Demokrasia haileti maendeleo ila udikteta ndio unaleta maendeleo?

Demokrasia haileti maendeleo ila udikteta ndio unaleta maendeleo?

Naomba mnisaidie wadau ni nchi gani duniani imepiga hatua za maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya demokrasia ?
Nyingi sana ila SIO za AFRIKA .NCHI za AFRIKA VIONGOZI wake Demokrasia Wanalazimishwa tu sababu ya MIKOPO na MISAADA wao wanataka sana tena sana UDIKTETA ili wakae MADARAKANI wao na Watoto wao.VIONGOZI wa AFRIKA wakiingia Madarakani wanawaza Kubadili KATIBA ya Kuwafanya MIUNGU WATU Kuunda TUME za UCHAGUZI za KUWATANGAZA wao hata kama Wameshindwa tumejionea ya BONGO mwaka 2020 Mabango yakibandikwa ya MGOMBEA MMOJA utadhani UCHAGUZI wa chama kimoja kumbe kuna UTITIRI wa Vyama.Tumeshuhudia Danadana zikipigwa juu ya Mchakato wa KATIBA MPYA Katiba ya Wananchi na TUME HURU ya UCHAGUZI hiyo ndio Demokrasia ya NCHI za Afrika

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Unatafuta visingizio vyote ila ukweli uko pale pale. Kwanini Poland iliyotawaliwa na Warusi mpaka 1990 iwe na maendeleo kuliko sisi tuliopata uhuru 1961?

Kwanini Nchi zile za Yugoslovakia ya zamani ziendelee kuwa nyuma kuliko hata Romania?
Poland haijawahi kutawaliwa na Russia
 
Ulaya yote nchi za EU zimeendelea. Zipo karibu 30. Kule USA zote zilizoendelea ni za kidemokrasia.

Angalia Russia na utajiri wote ule waliko. Wanazidiwa maendeleo na nchi ndogo walizozitawala kama Poland.

Nenda kule Asia ya Japan, Taiwan, Hongkong , Malaysia nk.
Rudi nyuma huko waliishije, 500 yrs back.kuna miaka USA mademu walibanwa urefu wasketi uvaaji wake
 
Demokrasia ndio mpango mzima hata ukimpa mtu kila kitu akijua kwamba umemyima uamuzi basi atafanya fujo LAKINI swali kubwa linakuja Dunia hii kuna Demokrasia wapi au ni mwendo wa kudanganyana na ILLUSION..., na kupiga blah blah blah sisizoisha kujaribu kugawana klichopo kuliko kuhangaika kuongeza zaidi... kwahio kutokana na kwamba mengi ni maigizo ndio maana nilishasema....

hizo nchi ulizo taja pia there's no democracy when it come usalama wa mataifa yao... kila nchi ina angles ambayo ikiguswa na yeyote ata kama ameifanyia vipi vyema serikali wanamu eliminate as a threat...

democracy ni wimbo mgumu kutekelezeka amini nakwambia...!​
Kila jambo lina mipaka yake..
Kila mahali penye haki pia
kuna wajibu.
Demokrasia haimaanishi kuwa na uhuru wa kuvunja haki za watu wengine.
Huwezi kuiba mali za watu wengine eti ukidai kwamba hiyo ni demokrasia.
 
Naomba mnisaidie wadau ni nchi gani duniani imepiga hatua za maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya demokrasia ?
Hawakuwepo hawa vijana wa lissu wakati tunaipigania Ujerumani mashariki katika ww2. Udikteta ni maendeleo.
 
Pia lazima tufahamu kati ya democracy na dictatorship kipi kianze. Nchi za magharibi zilianza na udikteta baada ya kupiga hatua katika nyanja za maendeleo na ustaharabu Wakashift kwenda Kwenye democracy.
Africa ni vice versa tumeanza na democracy 🤣🤣
Hakuna democracy kwenye jamii masikini na isiyostaharabika.
Misingi ya German ya Leo ilijengwa na Adolph Hitler.
Misingi ya ujeruman imejengwa na hitler huu ni uongo mtakatifu
 
Hawakuwepo hawa vijana wa lissu wakati tunaipigania Ujerumani mashariki katika ww2. Udikteta ni maendeleo.
Miaka ya 1770 kuendelea nchi za america zilipata uhuru
Marekani na canada zilichagua democracia na angalia zilipo leo
Nchi za america ya kusini zilikumbatia udikteta leo hii ni maskini baada ya miaka 200 ya uhuru
 
Jidanganye usione USA kapendeza ivo ukadhani ni demokrasia.....kapigana sana vita vya wenyewe kwa wenyewe kuweka mambo sawa.
Canada nae anatembelea kivuli cha muuza marashi...
 
Jidanganye usione USA kapendeza ivo ukadhani ni demokrasia.....kapigana sana vita vya wenyewe kwa wenyewe kuweka mambo sawa.
Canada nae anatembelea kivuli cha muuza marashi...
Ukitoa america civil war alivyopigana kwa mda wa miaka 5 tu kati ya 200+ ya uhuru ni vita vipi vya wenyewe kwa wenyewe alivyopigana marekani

Waafrika acheni kupenda shortcut nchi inaendelea kwa kua na taasisi zenye misingi imara na sio kwa ubabe wa mtu mmoja
 
Hiyo miaka mitano inatosha kupata somo na watu wakaheshimiana. Kwenye kila nchi lazima damu za watu zimwagike kusimamisha misingi imara ya kiutawala.
 
Hiyo miaka mitano inatosha kupata somo na watu wakaheshimiana. Kwenye kila nchi lazima damu za watu zimwagike kusimamisha misingi imara ya kiutawala.
Damu ya akina Saanane na akina Lissu mliyomwaga haitoshi?
 
Mimi nilifikiri ungeuliza nchi gani ya kidikteta imeendelea?

Nchi zaidi ya asilimia 90 zilizoendelea ni za kidemokrasia. Dictatorship labda China tu.

Afrika yote sehemu kubwa madikteta tu na huku ombaomba
Akili hauna...kuna aina mbili za udictotor nazo ni
1) U dictator wa ndani ya nchi
2) U dictator wa nje ya nchi

Na kila kwenye hizo aina mbili ndani yake kuna makundi mawili
A) U dictator dhidi ya nchi
B) U dictator kwa ajili ya nchi

Kama ungekuwa na akili ungejua nchi zinazo jidai za ki democracy unazo ziongelea wewe kama Marekani. Uk ,ufaransa nizaki dictator pia katika AINA YA 2B hizi nchi zenye kufata aina hii ya udictor zenyewe nazo huwa tajiri kwa kupitia aina hii ya u dictator......Nchi nyingine ambazo huwa tajiri kwa u dictator ni AINA YA 1B ......Sasa hapo utaona ni namna gani u dictator unavyo fanya kazi ....ila kuna AINA 2A NA 1A hizi aina za u dictator ndiyo mbaya na zenge kuaribu taifa lolote lisiwese kuwa na maendeleo....HIVYO NI MTU MPUMBAVU ADHANIAYE KUWA MAREKANI SIYO DICTATOR.....MAREKANI NI DICTATOR WA KIMATAIFA KWA AJILI YA NCHI YAKE.
 
Naomba mnisaidie wadau ni nchi gani duniani imepiga hatua za maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya demokrasia ?

Jinga jinga hivi kwanini wakimbizi wanakimbilia EU, USA na Canada na sio China na Urusi?
 
Wewe inaelekea hata hujui historia ya dunia. Hao scandinavia walifaidika na utumwa wa wapi?

Sisi tumepata uhuru 1961 tunazidiwa na nchi za Ulaya zilizopita uhuru 1990?
Mlipata Uhuru gani?Kuna nchi hata moja ya Afrika ambayo iko huru? Namna nzuri ya Afrika kuendelea ni kutumia dictatorship tu siyo democracy hapana
 
Pia lazima tufahamu kati ya democracy na dictatorship kipi kianze. Nchi za magharibi zilianza na udikteta baada ya kupiga hatua katika nyanja za maendeleo na ustaharabu Wakashift kwenda Kwenye democracy.
Africa ni vice versa tumeanza na democracy 🤣🤣
Hakuna democracy kwenye jamii masikini na isiyostaharabika.
Misingi ya German ya Leo ilijengwa na Adolph Hitler.
Lkn walishift baada ya kuona udictator hauwafikishi popote.Ni kama ulivyo ujamaa na ubepari
 
U.S.A, Canada, Ulaya hawa maendeleo yao kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na shughuli za ukoloni na utumwa na nafikiri wafahamu yale watumwa waliyokuwa wakitendewa ni kinyume kabisa na vitabuni demokrasia inavyo elekeza.
Hakuna mahali udikteta ulileta maendeleo.

China chini ya udikteta wa kijamaa ilikuwa hoi bin taabani. Mpaka miaka ya karibuni ilipoamua kulegeza mifumo ya kiutawala. Hata hivyo, kwa rasilimali ilizo nazo na uwingi wa watu, haikustahili kuwepo mahali ilipo.

USSR chini ya udikteta wa kijamaa ilikuwa hoi mpaka miaka ya 1990 ilipoomba kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, ambayo kabla ya kuipa msaada, yaliipa USSR masharti ya kuzingatia demokrasia, masharti ambayo yalisababisha kufa kwa USSR, na hali ikawa na unafuu, japo mpaka leo Urusi demokrasia yake ni dhaifu. Na laiti kama Russia ingekuwa na demokrasia imara, kwa kuzingatia rasilimali ilizo nazo, ingekuwa na maendeleo ya kiwango cha juu sana, lakini inaburutwa kiuchumi na mataifa mengi madogo kama South Korea.

North Korea, iliyokuwa juu zaidi kuliko South Korea, udikteta umeifanya iwe duni kabisa ukilinganisha na South Korea.

Ukiacha mataifa makubwa, nchi zenye demokrasia nzuri kabisa, ni Nordic countries, na zile za Mashariki zenye uchumi wa kasi kama vile Singapore, Thailand, Malaysia na Hong Kong. Zote zina maendeleo ya hali ya juu ukilinganisha na mataifa yanayoongozwa kidikteta.

Udikteta ni laana, unaua maendeleo yote kuanzia yale ya kiuchumi, kitekinolojia mpaka ya kijamii kama vile amani na furaha ya wananchi.
 
Back
Top Bottom