Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Mimi nadhani hii mipango inapikwa na mzee baba mwenyewe.
Tujiandae kuwa na Kim Jong un wa bongo aisee.
Wa tz tumeisha aisee
 
Nimeangalia taarifa zake kwenye tovuti ya Bunge nimegundua kwa Umri alionao wa miaka 65 (Amezaliwa 1 January, 1956) hawezi Ku feel machungu ya ukosefu wa Ajira uliopo, mambo ya kuboreshewa mishahara, kikokotoo, wala mfumko wa bei uliopo kwani tayari ana uhakika wa mshahara wa 11milioni.🙆🙆

Ameingia Bungeni tangu 2010, kwa haraka haraka ameshalipwa kiinua mgongo cha zaidi ya 500Milioni.
2010-2015 .........250m
2015-2020..........250m

Mzee amekosa hoja za kuchangia Bungeni hadi analeta hoja za kijinga namna hiyo, kuna hoja za wanufaika wa bodi ya mikopo kupandishiwa makato kutoka 8% hadi 15% ameshindwa kulisemea hata hili??

Dawa ya Wazee kama hawa ni kuwategea Pisi kali za miaka 18 -33 ziwatangulize kwenda kwa Sir God tu.
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

View attachment 1693592

Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania .
Hii ndio major target kwa awamu hii yaani kama hawajabadilisha katiba basi Mungu atakuwa katenda miujiza ulevi wa madaraka umewatawala hawa watu.
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

View attachment 1693592

Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania .
Uchawi bungeni ushaanza eti wananzengo
 
Hapana Mkuu. Mzee Magu anapenda madaraka kuliko hata uhai wake mwenyewe. Fuatilia matamshi na mwenendo wake.
kuna tofauti kati ya kupenda madaraka na kupenda kuogopwa.
sasa hawa wabunge wanacheza na beat.. yaani all this niku secure vyeo vyao.
 
Deo Sanga: Mbunge wa Makambako said:
Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka!
Na "sisi" tunasema kwa kuwa amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais, tunataka aongezewe muda wa kuishi hata kama hatma yake imefika, tusikubali aondoke na kutuacha yatima.
 
Kigogo alisema, hili bunge februari linaanza na mambo ya Mfalme JUHA atawale milele.. Yametimia..
Popote ulipo Shemasi nakupigia "SALUTO.. "
 
Ni aina ya watu tunaowategemea kama viongozibna wawakilishi wetu Kama wananchi lakini ndani ya fikra zao kumefungwa na aina ya mtizamo ambao hauwakilishi matakwa ya wananchi Kama wanavyotakikana.

Pole Ni kwetu watanzania maana kwa aina hii ya watu tunadhania ndio viongozi wetu hakika hutufika tunakotaria na huwenda tukajachekwa Sana na wana wetu ama wajukuu wetu kwamba tulikua Ni wajinga mno!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu COVID-19 jamani inachukua watu wazuri tu inatuachia haya matakataka? Zee pumbavu sana hili! Halafu Magu na yeye anauchuna tu bila kuwakaripia? Hatutaruhusu upumbavu huo, yeye amalize miaka yake tu atembee tunajua imebaki miaka minne tu full stop!
 
Ndio, tunaweza kubadilisha katiba na kuongeza vipindi vya rais aliyepo madarakani kugombea, yaani kwa sasa anaruhusiwa kugombea mara mbili, tunaweza kuongeza hata mara nne au sita.

Wananchi wenyewe wataamua kupitia sanduku la kura, mbona Mheshimiwa Mbowe pale Chadema amegombea zaidi ya mara 3? Yupo in power kwa zaidi ya miaka 20. Kansela wa Ujerumani yupo in power kwa mda gani? Tuache uoga

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Wataamua kupitia sanduku la kura????
 
Back
Top Bottom