Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

Mda ukifika kila mmoja anabaki na plot yake , hakuna kuhurumiana
 
Nyinyi wenye akili kubwa na fikra tunduizi ndiyo hamtakiwi nchi hii!
Mimi nimehoji kuhusu ukarabati wa kivuko kwenda Kenya badala ya kumpa Songolo,Msigwa ameni-block!
Ukitaka jenga, ukaomba quotation, Ndugu yako mliye mkoa 1 akakuletea quotation ya 10mil kwa kazi uliyotaka, akajitokeza mtu wa mbali sana kwa kazi hiyo hiyo akaifanya kwa 7.5mil utampa nani kazi?
 
Hivi Mkapa aliwezaje kuendesha Nchi Kwa miaka 10 bila kukopa hata sent Tano?

Yaani HAKUKOPA, bt alihakikisha analipa madeni ya watangulizi.

Hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya ml 60 tukimtafuta mtu wa aina ya Mkapa tutampata?
Achana na kile kichwa kiiliheshimu mifumo na taasisi mbalimbali ndiyo maana alifanikiwa sana kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia.
 
Zero debt, katika nchi zenye madeni Africa hatupo hata kwenye 30 bora, Nchi ya kwanza kuwa na deni kubwa ni Cape Verde na wapo poa tu, hakika tunapozungumzia suala la madeni Tanzania ni kama hatudaiwi kabisa, Kenya kidogo wapo juu maana wapo kwenye kumi bora katika madeni, heko ccm kwa kukopa kwa umakini mikopo hii kwa ajili shughuli nyeti tu na za msingi kabisa.
 
Ukitaka jenga, ukaomba quotation, Ndugu yako mliye mkoa 1 akakuletea quotation ya 10mil kwa kazi uliyotaka, akajitokeza mtu wa mbali sana kwa kazi hiyo hiyo akaifanya kwa 7.5mil utampa nani kazi?
Nampa Ndugu yangu kwasababu hela itabaki nyumbani,kuongeza mzunguko wa pesa.
 
Hivi Mkapa aliwezaje kuendesha Nchi Kwa miaka 10 bila kukopa hata sent Tano?

Yaani HAKUKOPA, bt alihakikisha analipa madeni ya watangulizi.

Hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya ml 60 tukimtafuta mtu wa aina ya Mkapa tutampata?
Mahitaji yameongezeka

Serikali imejiingiza katika yasiyo wahusu mf kusomesha watoto

Serikali imeamua kujenga shule, vituo vya afya, zahanati, hospital, barabara, mabwawa, mbolea etc.

Kodi yetu haiwezi kabisa.
Makusanyo yetu ni Tril 28
Bajeti yetu ni Tril 41
Mwaka huu itafika Tril 45
 
Deni la serikali ya Tanzania limeongezeka na kufikia trilioni 76 mpaka Januari 2023 kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania, hi ikiwa ni ongezeko la trilioni 4 toka Septemba 2022. Takribani asilimia 65.2 ya deni hili ni deni la nje huku asilimia 34.7 ikiwa ni deni la ndani ambalo ni jumla ya trilioni 26.4.

Kwa kuendesha miradi mikubwa mikubwa kwa pamoja, ambapo sehemu kubwa miradi hiyo imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha za kigeni, Tanzania imejikuta katika shinikizo kubwa la kutafuta mikopo ili kuweza kufidia mapungufu katika bajeti yake.

Madhara ya mtikisiko katika anga ya kimataifa pia yameongeza makali, hii ni kutokana na Tanzania kuhitaji fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa kuliko fedha zinazoingia kupitia mauzo ya nje.

Mijadala mikali imekua ikiendelea nchini juu ya deni la taifa, juu ya ustahimilivu wake. Kwa kutumia ripoti ya tathmini inayofanywa na Benki ya Dunia, IMF a serikali ya Tanzania, serikali ya Tanzania imekua ikieleza kuwa bado deni la serikali ni stahimilivu.

Hata hivyo wadau wa uwajibikaji wamekuwa wakitaka maboresho zaidi kwenye mfumo wa ukopaji, ikiwemo kuongeza wadau katika Kamati ya Madeni ya Taifa ambapo kwa sasa inaongozwa a Wizara ya Fedha kupitia Katibu wake. Wadau wanaopendekezwa kuongezwa ni Bunge la Tanzania, kama uwakilishi wa wananchi.

Wadau kama Muunganiko wa Azaki Katika Mikopo na Maendeleo (TCDD) wamekua wakishauri kuwepo na mfumo wa kikomo cha kukopa (debt celieng), katika mtiririko mzima wa ukopaji Tanzania.

Chanzo: The Chanzo
Ila msishau kwamba deni la Nchi ni sawa na Deni la serikali na private sector.
 
Zero debt, katika nchi zenye madeni Africa hatupo hata kwenye 30 bora, Nchi ya kwanza kuwa na deni kubwa ni Cape Verde na wapo poa tu, hakika tunapozungumzia suala la madeni Tanzania ni kama hatudaiwi kabisa, Kenya kidogo wapo juu maana wapo kwenye kumi bora katika madeni, heko ccm kwa kukopa kwa umakini mikopo hii kwa ajili shughuli nyeti tu na za msingi kabisa.
Tunahitaji kukupa zaidi mikopo kama hii ili.kuifungua Nchi.
 
Hizo ni siasa tu
Kwaiyo pale unaona serikali imefanya fair?wakati tuna uwezo wa kuifanya kazi ndani ya nchi!
Unatoa tender kwa kampuni ambayo ina uwezo wa kufanya kazi kuzidi ya ndani.Sasa Songoro anajenga Meli,atashindwa kukarabati lile sinia la Kivukoni kweli!
Yaani sawa na serikali ya China kuipa Uturuki kazi ya kuijengea reli wakati na yenyewe ina uwezo mkubwa!
 
Tusemezane ukweli kwenye issue ya kivuko kuna upuuzi umefanyika tena wa hali ya juu kabisa!
 
kiongozi wangu mkuu Gadafi mpaka mauti nchi yake haikiwa inadaiwa lakini ilikuwa ikikopesha
 
Mahitaji yameongezeka

Serikali imejiingiza katika yasiyo wahusu mf kusomesha watoto

Serikali imeamua kujenga shule, vituo vya afya, zahanati, hospital, barabara, mabwawa, mbolea etc.

Kodi yetu haiwezi kabisa.
Makusanyo yetu ni Tril 28
Bajeti yetu ni Tril 41
Mwaka huu itafika Tril 45
Mkapa alifanya yote hayo bila kukopa.

Shule, Barabara zilijengwa, na mikopo Kwa wanafunzi vyuo alitoa Si degree pekee, Hadi certificate walikopeshwa😳😳
 
Swali jingine; Hii wanapoenda kukopa bila idhini yetu, Huwa wanaweka BOND au DHAMANA zipi?

Maana wanatuambia hii ni nchi MASKINI bt hapo hapo wanasema TUNAKOPESHEKA.

Hivi Kuna maskini ANAEKOPESHEKA?

Mbona mtaani maskini akienda bank kukopa pesa na Hana dhamana hutimuliwa?
Ndio maana mikopo tunayopewa Ina kiwango,huwezi kopeshwa til.3 na zaidi at once.
 
Kwaiyo pale unaona serikali imefanya fair?wakati tuna uwezo wa kuifanya kazi ndani ya nchi!
Unatoa tender kwa kampuni ambayo ina uwezo wa kufanya kazi kuzidi ya ndani.Sasa Songoro anajenga Meli,atashindwa kukarabati lile sinia la Kivukoni kweli!
Yaani sawa na serikali ya China kuipa Uturuki kazi ya kuijengea reli wakati na yenyewe ina uwezo mkubwa!
Alishindwa kwenye ushindani wa bei,kazi za serikali hazigawiwi tuu kama nyanya.
 
Nampa Ndugu yangu kwasababu hela itabaki nyumbani,kuongeza mzunguko wa pesa.
Kwani malipo yatalipwa Kenya? Yaani uingiliwe zaidi ya Bilioni 10 kisa ndugu Yako? Subiri Ukiwa Rais wa juha ndio uje kufanya hivyo..
 
Back
Top Bottom