Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6 ndani ya mwaka. Chanzo ni ukopaji wa fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo

Hilo deni la ndani ndio linanitisha, ni kama Serikali inashindana na wananchi wake kukopa katika taasisi za fedha.

Serikali ipunguze Deni la ndani, na inapaswa itoe dhamana ktk mabenki kwa ajiri ya mikopo nafuu kwa raia na wafanyabiashara... Mikopo nafuu yenye riba ndogo na gharama kdg... Mzunguko wa pesa utaongezeka...
 
CCM ni chama janja janja sana. Deni linazidi kupaa halafu tunaambiwa miradi yote mikubwa inatumia fedha za ndani na zinazotokana na makusanyo ya TRA!!

Wizi mtupu!! Miaka mitano hakuna kupanda madaraja wala nyongeza ya mishahara.
 
[emoji854]
FB_IMG_16128586360763112.jpg
 
Huyo marekani mwenyewe anadaiwa na china, china mwenyewe anadaiwa, kwa hiyo ni jambo la kawaida tu
 
Ukikopa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo hili ni jema sana mbaya ni kukopa pesa kwa ajili ya kulipa mishahara.
Ikiwa miradi hiyo ina faida ni sawa kabisa. Tatizo ni kama faida haipatikani.
Mfano ndege wanasema ni shida, wataalam wanasema
 
DENI la Taifa limefikia Sh. trilioni 59 hadi kufikia Disemba mwaka jana, ikilinganishwa na Sh. trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 7.6, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.

Kati ya kiasi hicho, deni la ndani limefikia Sh. trilioni 16.2 na deni la nje Sh. trilioni 42.8. Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pamoja na kwamba deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu, serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wake, kwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani, kwa pato la Taifa ambacho kwenye mpango hakijaripotiwa.

Hayo yalibainishwa na Sillo Baran, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21), mapendekezo ya Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/22-2025/26) na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2021/22, na kusema wanashauri hilo kwa sababu deni la taifa uhudumiwa na makusanyo ya ndani na ni malipo ya lazima katika matumizi ya serikali.

“Vilevile kamati inaishauri serikali kukamilisha haraka mchakato wa nchi yetu kufanyiwa credit rating (kiwango cha mkopo) ili kuiwezesha serikali kupata mikopo nafuu na kwa urahisi,” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema Bunge kwamba kwa mujibu wa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanywa Disemba 2020, deni, ni himilivu kwa vigezo vyote vya kimataifa na hivyo, nchi ina uwezo wa kukopa ndani na nje, na kulipa mikopo hiyo bila kuwa na athari hasi kwenye ukuaji wa uchumi.

Katika maoni ya jumla ya kamati hiyo ya bajeti, serikali imeshauriwa kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.

Badala yake, serikali ijikite zaidi katika kuongeza udhamini wa wakopaji wadogo (credit gurantee schemes) pamoja na kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini yenyewe (lease finance).

Vilevile, serikali iangalie uwezekano wa kufungua zaidi soko la mitaji (liberization of capital market) ili kupunguza athari za serikali kukopa kwenye soko la ndani.

Chanzo: Nipashe

Atake asitake apewe miaka mingine 100 deni lifike Trilioni 900 itapendeza zaidi.
 
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
Hao Wadudu wakiwa sugu bado hatuwezi kuwakwepa maana ugonjwa hauna mipaka, tutaambukizwa haohao sugu...ndio maana umeenea kila nchi.
 
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
Jana niliasikiliza mahojiano kuhusu jambo hili.
Tahadhari inachukuliwa kwa sababu idadi ya chanjo ni ndogo kuliko idadi ya watu. Alijibu mtaalamu. Hii ni hata ya mwanzo, wanasayansi wanaendelea na utafiti zaidi
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
Sjaelewa hii inahusikaje kwenye uzi wa deni la taifa
 
DENI la Taifa limefikia Sh. trilioni 59 hadi kufikia Disemba mwaka jana, ikilinganishwa na Sh. trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 7.6, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.

Kati ya kiasi hicho, deni la ndani limefikia Sh. trilioni 16.2 na deni la nje Sh. trilioni 42.8. Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pamoja na kwamba deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu, serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wake, kwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani, kwa pato la Taifa ambacho kwenye mpango hakijaripotiwa.

Hayo yalibainishwa na Sillo Baran, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21), mapendekezo ya Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/22-2025/26) na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2021/22, na kusema wanashauri hilo kwa sababu deni la taifa uhudumiwa na makusanyo ya ndani na ni malipo ya lazima katika matumizi ya serikali.

“Vilevile kamati inaishauri serikali kukamilisha haraka mchakato wa nchi yetu kufanyiwa credit rating (kiwango cha mkopo) ili kuiwezesha serikali kupata mikopo nafuu na kwa urahisi,” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema Bunge kwamba kwa mujibu wa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanywa Disemba 2020, deni, ni himilivu kwa vigezo vyote vya kimataifa na hivyo, nchi ina uwezo wa kukopa ndani na nje, na kulipa mikopo hiyo bila kuwa na athari hasi kwenye ukuaji wa uchumi.

Katika maoni ya jumla ya kamati hiyo ya bajeti, serikali imeshauriwa kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.

Badala yake, serikali ijikite zaidi katika kuongeza udhamini wa wakopaji wadogo (credit gurantee schemes) pamoja na kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini yenyewe (lease finance).

Vilevile, serikali iangalie uwezekano wa kufungua zaidi soko la mitaji (liberization of capital market) ili kupunguza athari za serikali kukopa kwenye soko la ndani.

Chanzo: Nipashe
Mbona tuliambiwa kwa jinsi tulivyo vizuri kiuchumi sisi tutakopesha na miradi yote ya maendeleo ni fedha zetu za ndani. Kumbe JIWE ni muongo!
 
Hii taarifa ni ya kweli? tujilizishe kwanza chanzo chake maana kwa sasa tupo uchumi wa kati na tumeambiwa tutembee kifua mberee sisi ni matajiri...sasa hilo deni nani anakopa au wanatubambikia hawa mabeberu?
 
Ukikopa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo hili ni jema sana mbaya ni kukopa pesa kwa ajili ya kulipa mishahara.
Tatizo ni uongo. Mnatwambia mnatumia fedha za ndani kumbe uongo mkubwa. Haipendezi jitu zima kuwa ongo.
 
"Kwa fedha zetu za ndani" kumbe huwa wanamaanisha kinyume chake.Wakisema ni fedha za ndani maana yake ,ni kwamba mikopo tunayo chukua inalipwa na hela inayotokana na kodi za ndani lakini sio kwamba hela zinakusanywa na kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo moja kwa moja.

Madeni haya yatalipwa na vitukuu wetu
 
Umesema ukweli wenyewe [emoji23].

Ila ujue unapotembelea vieite la dezo unapoteza kabisa ufahamu wa kuelewa kuwa hii nchi bado ni masikini sana. Unapata taabu sana kuelewa inakuwaje mtu anakuwa ndani ya passo/ist/mwendokasi/daladala/bajaji/bodaboda/TZ 11... Kakosa uzalendo? [emoji848]

Maruweruwe ya vieite si mchezo.
 
Attachments

  • IMG_20210112_150518.jpg
    IMG_20210112_150518.jpg
    86.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom