Defense budget ya Marekani ni kubwa sana

Defense budget ya Marekani ni kubwa sana

Biashara na uzalishaji wa silaha kwa US ni complex sana, kiasi cha kuongeza bei ya silaha kunakopelekea bajeti kubwa.
 
Japan, Singapore, Korea Kusini, Switzerland, Taiwan na Israel ni tajiri kuliko DRC/Congo,
Korea Kusini na Japan pia ni tajiri kuliko Urusi.
Ungesema pia nini sababu ya utajiri wao.

Je ni mapesa mengi waliyochapisha au kuna rasilimali zingine?

Jibu kisomi pls.
 
Ni kampuni gani kubwa ya silaha ya Urusi inamilikiwa na jeshi. Haipo.

Kampuni gani kubwa ya silaha ya China inamilikiwa na jeshi. Haipo.

Na nani kakwambia Urusi au China hawanunui silaha na huduma za kijeshi? Tenders za silaha, ugavi, ukarabati, design na mengine wanatoa kwa enterprises. Hawachukui bure sio maji yale kwamba unachota tu. Wangekuwa wanachukua bure, wangepata bure kwa nani.
Ni kama umeamua kukomaza kichwa hiv mkuu..Yan ni kama hujaelewa au umegoma kuelewa ila point iko clear kabisa
 
Ungesema pia nini sababu ya utajiri wao.

Je ni mapesa mengi waliyochapisha au kuna rasilimali zingine?

Jibu kisomi pls.
Ni rasilimali yao ya AKILI, ukiwa na akili za kuuendesha ulimwengu hata kama hauna madini, misitu, ardhi kubwa, mafuta n.k bado utaishi vizuri tu.
 
Ni kama umeamua kukomaza kichwa hiv mkuu..Yan ni kama hujaelewa au umegoma kuelewa ila point iko clear kabisa
Basi jibu maswali yangu mawili.

Kampuni gani kubwa ya silaha inamilikiwa na jeshi, iwe Russia au China?

Je, Urusi au China zinachukua silaha bure tu kwenye enterprises zao?
 
Kwa nini na Russia wasichapishe Rubu tu??
Marekani iliifanya pesa yake itumike kimataifa hasa kwenye biashara ya mafuta petrodollar ndio maana inaprint hovyo hela zake.
Siku dunia itakapoacha kunitumia kwenye biashara ya kimataifa hasa mafuta ndio itakuwa anguko la dollar
 
Kuwa na bajeti kubwa sio lazima uwe na uwezo mkubwa mfano nchi za kiarabu.
Marekani makampuni makubwa ya kuzalisha silaha yanamilikiwa na watu binafsi tofauti na nchi Kama Urusi mashirika ya silaha yanamilikiwa na serikali.
 
Resources za Africa ndio chimbuko la utajiri wao.

Kiufupi uchumi tayari wanao ila wanatumia pesa kuulinda na pia kujitanua.

Ukiachana na silaha kama bunduki, pesa ni silaha ambayo huwa ina matokeo mazuri tu.

Namna viongozi wetu wa kiafrika wanavyohongwa na kuuza rasilimali utaona faida yake.
 
Kombora moja ndani ya jeshi la Marekani linagharimu bilioni moja wakati la kiwango kile kile kwa wenzao ni milioni mia moja au chini. Lazima wawe na bajeti ya kutisha.
 
Basi jibu maswali yangu mawili.

Kampuni gani kubwa ya silaha inamilikiwa na jeshi, iwe Russia au China?

Je, Urusi au China zinachukua silaha bure tu kwenye enterprises zao?
China silaha zinatengenezwa na state owned companies kwa asilimia kubwa
Mfano Chengdu Aerospace inamilikiwa na AVIC wanatengeneza ndege J series
Anyway mim kuandika sana siwezi jifunze zaidi mtandaoni ila baadhi ya hints hizi hapa
Hizi corporation zinamiliki dozens of subsidiaries za kuzalisha meli,ndege,mabomu na research mbalimbali.
Screenshot_20240616-185833.png
 
Attachments

  • Screenshot_20240616-185845.png
    Screenshot_20240616-185845.png
    152.2 KB · Views: 1
Basi jibu maswali yangu mawili.

Kampuni gani kubwa ya silaha inamilikiwa na jeshi, iwe Russia au China?

Je, Urusi au China zinachukua silaha bure tu kwenye enterprises zao?
Ukiachana na hayo yote pia ni swala lipo wazi,labda kaba lengo lako sio constructive criticism bali kujitoa ufahamu tu kua gharama za uzaliahaji bidhaa china na Russia zipo chini sanaa ukilinganisha na Europe na USA hivyo kulinganisha numbers za bajeti haireflect situation ya majeshi yao.USA akitumia gharama kama za china basi atakua na jeshi dhaifu.
 
China silaha zinatengenezwa na state owned companies kwa asilimia kubwa
Mfano Chengdu Aerospace inamilikiwa na AVIC wanatengeneza ndege J series
Anyway mim kuandika sana siwezi jifunze zaidi mtandaoni ila baadhi ya hints hizi hapa
Hizi corporation zinamiliki dozens of subsidiaries za kuzalisha meli,ndege,mabomu na research mbalimbali.
View attachment 3018868
Hizi zote state owned enterprises nazijua kina Chengdu, Shenyang, DongFeng na nyingine. Hata Urusi zipo zikiongozwa na ROSTEC.

Nimeuliza wanitajie kampuni za kutengeneza silaha zinazomilikiwa na jeshi hapo China au Urusi. Unanitajia kampuni zinazomilikiwa na serikali. Kwamba tofauti ya jeshi na serikali hujui?
 
Ukiachana na hayo yote pia ni swala lipo wazi,labda kaba lengo lako sio constructive criticism bali kujitoa ufahamu tu kua gharama za uzaliahaji bidhaa china na Russia zipo chini sanaa ukilinganisha na Europe na USA hivyo kulinganisha numbers za bajeti haireflect situation ya majeshi yao.USA akitumia gharama kama za china basi atakua na jeshi dhaifu.
Sawa sawa ni maoni yako. Hata mimi naweza sema Marekani wanaunda silaha kwa faida hivyo kampuni zao zina uwezo wa kufanya research and development zenyewe bila kutegemea state. Na zina uwezo wa kufanya mass production sababu zinapata faida.

Kwenye WW2 makampuni ya Marekani ilizalisha silaha hizi hapa ikawapa USSR waliokuwa wana state owned enterprises, mbona USSR walifeli kuzalisha silaha kwa wingi kama kigezo ni silaha kuzalishwa na serikali?
20240610_220731.jpg
 
Kwa sababu wenzio hawapendi kuishi maisha ya kuiga-iga, hasa maigizo ambayo mwishowe ni kujiangamiza mwenyewe.

By printing and printing and printing again the currency, US has been shooting her own foot all along.
Tangu mmejifunza kuwa kuna neno Print basi mmeamua kuzigotesha akili. Hamuoni chochote zaidi ya ku print.
Hao mnaosema wana print hela hivi mmewahi kufika kwao mkaona jinsi kuanzia raia wanavyozitafuta hizo hela?
Au mnajua vigezo vya ku print hela?
 
Kuwa na bajeti kubwa sio lazima uwe na uwezo mkubwa mfano nchi za kiarabu.
Marekani makampuni makubwa ya kuzalisha silaha yanamilikiwa na watu binafsi tofauti na nchi Kama Urusi mashirika ya silaha yanamilikiwa na serikali.
Kama ambavyo Marekani makampuni ya teknolojia yanamilikiwa na watu binafsi na bidhaa zao tunaziona sokoni, na hadi hapa umetype kwa kuzitumia.
Urusi bidhaa zake za bei ndogo ziko wapi sokoni.

Iko wapi internet ya Urusi, operating system yao (US ana Android na iOS). Wakati US ana HP na Dell mnazosema ni za watu binafsi na za bei kali, za Urusi za serikali na za bei nafuu ziko wapi. US aweke Pixel, Sony, Motorola, iPhone na wengine mezani Urusi yeye ataweka kina nani wa ubora kuzidi Marekani ila ana quality zaidi na cheap.

Ushindwe kubobea kwenye civilian technology uje uweze military tech? Camera, simu, ndege za raia hujui eti uje uwe bora kwenye fighter jets na electronics za kivita.
 
Tangu mmejifunza kuwa kuna neno Print basi mmeamua kuzigotesha akili. Hamuoni chochote zaidi ya ku print.
Hao mnaosema wana print hela hivi mmewahi kufika kwao mkaona jinsi kuanzia raia wanavyozitafuta hizo hela?
Au mnajua vigezo vya ku print hela?
Waitake Urusi nayo iprint Ruble waone kama hatujazifungia maandazi na kuzibeba kwenye matoroli tukienda bureau de change
 
Resources za Africa ndio chimbuko la utajiri wao.

Kiufupi uchumi tayari wanao ila wanatumia pesa kuulinda na pia kujitanua.

Ukiachana na silaha kama bunduki, pesa ni silaha ambayo huwa ina matokeo mazuri tu.

Namna viongozi wetu wa kiafrika wanavyohongwa na kuuza rasilimali utaona faida yake.
Africa tuache kujipa umuhimu as if mataifa mengine hayana rasilimali kabisa.
 
Back
Top Bottom