Taiwan ilikuwa chini ya udikteta wa KMT chini ya Chiang Kai-Shek na mwanae kwa miongo mingi tu. Korea kusini iliweza pita mikono ya military dictatorship, Japan imefanya udikteta wa kifalme ndani na nje ya mipaka yake wakati wa mchakato wake wa maendeleo kuhusu Hongkong ilikuwa mikononi ya ukoloni wa Uingereza
Argument yako ni baseless. Kama udikteta unaleta maendeleo, basi nchi zilizodumu kwenye udikteta miaka yote ndiyo zingekuwa na maendeleo makubwa kuyazidi mataifa yote.
Unapotaja nchi ambazo labda awali zilikuwa kwenye dictatorship rule, baadaye zikabadilika na kufuata demokrasia, na sasa zimeendelea, utakuwa unaunga mkono kuwa demokrasia ina mchango mkubwa katika maendeleo. Labda kama ungesema kuwa nchi hizo ambazo zamani zilipokuwa zikiongozwa kidikteta zilikuwa na maendeleo, lakini baada ya kukumbatia demokrasia, maendeleo yake yamekuwa duni au yanaporomoka.
Tupatie mfano wa nchi iliyodumu katika udikteta ambayo inaendelea kwa kasi.
Tupatie mfano wa nchi iliyokuwa ya kiditeta iliyokuwa na maendeleo makubwa wakati wa udikteta, lakini baada ya kufuata demokrasia, maendeleo yake yamekuwa duni.
Tupatie mfano wa nchi iliyokuwa ya kidemokrasia ambayo ilikuwa na maendeleo duni, lakini baada ya kukumbatia udikteta imepata maendeleo makubwa.
Kudai kuwa nchi ambayo ni ya kidemokrasia na ina maendeleo makubwa sasa, eti ni kwa sababu misingi yake ilijengwa na udikteta ni nadharia duni kabisa. Ni sawa mtu awe maskini wakati alipokuwa mvivu wa kufanya kazi, baadaye akaachana na uvivu, akawa anafanya kazi kwa bidii, akapata maendeleo, halafu mtu atokee aseme kuwa eti maendeleo aliyoyapata huyo mtu kwa kufanya kazi kwa bidii yamekuja kwa sababu ya misingi iliyojengwa na uvivu aliokuwa nao zamani.