Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Kama umezaliwa na mtumwa utumwani ni ngumu kutokuwa mtumwa
Hata wamarekani weusi, kabla na baada ya wale milioni nne, walizaliwa hivyo, lakini walikataa maslahi ya kitumwa! Hadi Leo, the saga continues!
 
Ni kupoteza muda kuandika juu maoni ya mtu. Jikite kuandika issues - namna ya kupata maendeleo na siyo mtu kasema au kafanya nini.
 
Mdude hajakosea

Na mimi nasema hivi, kama Samia atafuata njia ileile ya kidikteta ya Magufuli, basi wembe uleule tuliotumia kumnyoa Magufuli tutamnyoa nao na yeye pia.

Mimi nampongeza Mdude kwa kauli nzuri kabisa ya kijasiri.

Kama Mdude kakosea mpelekeni mahakamani

Nyoka wa kkbisa wewe. Jitokeze wewe. Sio ushabiki wa kipumbavu.
 
DEMOKRASIA HAIWAFAI WATU AINA YA MDUDE CHADEMA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Mwaka juzi niliandika makala moja iliyokuwa ikimuonya na kumrekebisha Mwanaharakati na mwana chama wa Chadema, Ndugu Mdude Chadema kuwa ukosoaji wake haufai kwani anatumia lugha chafu zilizochanganyika na matusi.

Napenda wakosoaji, warekebishaji, Wanaharakati, ambao Wana misimamo mikali na wenye lugha ngumu lakini zisizo chafu wala matusi.

Mdude Chadema yakupasa ujirekebishe tena Kwa sehemu kubwa.

Kama ulivyozoea kukosoa basi Leo hii natumia nafasi hii kukukosoa kuhusu ukosoaji wako, ikiwa hii ni mara ya pili tangu nilipokukosoa mwaka 2019.

Tumia Lugha Kali Kama za wenzako kina Malisa, Maria Sarungi, Fatma Karume, miongoni mwa wengine.

Usije sema wewe u-unique wako ni kutumia lugha chafu zenye matusi. Huo ni Upumbavu.

Niliwahi andika kuwa Demokrasia haiwafai watu Masikini na Wapumbavu.

Wapumbavu wao huitumia demokrasia Kama kichaka cha kutukana wengine, kuwadhalilisha, kuwavua nguo Kwa matusi ya nguoni kabisa.

Watu dizaini ya Mdude Chadema huweza kuvumilika Kwa Watawala wenye dharau, wanaowapuuza, na wasiojali watu wapumbavu.

Lakini Kwa Watawala wasioweza kuvumilia, watu mithili ya Mdude huweza kujikuta katika taabu, dhahama na shurba isiyoelezeka.

Mdude Chadema Kwa vile hawezi kujizuia mipaka yake ya kuongea ni hatari ikiwa atakutana na mtawala asiyejua naye kujizuia mipaka yake ya mamlaka.

Hii ni kusema,
Mdude atatumia Uhuru wake wa kuongea vibaya.
Na mtawala naye atatumia Madaraka yake vibaya.

Hata hivyo,
Mdude Chadema anaweza akawa jasiri Jambo ambalo ni zuri, lakini kuwa jasiri kipumbavu ni Jambo baya.

Uwezo mzuri wa Mdude wa kuonyesha ujasiri wake ingependeza Kama angeutumia Kwa njia nzuri ya kukosoa kama mtu mwenye hekima.

Vita ya Mdude kipindi cha nyuma dhidi ya utawala wa JPM ilikuwa vita nzuri lakini iliyoharibiwa na wachezaji, wote Mdude na JPM.
Mdude alikuwa na hoja, lakini alikuwa akizitoa Kwa njia chafu na matusi Jambo ambalo halikuwa zuri na nilimtahadharisha.

Wembe alioutumia Mdude awamu ya JPM unafahamika, ulikuwa ni wembe wenye lugha chafu, matusi na lugha zenye ukakasi. Ndio maana mpaka naandika hapa ni kutokana na kuielewa kauli yake Kwa namna hiyo, nikikusudia kumtahadharisha na kumuomba atumie mbinu nyingine.
Kwa maana Kama atatumia wembe ule ule basi mtawala naye Hana budi kutumia shoka Kama alivyokuja akifanya JPM.

JPM naye hakuona ulazima wa kutumia busara Kwa kijana atumiaye upumbavu kumshambulia. Matokeo yake tunayajua.

Mdude na wenzako WA namna yako.
Lazima uelewe kuwa kanuni ya mapambano au vita hutumia Mirror principles ambapo unashambuliwa kadiri unavyokuja.
Ukija unacheka utashumbuliwa unacheka, ukija unapiga mayowe utashumbuliwa wakiwa wanapiga mayowe.

Kanuni za kioo ambazo huzingatia law isemayo input is equal to output ndio msingi WA mapambano.
Wahenga walisema; Dawa ya Moto ni Moto.

Mdude Chadema sitaki kuamini kuwa wewe ni mpumbavu ambaye Demokrasia huiwezi.

Tafadhali, fanya Sub katika mapambano yako, ingiza akili na hekima alafu mtoe upumbavu akae bench Kwanza.

Siku zote ukitumia upumbavu basi matokeo yatakayo kupata yatafanana kiwango cha upumbavu uliowekeza. Halikadhalika na ukitumia akili, hekima na maarifa.

Pambano liendelee lakini tahadhari zizingatiwe, sheria za mchezo zisipuuzwe.

Linda nchi yako, penda watu wako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro

Wembe ni ule ule
 
Kwa wenzetu msio ona shida kutumia dhulma, utekaji/kudhuru, vitisho na mbinu chafu kama hizo kuwanyamazisha mnaopingana nao mawazo, Mdude kupitia aliyopitia akabaki na misimamo yake bila ya kuonyesha amekuwa broken, litakuwa ni jambo la kuogopesha sana.
 
Kayabebe Mateso aliyofanyiwa NYAGALI ..ndo uje UTAPIKE HAPA

Aliyemfanyia mateso yupo wapi?

Wote tunafahamu, Kama angekuwepo mdude bado angekuwa nyuma ya nondo kivyovyote.

Lengo langu sio kumtetea yeyote Bali kuweka Suluhu.

Mdude asivuke mipaka Kwa upumbavu,
Asijefanyiwa maamuzi ya kipumbavu na viongozi wapumbavu

Yaani dawa ya Upumbavu ni upumbuvu
 

Wembe ni ule ule

Wembe wa Mdude Nani asioujua?
Ndio maana nimemtahadharisha tuu ili asije analalamika wenzake nao wakitumia shoka lile lile
 
Kwa wenzetu msio ona shida kutumia dhulma, utekaji/kudhuru, vitisho na mbinu chafu kama hizo kuwanyamazisha mnaopingana nao mawazo, Mdude kupitia aliyopitia akabaki na misimamo yake bila ya kuonyesha amekuwa broken, litakuwa ni jambo la kuogopesha sana.

Utekaji umeusikia lini sheikhe?

Hayo mambo tuliyakemea na yakitokea tutayakemea Sana tuu.

Lakini na watoa kauli chafu nao tutawakemea.
 
Wembe wa Mdude Nani asioujua?
Ndio maana nimemtahadharisha tuu ili asije analalamika wenzake nao wakitumia shoka lile lile
Shoka limeshatumika kwake na kwa wengine wengi tayari...
IMG_20210704_153830.jpg
 
Mdude hajakosea

Na mimi nasema hivi, kama Samia atafuata njia ileile ya kidikteta ya Magufuli, basi wembe uleule tuliotumia kumnyoa Magufuli tutamnyoa nao na yeye pia.

Mimi nampongeza Mdude kwa kauli nzuri kabisa ya kijasiri.

Kama Mdude kakosea mpelekeni mahakamani
SikU Zote nilikuwa na wewe Mkuu Missile of the Nation katika kuoambana na DIKTETA Magufuli. Kwa hili sikubaliani na wewe.

Rais SSH ni muungwana, msikivu, mpenda haki na tumeona anavyojiyahidi kuleta utawala wa Sheria na demokrasia kwa kipindi kifupi.

Tumlinde Rais wetu dhidi ya Vichaa kama Mdude. Tumkosoe kwa staha kama alivyoagiza.

Rais SSH ni tunu Mungu katuzawadia, na kama tutaitumia vibaya tutegemee mabaya kuliko ya DIKTETA Magufuli.
 
Uzuri wa Mdude ni confidence aliyonayo, anaongea mawazo yake kwa uwazi na anatafuta platform sahihi.

Anatapotakiwa kujiweka sawa ni uwezo wa kujenga hoja kwa kutumia maneno ya busara. Akiwa na hivi viwili atakua kiongozi bora zaidi.
Mdude ana Historia ngumu sana. Hajui hata wazazi wake wako wapi, wala hajui kwao ni wapi. Hata viongizi wa CDM hawajui whether ni Mtanzania au Mkongo . Alizaliwa akajikuta anaishi tu na wasamaria wema. Up bringing yake ndiyo inamfanya awe kama myama, yaani fearless.

Siyo kwamba ana ujasiri bali maisha kwake hayana maana. Yuko kama mnyama akifa sawa, akijeruhiwa sawa, akilala shimoni sawa.

Mwenye akili nzuri, malezi na familia hawezi kutoa kauli kama Ike siku 3 tu baada ya kutoka kwenye mateso kama yale
 
Kauli ya kibabe sana na hakuna tusi lolote pale sema tu wabongo wengi ni wanafiki sana, kama Samia ataleta pigo kama za mtangulizi wake mdude anasema hatakaa kimya lazima harakati zake ziendelee tu, ebu tujiulize je magufuli alinyolewa na wembe gani ili tujue tusi liko wapi hapo
 
Kuna yule wa uvccm aliyetaka wapinzani kuuwawa. Yule mbunge mama mwingine aliyesemea bungeni kutaka mbunge wa upinzani auawe.

Vipi yule aliyewauwa kina Azory Mawazo Ben. Aliyewajeruhi kina Lissu, kudhulumu watu, nk.

Kuna ushauri wowote mliwahi kuwapa au ni machozi mengine ya mamba tu?
huyu fala wa lumumba ROBERT HERIEL akili ubongo wake umeishia kwa MDUDE tu hao wengine yaliyowapata ni sawa tu kwake. shwain sana huyu
 
Wapi ametukana na kutumia lugha chafu??

Kuhusu kupigwa risasi Lisu, utekaji, mauaji ya kihole holela yote hayo tuliyapinga Kwa nguvu moja.

Ninachokisema hivi leo ni kuwa matokeo ya hayo hutokana na uvukaji wa mipaka baina ya wapambanaji.

Mmoja anatumia lugha mbaya na chafu(kavuka mipaka yake)
Mwingine anatumia Madaraka yake vibaya (kavuka mipaka yake) ili kumtuliza hasimu wake
toa hoja moja tu humu uliyowahi kueleza kuulizia wapi alipo Ben SANANE.. AZORI na wengineo.. vinginevyo wewe ni ndezi tu
 
Back
Top Bottom