Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

MBUNGE WA MAKAMBAKO AT
Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.
Yule hata siyo wa kupoteza muda kujadili kauli yake. Mtu ambaye hata kuandika tu ni shida, na alipelekwa shule, nadhani hiyo inathibitosha kuwa hafundishiki, na watu wasiofundishika ni wale wenye low IQ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jah People akitumika kwenye njama za kihalifu ambazo hisia zangu zime asisisiwa na Jiwe na Ndugai
Siku zote wale wabunge vilaza kama huyu ndio hutumika kuanzisha njama hizi na kiitikio kitatoka kwa Joseph Kasheku Musukuma
 
Wabunge wa-darasa la saba ni mzigo kwa Taifa. Huyu "japipo" ndiye alikata mauno bungeni ulipokwama mchakato wa katiba mpya maana kulikuwa na kipengere cha sifa ya mbunge angalau awe na degree.
 
Kazi kuu ya Bunge ni pamoja na kuisimamia Serikali katika utekelezaji wake.

Ina maana anakiri kuwa Bunge linashindwa kuisamamia Serikali hadi wamtegemee mtu mmjoa?! Tunawahitaji wa nini sasa? Bora warudi mtaani na mishahara yao apewe JPM ambaye anatekeleza majukumu yao!

Badala ya kujenga mifumo ya kutunza na kuendeleza hayo mafanikio, wanawaza kumtwisha mtu mmoja majukumu yote! Hana hata aibu!!
 
Mipango haramu imeanza!

Mkuu sio imeanza, haya ni matakwa ya Magu toka ameingia madarakani, na amenajisi chaguzi zote za nchi ili awaweke wanaccm wajifanye wanamlazimisha. Ki ukweli hakuna kumlazimisha kokote, bali ndio mkataba alio nao na hao wabunge alioagiza waingie bungeni bila kushinda kwenye box la kura.
 
MBUNGE WA MAKAMBAKO AT
Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.
Hakuna tatizo aongezewe tu ili mambo mazuri yakamilike.Mimi naamini siku raisi wetu atakapomaliza muda wake tutatamani aendelee
 
Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais
-
Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha
-
Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka akisema hata #China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.


Mambo yameanza kuumana`

Apewe Miaka 100 itapendeza sana.
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

View attachment 1693592


Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania .

Mwili Mkubwa kama le Mutuz alafu Brainless.
 
Back
Top Bottom