Deni la Taifa laongezeka kwa asilimia 7.6 ndani ya mwaka. Chanzo ni ukopaji wa fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo

Mbona huwa anatuambia kwa ujasiri na sauti kubwa kuwa '''hii miradi inajengwa kwa pesa zetu wenyewe?''

Tunatekereza wenyewe, Mabeberu sio watu wazuri
 
Sjaelewa hii inahusikaje kwenye uzi wa deni la taifa
Huyu ametumwa kuharibu uzi

CCM hawataki kabisa watu wajadili maovu yao wanatumia kila njia kuhalalisha uharamia wanaofanya dhidi ya wananchi na kuwafunga midomo.
 
kukopa sio issue swala ni uwezo wa kulipa upo kama upo hakuna shida.Sasa anakopa halafu almost asilimia 80 inaenda miradi ya maendeleo hakuna shida zamani tulikuwa tunakopa kulipa mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa serikali ambao hawaingizi hata mia !!!! Sasa hivi mikopo inaenda kujenga mabwawa ya umeme miradi ya umeme kuhakikisha kila nyumba ina umeme mijini na vijijini matokeo watalipa bili pesa zitarudi ,miradi ya maji pia bili zitalipa pia miradi ya reli nk

tofauti ya Magufuli na watangulizi wake ni kuwa tulikuwa hatukopesheki ndio maana mikopo ilikuwa kiduchu na hata tukikopa nyingi zilikuwa zikienda serikalini tu kulipia wafanyakazi .Sasa hivi tunakopesheka ulitegemea deni la taifa lilingane na kipindi tulikuwa hatukopesheki hadli tunaunda tume za kwenda kuomba watupunguzie au kutufutia madeni kwa kuwa uwezo wa kulipa hatuna?
 

Twende taratibu ili ujue kuwa hujui. Ndani ya miaka hii mitano ya mwanzo amekopa 20t, huku akisema anakusanya zaidi ya 1.3t. Miradi pekee inayozidi 1t ni ya SGR na SG respectively. Miradi yake mingine ni chini ya 1t, ukiachia ndege zake 8 zilizofikia 1.8t ambazo huwa anasema amenunua kwa fedha za ndani. Hiyo miradi miwili ni ya 15t na hakuna wowote uliofikia 40% kwa mantiki kuwa hata kama ametoa hela, hazijafika 10t, je 10t nyingine aliyokopa kuingiza kwenye miradi gani? Na hiyo 1.3t+ - 1.8t huwa wanapeleka kwenye miradi gani? Hospitali Zote alizojenga na vituo vya afya na zilizoko kwenye hatua Za ujenzi hazijafikia 500b.Umeme wa rea ni kodi kila tukinunua umeme kuna 3% tunakatwa. Je unaweza kusema 10t aliyokopa kaipeleka wapi?
 
mfano umeenda benki kukopa milioni 200 ujenge nyumba kwani zote unazitumia mwezi mmoja?

pili kukopa waweza kopa kwa miradi tofauti mingine yaweza kuwa kwenye upembuzi au inatengelezwa miaka iliyobaki au iko kwenye stage ya tenda nk si kuwa iukikopa zote unazimaliza mara moja mara ingine haxitolewi zote mara moja hutolewa kwa instalments kuwa ukikamilisha stage unapewa zingine

Zikikopwa zipo zizonalipwa taratibu kutokana na progress ya miradi
 

Nilijua lazima upagawe kwenye hili. Kwahiyo hiyo 20t tumekopa lakini hatujapewa yote ama? Au hiyo 20t aliyokopa kuna nyingine bado iko bank? Kama kweli hiyo 20t aliyokopa iko bank, mbona hata kipande cha SGR Dar-Moro kimeshindikana kukamilika ndani ya 3yrs?
 
Miradi yote tunajenga kwa fedha za ndani
 
Tunajenga kwa pesa za ndani kama mwenyekiti wenu anavyotudanganya?
ndio kwani tukikopa tunalipa kwa pesa zao? si za kwetu wenyewe ziwe dola au za Tanzania lakini tutawalipa wa pesa zetu ukisema tunajenga kwa pesa zao labda uwe msaada wametusaidia bure lakini mkopo ni tunajenga kwa pesa zetu
 
Kukopa sio tatizo hata kidogo, tatizo hilo deni unaenda kufanyia nini? Kama ni matumizi ya kawaida na sio ya uwekezaji na kukuza uchumi, basi hapo ni tatizo.
 
Ukikopa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo hili ni jema sana mbaya ni kukopa pesa kwa ajili ya kulipa mishahara.
Inakuwaje kila siku unawaaminisha watu kuwa kila mradi unaoujenga ni kwa pesa za ndani?!!na hatukopi!!!siasa za kilagai za nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…