Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6 ndani ya mwaka. Chanzo ni ukopaji wa fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo

Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6 ndani ya mwaka. Chanzo ni ukopaji wa fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo

Mbona tuliambiwa/aminishwa ni hela za ndani.
Hii nchi ina hela kweli kweli.....
Nasema uongo ndugu zangu??
 
Wewe ni mtaalam wa kitu gani? Huna unalojua kwa haya uliyoandika hapa.

Kwanza mada iliyopo haihusiani kabisa na ulichoandika. Inawezekana hata kusoma na kuelewa ni kwa taabu sana kwako!
You shakes up thread low concentrations you should ignore thats means your brain could be treamed easly
 
Sie tumekalia kukamuana tu.

Hii VAT ya Tanganyika na Zenji utadhani sio TZ.
 
DENI la Taifa limefikia Sh. trilioni 59 hadi kufikia Disemba mwaka jana, ikilinganishwa na Sh. trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 7.6, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.

Kati ya kiasi hicho, deni la ndani limefikia Sh. trilioni 16.2 na deni la nje Sh. trilioni 42.8. Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pamoja na kwamba deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu, serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wake, kwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani, kwa pato la Taifa ambacho kwenye mpango hakijaripotiwa.

Hayo yalibainishwa na Sillo Baran, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21), mapendekezo ya Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/22-2025/26) na Mwongozo wa maandalizi ya Mpango na bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2021/22, na kusema wanashauri hilo kwa sababu deni la taifa uhudumiwa na makusanyo ya ndani na ni malipo ya lazima katika matumizi ya serikali.

“Vilevile kamati inaishauri serikali kukamilisha haraka mchakato wa nchi yetu kufanyiwa credit rating (kiwango cha mkopo) ili kuiwezesha serikali kupata mikopo nafuu na kwa urahisi,” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema Bunge kwamba kwa mujibu wa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanywa Disemba 2020, deni, ni himilivu kwa vigezo vyote vya kimataifa na hivyo, nchi ina uwezo wa kukopa ndani na nje, na kulipa mikopo hiyo bila kuwa na athari hasi kwenye ukuaji wa uchumi.

Katika maoni ya jumla ya kamati hiyo ya bajeti, serikali imeshauriwa kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.

Badala yake, serikali ijikite zaidi katika kuongeza udhamini wa wakopaji wadogo (credit gurantee schemes) pamoja na kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini yenyewe (lease finance).

Vilevile, serikali iangalie uwezekano wa kufungua zaidi soko la mitaji (liberization of capital market) ili kupunguza athari za serikali kukopa kwenye soko la ndani.

Chanzo: Nipashe
Mbona kila siku tunaambiwa miradi yote ni pesa za ndani?
 
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
unazumgumzia technology ya zamani (iliyozoeleka) ya kutengeneza chanjo yaani kutumia kirusi cha ugonjwa husika kilichofubazwa
"Vaccines such as the inactivated polio vaccine, or most flu vaccines, use inactivated viruses to trigger a person’s immune system to respond to that disease-causing organism. In other vaccines, such as the hepatitis B vaccine, an individual protein made by that organism is injected instead to trigger a similar response."
Technology inayotumika sasa inaitwa mRNA "mRNA vaccines, however, trick the body into making the viral protein itself which, in turn, triggers an immune response."
. The (vaccine) mRNA will not enter the nucleus of the cells, where our DNA is.’
Once the injected mRNA enters a human cell, it degrades quickly and only stays in the body for a couple of days. This is why people need two injections to develop the best immune response.
Nadhani umeona tofauti iliyopo na ndiyo maana hii ni ya haraka zaidi
 
Deni la ndani ndilo linaloharibu mzunguko wa fedha ndani ya nchi serikali ione jinsi gani inaweza kulipa madeni ya ndani
Serikali ya CCM inaongozwa na washamba na malimbukeni haiwezi kufikiria namna ya kupunguza hilo deni la ndani
 
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
Linahusiana vipi na huu uzi??
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Cha kushangaza Mkuu BOT March 2018 ilidai deni limefikia 59 trillions. Miaka mitatu baadaye pamoja na riba kubwa na mikopo mipya bado deni limebaki 59 trillions 😂😂😂😂 wahuni hawa Mkuu ni hatari sana.
1612888081043.jpeg

Hiyo mikopo ni fedha zetu za ndani...ambae hajaelewa apige simu kwa Magufuli aeleweshwe
 
unazumgumzia technology ya zamani (iliyozoeleka) ya kutengeneza chanjo yaani kutumia kirusi cha ugonjwa husika kilichofubazwa
"Vaccines such as the inactivated polio vaccine, or most flu vaccines, use inactivated viruses to trigger a person’s immune system to respond to that disease-causing organism. In other vaccines, such as the hepatitis B vaccine, an individual protein made by that organism is injected instead to trigger a similar response."
Technology inayotumika sasa inaitwa mRNA "mRNA vaccines, however, trick the body into making the viral protein itself which, in turn, triggers an immune response."
. The (vaccine) mRNA will not enter the nucleus of the cells, where our DNA is.’
Once the injected mRNA enters a human cell, it degrades quickly and only stays in the body for a couple of days. This is why people need two injections to develop the best immune response.
Nadhani umeona tofauti iliyopo na ndiyo maana hii ni ya haraka zaidi
Huyo uliyemjibu ni matokeo ya juhudi zinazofanywa na serikali kulipumbaza taifa.

Tanzania will pay heavily in years to come for what it is not doing today.

Wizara yenyewe inayotakiwa iwe mbele kuhimiza wataalam wetu wafanye kila liwezekanalo kutumia janga hili kujinoa vyema, ndiyo wizara iliyo mbele kuwakatisha tamaa!

Hata hizo miti shamba wanazohimiza na kujifukizia, hawatafuti njia za kuzifanyia utafiti angalau kuzipa kiasi cha maelezo kwa nini zina/hazifanyi kazi!
 
yaan nchi na wana nchi wake hawajui matumizi ya mkopo, akikopa meananchi kwenye Taasisi ya kifedha matumizi kibao na kula bata majigambo mtaa mzima mtamkoma, baada ya muda mfupi unashangaa anatafuta mkopo wa kulipa deni mata kauza nyumba mara gari yaani inakuwa vangarati tu mtu kuchanganyikiwa, na nchi nayo hivyo hivyo majigambo meengi kumbe deni linazid kupaa(Tafadhari kabla ya kuchukua mkopo jipange vizuri na uheshimu huo mkpo/sio tuogope mkopo)
 
"Tunajenga miradi hii kwa pesa zetu za ndani" alisikika Raisi Magufuli akisema jukwaani
 
kwani deni huwa unalipa kupitia pesa za wapi za kwako mwenyewe ulizokusanya kodi

Unadanganya wananchi kuwa unakusanya over 1.3t kila mwezi, kisha deni la taifa linavuka waliokusanya kidogo! Wakati JK anatoka madarakani deni la taifa lilikuwa 39t+, hii maana yake ni kuwa Magufuli kakopa 1/3 ya marais wote wanne walio tawala nchi hii ndani ya 5yrs, huku akiwa hana mradi wowote aliomaliza unaozidi 1t+. Halafu kuna watu wanasema tuna bonge la rais. Eti deni ni pesa zako, je ukishindwa kulipa? Huyu anayekopa analipa bila kujali athari za madeni huko mbeleni kwa kusaka political millage maana anajua hatakuwepo madarakani, na hilo deni halitomuumiza yeye na kizazi chake.
 
Kitu kinachotia shaka kwenye hii chanjo ya covid-19 ni kwamba hata mara baada ya kupatiwa chanjo mtu hulazimika bado kujilinda kwa barakoa na taratibu zote kama zile zilizopaswa kutumika kabla chanjo haijatengenezwa sasa hapa chanjo inaumaana gani?

Je, chanjo hii ambayo mara nyingi huwa ni aina virus itakapofail nini kitatokea?kwa vyovyote wadudu watakuwa sugu zaidi may be 10 times hivyo RAIS wetu anaposema tusiwe na haraka juu ya chanjo hizi tumuelewe>

Chanjo zozote duniani zilipita stage mbali mbali ya kwanza ni watu wa kuwajaribia chanjo husika pili kuipa chanjo hiyo muda kuona jinsi gani ina fanya kazi [it should take even 3-5 years] baada ya hapo ndipo chanjo hiyo huthibitishwa rasmi na mamlaka husika za kimataifa zenye wajumbe labstechs toka nchi mbali mbali.

Nampa heko mkemia magufuli lets wait no hurry acha wengine wajaribiwe kwanza
Kwani mtoto unapomvisha pampers ndio unamwambia ajisaidie tu anavotaka jwa vile umemvisha pampers? Chanjo si sababu usichukuwe tahadhari.
 
Back
Top Bottom