Demokrasia haileti maendeleo ila udikteta ndio unaleta maendeleo?

Demokrasia haileti maendeleo ila udikteta ndio unaleta maendeleo?

Hakuna nchi imewahi kutoka kwenye umaskini na kuendelea huku ikiwa ya kidemokrasia.
Maendeleo yanaendana na matumizi ya akili ipasavyo na sio ubabe ambao ni udikteta
Magufuli alitumia ubabe kufuta mikataba kwa nguvu matokeo yake nchi imelipa mafidia mengi na bado kesi nyingine za kuvunja mikataba kiharamia zipo mahakamani

Afrika hatutaki kutumia akili alafu tunadhani kupitia udikteta tutapa maajabu ya maendeleo tunasafari ndefu sana
 
Pia lazima tufahamu kati ya democracy na dictatorship kipi kianze. Nchi za magharibi zilianza na udikteta baada ya kupiga hatua katika nyanja za maendeleo na ustaharabu Wakashift kwenda Kwenye democracy.
Africa ni vice versa tumeanza na democracy [emoji1787][emoji1787]
Hakuna democracy kwenye jamii masikini na isiyostaharabika.
Misingi ya German ya Leo ilijengwa na Adolph Hitler.

Umeeleza vizuri sana maccm Kindakindaki na Chadema wa mchongo hawawezi kukuelea
 
Hujui maana halisi ya demokrasia wala udikteta umekariri ujinga
 
Hizo ni hadithi. Ebu weka hapa thamani ya rasilimali zilizochotwa na Japan nchini China Vs zilizoachwa ambazo zipo mpaka leo?

Na kweli elimu yako ni ndogo sana.

Japan iliwahi kutawala eneo tu dogo la China, na siyo China yote.

US imewahi kutawaliwa na mataifa ya kigeni, lakini leo ni superpower.

Who colonized America?

Britain, France, Spain, and the Netherlands established colonies in North America. Each country had different motivations for colonization and expectations about the potential benefits.

Halafu ufahamu kuanzia leo kuwa natural resources haziifanyi nchi kuwa na maendeleo, japo inaweza kuwa ni ingridient. Utajiri mkubwa upo kichwani.


Wataalam wa Sayansi ya Saikolojia wanasema kuwa udikteta hufubaza akili na kuzuia ubunifu na ugunduzi. Ndiyo maana unaona mataifa kama China, hayagundui chochote. Wanaishia kuiga walivyogundua wenzao. Mifumo ya kidikteta ua Afrika, kuanzia ngazi za familia imefubaza akili ya Mwafrika. Hawezi kugundua wala hata kuiga.
Hongera kumbe china hawagundui chochote ,tuishie hapo
 
Mada ya udikteta na maendeleo inajuridia mara Kwa mara, labda hii inatokana na mageuzi makubwa ya baadhi ya authoritarians leaders kufanya mageuzi na mabadiliko makubwa, mfano

1. Stallin kuigeuza soviet kuwa industrialised ndani ya muda mfupi
2. Lee Kuan Yew WA Singapore
3. Park Chung Hee WA Korea kusini
4. Chiang Kai shek WA Taiwan
5. Augusto Pinochet WA Chile
6. Jeshi la Japan miaka 1930s
7. Maathir Mohammed WA Malaysia

Lakini licha hivyo udikteta WA hao jamaa hauwezi ukakupa ufafanuzi ama jibu la maendeleo waliyoyapata katika muda mfupi.

Kwa mfano Chiang Kai Shek WA Taiwan alikuwa Rais WA china na ndiye alieunganisha china yote kutoka Kwa wababe WA kivita, lakini huyu jamaa alikuwa ni janga na mwenye upeo mdogo kiasi cha kukosa uungwaji mkono Kwa wananchi wengi hasa vijijini watu wengi walikuwa maskini na hawakuwa na ardhi, na rushwa ilitamaraki, hii ni moja ya sababu ya kushindwa na Mao Zedong

Korea kusini kulikuwa kuna dikteta mwingine raisi WA Kwanza, sygman Rhee huyu jamaa alisbabisha umaskini kuongezeka na ufisadi kwenye serikali yake kuwa mkubwa, watu walikuwa wanapropose Sera za kiuchumi zinazoamasisha mageuzi ya kiuchumi waliitwa wakomunist na kuafhibiwa.

Maandamano yakawa mengi kutokana na ugumu WA Maisha akajiuzuru na kukimbilia us.

Sababu kubwa ni kwamba Udikteta ama democracy sio economic model ama development strategy, ndio maana mwisho WA siku Uzi utaishia kwenye mabishano maana vinavyojadiliwa ni vitu tofauti.

Ninawashauri msome kitabu cha Joe Studwell kinachoitwa How Asia Works kinachoelezea Kwa nini baadhi ya nchi za zimeendelea Sana huku zingine zikibakia kuwa maskini kupata picha juu ya Sera za uchumi na utekelezaji wake
 

Attachments

Naomba mnisaidie wadau ni nchi gani duniani imepiga hatua za maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya demokrasia?
Maendeleo ni nini? Maendeleo ya kiuchumi ni nini? Maendeleo endelevu ni nini?

Unawezaje kuwa na maendeleo endelevu bila kuwahusisha hao watu unaowaongoza kidemokrasia na kupata mrejesho kutoka kwao kuhusu muelekeo wenu? Utajuaje unachotaka kuwapa wewe kiongozi kama maendeleo ndicho wanachohitaji hao wananchi, kama hujapata feedback yao?

Kwa mfano, kama watu hawataki maendeleo ya kiuchumi yatakayoharibu sana mazingira, kwa sababu washaona maendeleo ya kiuchumi hayo yataleta uharibifu mkubwa wa mazingira utakaopelekea extinction level event kwa jamii nzima, hapo watu kuweza kujipangia mambo yao na kukataa maendeleo hayo ya kiuchumi ni sawa au si sawa?

Hatuoni kuwa hiki ndicho kizungumkuti kilichoikumba dunia hivi sasa, kwa viongozi wake kuweka kipaumbele kwenye maendeleo makubwa ya kiuchumi ambayo yanapelekea kuharibu mazingira vibaya sana kiasi cha kuhatarisha ustawi mzuri wa dunia nzima?
 
Duniani hakuna Demokrasia ya watu zaidi ya mmoja. Demokrasia ya kweli ni ya mtu mmoja mmoja tu.

Kwa mfano,wewe mwenyewe pekee unaweza kuamua ule chakula au usile, hakuna mtu wa kukuuliza.
 
Maendeleo yanaletwa na siasa safi, wananchi kufanya kazi za maendeleo,elimu,na kupambana na rushwa
 
Take a good example of the late Lee Kuan Yew of Singapore…..leo Singapore wako wapi?
 
Denmark Canada Sweden Finland Norway alimfanyia nani utumwa akawa na maendeleo.
Achana na chuki za panafricanist wameandika chuki nyingi kuliko ukweli halisi
Ww uliishi enzi za ukoloni na pan Africanist hadi useme wameandika chuki nyingi kuliko ukweli Hv enzi zile Elimu ilikuwa kwa kila mtu.
 
Ww uliishi enzi za ukoloni na pan Africanist hadi useme wameandika chuki nyingi kuliko ukweli Hv enzi zile Elimu ilikuwa kwa kila mtu.
Population ilikuwa ndogo elimu iliendana na idadi ya waliyohiitaji.maisha yalikuwa simple ajira tele,kilimo soko uhakika,biashara zinalipa uende shule kufanya nini.
Walioishi enzi hizo wanasema maisha ya mkoloni yalikuwa mazuri kabla ya uhuru.
Uhuru ni kwa maslai ya wachache na sio wote kama enzi za ukoloni.
Hata ukifanya study maisha ya muafrika yalikuwa Bora zaidi kabla ya uhuru.
 
Population ilikuwa ndogo elimu iliendana na idadi ya waliyohiitaji.maisha yalikuwa simple ajira tele,kilimo soko uhakika,biashara zinalipa uende shule kufanya nini.
Walioishi enzi hizo wanasema maisha ya mkoloni yalikuwa mazuri kabla ya uhuru.
Uhuru ni kwa maslai ya wachache na sio wote kama enzi za ukoloni.
Hata ukifanya study maisha ya muafrika yalikuwa Bora zaidi kabla ya uhuru.
Ubora huo uweke hapa tuuone ss sote na kea vigezo maalum yawezekana tulikuwa na maendeleo makubwa sana wakati huo.
 
Ubora huo uweke hapa tuuone ss sote na kea vigezo maalum yawezekana tulikuwa na maendeleo makubwa sana wakati huo.
Sasa elimu ya kikoloni ni sawa na elimu yetu hii.
Tuendelea na mfumo wa elimu wa kikoloni tungekuwa mbali sana,kosa la mwalimu ni kuingiza siasa kwenye elimu,wao walifundisha elimu vitendo na sio elimu maneno kama sasa.
Shule zilijengwa kwa standard shule iweje kuanzia mazingira nk na sio hizi zilizozungukwa na makazi hata heka Moja haifiki eti shule.
Shule iwe shule inatakiwa isipungue eneo heka nne.
Iwe na kila kitu
 
Demokrasia ni nini?
Je demokrasia ndio mfumo sahihi kuliko mifumo mingine?
Nini faida na hasara za demokrasia?
Demokrasia ilianzia wapi? (ugiriki)
Je maendeleo ni nini?
Je kuna uhusiano chanya ama hasi wa demokrasia na maendeleo? (toa mifano 5 kwa hasi na 5 kwa chanya)
Taja nchi 5 zifatazo demokrasia na zina maendeleo
Taja nchi 5 zisizofata demokrasia na zina maendeleo
Taja nchi 5 zifatazo demokrasia na hazina maendeleo
Taja nchi 5 zisizofata demokrasia na hazina maendeleo
Taja mifumo mingine tofauti na demokrasia

PIA PITIA:
A. Demokrasia haileti maendeleo ila udikteta ndio unaleta maendeleo?
B. Maendeleo hayaletwi na Demokrasia au Udikteta
C. Uongo wa Demokrasia Barani Afrika: Je, ni Uzembe au Maendeleo?


View: https://x.com/FunnyWorld1313/status/1786718147644649851
 
Naogopa kuangalia….wanauana kwani hiyo video?
 
Back
Top Bottom