South Korea wanaunda meli kubwa kabisa za kisasa. Wana vifaa vya ujenzi. Home appliances nyingi. Vifaa vya mawasiliano. Vifaa vya matibabu hospitalini.
Urusi hasahasa ana maliasili ambazo hajaunda bali kazikuta. Ni kama Congo, Saudi Arabia au Qatar.
Satellite hata North Korea na Iran wamejaribu, na hawana cameras kwenye soko la dunia. Hata India.
Kumiliki market share kwenye soko la digital cameras kama Canon, Sony, Nikon, Fujifilm ni vigumu kuliko kurusha satellite angani.
Alafu Marekani akiongoza kiuchumi mnasema anaprint dola😂
Bidhaa zinaonekana kwenye market share ya industry kwenye soko la dunia. Hizo bidhaa za Urusi ziko wapi mbona kama gesi na mafuta mnataja, kwamba mfano Lada inashindana na soko la Toyota, Ford, RR ama Hyundai?
Umeona sasa? Marekani yeye anatumia maguvu ili kulazimisha bidhaa zake zinunulike duniani.
Yeyote anayeonekana mpinzani, anapambana naye ili kumwondoa. Ndiyo maana hawapatani kabisa na China, kwa mfano.
Hakuna soko huria kama wanavyotuaminisha. Kuna kuhodhi soko kwa nguvu.
Kila nchi inayojaribu kuinuka kiuchumi hugeuka kuwa adui wa Marekani, isipokuwa ikiridhia kufuata vigezo na masharti yanayofuata mrengo wa Amerika.
Angalia nchi zote zenye utajiri wa mafuta, gesi na madini na rasilimali zingine, namna zilivyovurugwa na Marekani. Hiyo ni data halisi, ambayo ni sera ya Marekani hadi kesho kutwa.
Si ajabu vita vya Ukreni ni jitihada za Marekani kumdhoofisha Russia kiuchumi ili asinufaike na soko kubwa la Ulaya.
Nchi inayoanzisha vita ili kunufaika na mauzo ya hazina ya silaha zake, au hata kusambaza kimakusudi magonjwa ya mlipuko, taifa kama hilo limefilisika kisiasa, kiuchumi na kimaadili, na ni adui namba moja wa dunia.
Ndiyo maana mbadala pekee unaokubalika kwa sasa katika kudumisha amani duniani ni sera za umoja wa BRICS.
Ni wazi katika karne hii ya 21, Marekani angali akiishi kwa kutegemea mbinu ya zama za giza, ambapo utawala fulani wenye nguvu uliangamiza mashamba au maghala ya hifadhi ya vyakula vya tawala zingine ili zijisalimishe na kutawaliwa.
Unajua kwa nini nchi kama Venezuela inaishi katika umaskini wa kutupwa, licha ya utajiri mkubwa sana wa mafuta? Sababu pekee ni Marekani.