Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Wembe uliotumika ndio uliojadiliwa hapa Mkuu

Umeeleweka na tumemwelewa Mdude Chadema...

Swali ni hili;

Kuna tusi gani hapo? Hiyo ni lugha kali na ni kweli...

Wanasiasa wote ni "Makenge" na wanahitaji kufikishiwa ujumbe unaowahusu kwa lugha kali kali kabisa ili waelewe...

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake Magufuli....

He was strongly and brutally criticized and foolishly, he reacted the same way and even worse...

Wewe hofu yako ndo iko hapo...

Kwamba, "unamwonea huruma" Mdude Chadema kwa sbb Rais Samia akiamua kuwa brutal kama Mwendazake, basi Mdude ataumia, atarudi gerezani...!!

Wewe huwa unaandika makala za kiimani. Na kwenye ukristo huwa unagusa. Kwa hiyo unaujua ukristo. Unaijua Biblia...

Je, unamjua Yesu Kristo na harakati au kampeni yake ya miaka 3 na nusu ya kuwaelimisha watu juu HAKI na WAJIBU wao hapa duniani...??

Kwa ujumla, kampeni au harakati za Yesu Kristo hapa duniani zilikuwa dhidi ya tawala OVU na DHALILI za binadamu wa dunia hii. Na watawala walimchukia kweli kweli maana deal zao zilivurugwa....

Kuna wakati Yesu Kristo mbele yao hao watawala aliwahi kuwaita "....enyi watoto wa uzao wa shetani/ibilisi........"

Hii ni lugha kali kweli na yaweza kuwa ya matusi kwako, au siyo..??

Kama ndiyo, unadhani watawala wa dunia ya leo akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, wana tofauti gani na watawala wa Kiyahudi na Warumi ya kale...??

Watawala hawa ni sharti wakosolewe kwa lugha ile wasiyoipenda ili katika kujibu (ku - react) kwao, wafanye makosa ya kiufundi na wajiue au wajihàribu wenyewe...!

Magufuli alifanya hivyo, akafa...

Warumi na wayahudi walifanya vile dhidi ya Yesu Kristo, wakafa wenyewe na Yesu yu hai leo na hata milele...!!
 
Umeeleweka na tumemwelewa Mdude Chadema...

Swali ni hili;

Kuna tusi gani hapo? Hiyo ni lugha kali na ni kweli...

Wanasiasa wote ni "Makenge" na wanahitaji kufikishiwa ujumbe unaowahusu kwa lugha kali kali kabisa ili waelewe...

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake Magufuli....

He was strongly and brutally criticized and foolishly, he reacted the same way and even worse...

Wewe hofu yako ndo iko hapo...

Kwamba, "unamwonea huruma" Mdude Chadema kwa sbb Rais Samia akiamua kuwa brutal kama Mwendazake, basi Mdude ataumia, atarudi gerezani...!!

Wewe huwa unaandika makala za kiimani. Na kwenye ukristo huwa unagusa. Kwa hiyo unaujua ukristo. Unaijua Biblia...

Na unamjua Yesu Kristo na huduma yake ya miaka 3 na nusu hapa duniani...

Kwa ujumla, huduma ya Injili ya Yesu Kristo hapa duniani ilikuwa juu ya tawala onevu na dhalili za dunia hii...

Kuna wakati Yesu Kristo mbele yao hao watawala aliwahi kuwaita "....enyi watoto wa uzao wa shetani/ibilisi........"

Ni lugha kali na ya matusi eti..??

Kama ndiyo, unadhani watawala wa dunia ya leo akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, wana tofauti gani na watawala wa Rumi ya kale...??

Watawala hawa ni sharti wakosolewe kwa lugha ile wasiyoipenda ili katika kujibu (ku - react) kwao, wafanye makosa ya kiufundi na wajiue menyewe...!

Magufuli alifanya hivyo, akafa...

Warumi na wayahudi walifanya vile dhidi ya Yesu Kristo, wakafa wenyewe na Yesu yu hai leo na hata milele...!!

Lugha Kali haijakatazwa Ila lugha CHAFU yenye matusi dooh.
 
Nyakati zinabadilika mkuu, vivyo hivyo namna kwa namna ya mbinu za kimaisha, maudhui na namna ya kudeal na mambo hubadilika pia. CD RW au DVD iliyokuwa deal miaka 10 nyuma kwa sasa si deal tena kwa flash dish, na flash disk ya MB 512 ilikuwa deal miaka kadhaa nyuma huwezi muuzia mtu kwa sasa hata kwa 500, sababu Kuna Flash za 64 kwa elfu kumi tu. Nachotaka kusema hapa kwa ufupi tu ni ya kuwa kila zama na kitabu chake.
Kuna yule wa uvccm aliyetaka wapinzani kuuwawa. Yule mbunge mama mwingine aliyesemea bungeni kutaka mbunge wa upinzani auawe.

Vipi yule aliyewauwa kina Azory Mawazo Ben. Aliyewajeruhi kina Lissu, kudhulumu watu, nk.

Kuna ushauri wowote mliwahi kuwapa au ni machozi mengine ya mamba tu?
 
Nanukuu tu "washughulikie huko bungeni, mimi nawashughulikia huku uraiani, "wapinzani wanapaswa kuchomwa sindano za sumu" ...n. k
 
Mdude hajakosea

Na mimi nasema hivi, kama Samia atafuata njia ileile ya kidikteta ya Magufuli, basi wembe uleule tuliotumia kumnyoa Magufuli tutamnyoa nao na yeye pia.

Mimi nampongeza Mdude kwa kauli nzuri kabisa ya kijasiri.

Kama Mdude kakosea mpelekeni mahakamani
Huku nako Steven Nyerere kaweka yake
"Nashangaa ma CD, RC hawajamueeka ndani kwa maneno aliyo sema"
~Stevennyerere
 
JPM alikuwa mtu mwema......
huyu kijana angekutana na madikteta siku nyingi angekuwa mchangani.....
Dikteta fashisti Hamnazo alikuwa mtu mwema?
Kuua watu, kushambulia watu kwa risasi na hata kumbambikia Mdude kesi ya ngada?
Ama kweli alikuwa mtu mwema.
 
Tumefika wakati kila maneno ya upinzani yanaitwa matusi sijasikia tusi lolote. Watanzania sio wajinga siku hizi kuna video kila mahali huwezi kulisha watu maneno. Kama unataka demokrasia ndiyo hii na yuko sawa Mungu atarekebisha hii nchi hataki iwe ya ki dikteta hivyo hapa ni kupigana na Mungu sio mdude. Ulisema hatutaki demokrasia Magu yuko wapi leo
 
Chanzo cha tatizo unafikiri sikijui???

Mdude anahoja nzuri lakini uwasilishaji wake ni wahovyo, sitegemei Kama atapewa majibu ya maana isipokuwa ya hovyo Kama alivyowasilisha.
Kwa kauli yako sasa umeamua kilinda chanzo cha tatizo kwasababu mlalamikaji alitumia lugha kali, hebu niambie, una hakika angetumia lugha laini ndio angejibiwa au ndio tatizo lingeongezeka? hiki ulichoandika hapa hakina mantiki.
 
Kwa Chadema lugha anayotumia huyo kijana ndio lugha tukufu katika chama chao! Anapongezwa sana kwa kuharisha kwa kutumia kinywa
Mkuu tujaribu kuweka mizani sawa. Yule aliyemtukana mwananchi ambaye alitaka kutoa maoni kuwa kalisha matakle chini alikuwa sahihi?

Mwendazake alipokuwa anawaita watu wapumbavu ilikuwa sana?

Nape alivyosema kuwa ikulu siyo ya wagonjwa alikuwa sawa?

Unakumbuka hawa watu Akwelina, Azwory, Ben sanane, Tundu Lisu?

Tukio la Sabaya la kuvamia wananchi, Makonda kumdhalilisha Waryoba, kuvamia Clouds Fm, tukio la uundwaji wa Task Force iliyokuwa ipora watu mali zao?

Tukio la MDUDE ni minor issue sana ukilinganisha na matukio ya CMM katika kukiuka haki za raia wake.
 
Lugha Kali haijakatazwa Ila lugha CHAFU yenye matusi dooh.
Mbona hujibu swali la msingi "Taikon wa Fasihi...??"

Lugha chafu ni ipi?

Matusi ni nini hasa?

As far as I know, tafsiri ya "tusi" is not universal. Unachokitafsiri kuwa tusi kwako inaweza ikawa siyo tusi kwangu au kwa mwingine...

Generally, tafsiri ya neno "tusi" iko kwa mtu mwenyewe anayesikia au kusoma...!

Nyie mliyemsikia au kumsoma Mdude Chadema, hebu tupeni "universal definition ya " tusi" na "lugha ya matusi" na "lugha chafu"

Kisha onesheni matusi na uchafu wa Mdude Chadema ktk aliyoandika/kusema...

Na kwa upande wa Rais Samia Suluhu Hassan, anatakiwa kutiwa moyo kuwa anaongoza watu karibu au zaidi ya 60,000,000...

Akifanya kosa la Kimagufuli na kudhani kuwa hawa watu wote wanaweza kuimba wimbo unaofanana kumsifu yeye, ataumia asubuhi tu....

Kwenye siasa kuna principle moja muhimu sana ktk demokrasia tulifundishwa shule. Inaitwa "political tolerance"...

Tumtie moyo Mama Samia Suluhu Hassan kuwa na political tolerance hata kama wakati fulani atahisi kuwa anametukanwa...

Mbona mwenzake Tundu Lissu amepigwa mpaka risasi lakini kamwe hajajibu kwa risasi bali anaendelea kutumia mdomo wake uleule kupambana...?

Nadhani jibu ni rahisi sana kwa swali hili....

Kwamba, maneno au mdomo una nguvu ya kubadilisha mambo/hali kuliko risasi au jeshi au UWT....!!

Kelele zote hizi ni kutaka kuziba midomo ya kina Mdude, Lissu, Mbowe, CHADEMA nk nk...

Hawataweza kamwe...!!
 
ROBERT HERIEL acha double standard kauli ya Mdude ni nyepesi kuliko ya Herry James, kuliko ya Magufuli kuliko ya Samia mwenyewe kipindi cha kampeni.

Utapimiwa kwa kiwango kile kile utoacho. Tumefika hapa kwasababu kuna watu wanaamini wana haki kuliko wengine, wanastahili heshima kuliko wengine, wanajiona miungu watu naona miaka mitano hamjajifunza mnataka kurudi kwenye kuabudu watu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
ROBERT HERIEL acha double standard kauli ya Mdude ni nyepesi kuliko ya Herry James, kuliko ya Magufuli kuliko ya Samia mwenyewe kipindi cha kampeni.

Utapimiwa kwa kiwango kile kile utoacho. Tumefika hapa kwasababu kuna watu wanaamini wana haki kuliko wengine, wanastahili heshima kuliko wengine, wanajiona miungu watu naona miaka mitano hamjajifunza mnataka kurudi kwenye kuabudu watu.

Enzi za mwendazake aliyekuwa anashambuliwa ni kiongozi Mkuu, huyo Kheri James ni mama dagaa tuu.

Hukuona waliokuwa wakimkosoa mwendazake??
 
Akili ya mwafrika ndo maana hata sasa ni watumwa. Hata Wakoloni muliwaona kuwa ni baba na mama zenu. Wtf?!
 
Back
Top Bottom