ya wilaya kwa matibabu; akahudumiwa, lakini hali yake ilikuwa mbaya ikabidi apelekwe Bugando Hospital kwa rufaa.

Ni kweli ajali inaweza kutokea mahali popote; lakini kwa mazingira ya ajali iliyomhusisha huyu mtoto kuna uzembe na kutokujali usalama wa watoto kwa hali ya juu sana kwa uongozi wa shule ya Magu, hususan Mwalimu Mkuu.

Magu kuna mtandao wa mabomba na maji yanatoka kwa wingi kila siku, isipokuwa kwa dharula tena kwa nadra sana. Shule ya Magu imeunganishwa na mtandao wa maji ya bomba, lakini shuleni hapo maji hayatoki kwa sababu mita iliibiwa!

Hivi, huko Idara ya Maji Magu mita za maji hakuna? Hata kama mita ya maji inauzwa, Shule haipati capitation grant kila mwezi kwa ajili ya matumizi ikiwemo ukarabati? Huu ni uzembe na kutojali kulikopitiliza kunakofanywa na uongozi wa shule ya msingi Magu.

Mita ya maji inagharimu kiasi gani mpaka usalama wa watoto uhatarishwe kiasi kikubwa hivyo kwa kwenda kuteka maji kwenye dimbwi la maji yaliyotuama kwa umbali ule wakivuka barabara yenye vyombo vya usafiri viendavyo kasi bila kusindikizwa na waalimu?

Maji yaliyotuama kiafya hayafai, hata kama hawayanywi, lakini ni kuwahatarisha watoto maana maji hayo yana uwezekano mkubwa yakawa na vijidudu vinavyosababisha kichocho na magonjwa mengine.

Hatari ya watoto kudumbukia kwenye hilo dimbwi na kupoteza maisha, maana hawana usimamizi wa waalimu. Hatari ya watoto kugongwa na magari, pikipiki au baiskeli kama ilivyotokea jana kwa huyo mtoto wa darasa ka kwanza.

Licha ya ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi, bado wanafunzi wameendelea kuteka maji kutoka kwenye dimbwi hilo, bila uongozi wa shule kujali kwamba mwenendo wao mbovu wa kuendesha mambo umeleta kadhia kubwa na mpaka sasa majaaliwa ya majeruhi hayajulikani.
Kukosekana kwa maji ya bomba hapo shuleni, maana yake ni kwamba hata lile agizo la kunawa mikono kama tahadhari ya corona hapo shuleni halipo!

Vyoo vya shule ya msingi Magu vinatumia maji; je hali ya vyooni hapo shuleni ikoje? Ni vema DED na DEO Msingi Magu mkachukua hatua kali dhidi ya uongozi wa shule hiyo.

Naamini mkifuatilia kwa undani hapo patakuwa na mambo mengi ambayo yatakuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Vipo viashiria vingi sana hapo shuleni ambavyo vinaonesha kwamba uongozi shuleni hapo siyo thabiti kwa sasa.

Rudisheni mita ya maji maji yatoke shuleni, ili kuwaepusha watoto na hatari zinazoweza kuzuilika.

Povu ruksa, maana ukiwaambia watu ukweli wananuna!!
Tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom