Kaji Bagome
Member
- Nov 5, 2019
- 16
- 22
Ujumbe huu uwafikie Mkurugenzi Mtendaji (DED) Bwn. Lutengano Mwalwiba na Afisa Elimu Msingi (DEO) Bi. Glory Mtui; wote wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya MAGU.
Kuhusu mada iliyobeba ujumbe huu ni kwamba, watoto wanaosoma Magu Shule ya Msingi iliyoko Magu Mjini wako hatarini tangu ujenzi wa jengo jipya la madarasa unaoendelea shuleni hapo.
Hatari hiyo inatokana na watoto kuamriwa na uongozi wa shule hiyo kwenda kuteka maji kutoka kwenye dimbwi ambalo liko umbali wa takriban nusu kilomita kutoka shuleni hapo; maji kwa ajili ya ujenzi nilioutaja, ikiwa ni kumwagilia matofali, jengo na ujenzi kwa ujumla.
Kabla ya kufikia dimbwi hilo, watoto inawabidi wavuke barabara ya lami inayoingia na kutoka hospitali ya wilaya; ambapo kuna magari, pikipiki nyingi na baiskeli; vyombo vyote hivyo vya usafiri huendeshwa kwa kasi, na watoto hao hufanya kazi hiyo ya kuteka maji bila kudindikizwa au kuongozwa na waalimu.
Jana kuna mtoto wa DARASA LA KWANZA (STD I) aligongwa na pikipiki na alipata majeraha makubwa kichwani, alipelekwa hospitali ya wilaya kwa matibabu; akahudumiwa, lakini hali yake ilikuwa mbaya ikabidi apelekwe Bugando Hospital kwa rufaa.
Ni kweli ajali inaweza kutokea mahali popote; lakini kwa mazingira ya ajali iliyomhusisha huyu mtoto kuna uzembe na kutokujali usalama wa watoto kwa hali ya juu sana kwa uongozi wa shule ya Magu, hususan Mwalimu Mkuu.
Magu kuna mtandao wa mabomba na maji yanatoka kwa wingi kila siku, isipokuwa kwa dharula tena kwa nadra sana. Shule ya Magu imeunganishwa na mtandao wa maji ya bomba, lakini shuleni hapo maji hayatoki kwa sababu mita iliibiwa!
Hivi, huko Idara ya Maji Magu mita za maji hakuna? Hata kama mita ya maji inauzwa, Shule haipati capitation grant kila mwezi kwa ajili ya matumizi ikiwemo ukarabati? Huu ni uzembe na kutojali kulikopitiliza kunakofanywa na uongozi wa shule ya msingi Magu.
Mita ya maji inagharimu kiasi gani mpaka usalama wa watoto uhatarishwe kiasi kikubwa hivyo kwa kwenda kuteka maji kwenye dimbwi la maji yaliyotuama kwa umbali ule wakivuka barabara yenye vyombo vya usafiri viendavyo kasi bila kusindikizwa na waalimu?
Maji yaliyotuama kiafya hayafai, hata kama hawayanywi, lakini ni kuwahatarisha watoto maana maji hayo yana uwezekano mkubwa yakawa na vijidudu vinavyosababisha kichocho na magonjwa mengine.
Hatari ya watoto kudumbukia kwenye hilo dimbwi na kupoteza maisha, maana hawana usimamizi wa waalimu. Hatari ya watoto kugongwa na magari, pikipiki au baiskeli kama ilivyotokea jana kwa huyo mtoto wa darasa ka kwanza.
Licha ya ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi, bado wanafunzi wameendelea kuteka maji kutoka kwenye dimbwi hilo, bila uongozi wa shule kujali kwamba mwenendo wao mbovu wa kuendesha mambo umeleta kadhia kubwa na mpaka sasa majaaliwa ya majeruhi hayajulikani.
Kukosekana kwa maji ya bomba hapo shuleni, maana yake ni kwamba hata lile agizo la kunawa mikono kama tahadhari ya corona hapo shuleni halipo!
Vyoo vya shule ya msingi Magu vinatumia maji; je hali ya vyooni hapo shuleni ikoje? Ni vema DED na DEO Msingi Magu mkachukua hatua kali dhidi ya uongozi wa shule hiyo.
Naamini mkifuatilia kwa undani hapo patakuwa na mambo mengi ambayo yatakuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Vipo viashiria vingi sana hapo shuleni ambavyo vinaonesha kwamba uongozi shuleni hapo siyo thabiti kwa sasa.
Rudisheni mita ya maji maji yatoke shuleni, ili kuwaepusha watoto na hatari zinazoweza kuzuilika.
Povu ruksa, maana ukiwaambia watu ukweli wananuna!!