Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Huyu mjinga sana,
Ndicho alitumwa na wapiga kura wake!
Sijui kala maharage ya wapi huyu.
 
MBUNGE WA MAKAMBAKO AT
Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.
Hii hoja si ya bahati mbaya ni jambo lililopangwa kwa mikakati madhubuti ambapo muda wake ukifika hakuna wa kulipinga, litaanza kama mzaha lakini wapiga zumari wataongezeka kila nyakati mpaka lionekane lina uhalisia wa mahitaji kumbe umugabe unaingia taratibu
 
Tumbo ka mgonjwa wa safura mbunge choko Sana huyu,hii nchi ina watu zaidi y la milioni 60 ,sio Magufuli pekee ndo anaweza kuongoza mpumbavu Sana wee Deo sanga
 
Huyu mjinga sana,
Ndicho alitumwa na wapiga kura wake!
Sijui kala maharage ya wapi huyu.
Kumjadili Deo Sanga hata kwakumuita mjinga ni kumpaisha tu. Ni pia umkijadili Deo Sanga ni dalili ya kukosa akili na kazi. Dawa ni kumpuuza tu.
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

View attachment 1693592


Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania .
Absolutely. Mwinyi alishasema huo muda ni wa shukurani.
 
Haahaa na huyu kashalipwa posho? Haaahaa halmashauri kuu ya ccm imehamia bungeni sasa
 
Uchaguzi umefanyika Oktoba 2020, Novemba 2020 Raisi alilihutubia bunge na kueleza vipaumbele vyake. Februari mwanzoni 2021 yaani kama miezi mitatu au pungufu tangu aingie madarakani anatokea mtu anazungumzia kuongeza muda wa Raisi kubaki madarakani. Kwa miaka 5 ya uongozi wa kikatiba hata mwaka mmoja hajamaliza ; bado ana miaka 4 na miezi 9. Hivi hiyo ndiyo kazi ya mbunge?
 
MBUNGE WA MAKAMBAKO AT
Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.
Faida ya kupita bila kupingwa.

Badala ya kupigania waalimu waongezewe madaraja yao anakuja na hoja zisizo na tija
 
Haya maneno ya kulishwa. Hivo munamuona MAGU ni mzuri sana?. Haya makampuni yenye kupewa kandarasi ya kujenga majumba na barabara munajuwa ni ya nani. Munajuwa waziri wa fdha ni nani na kawekwa hapo kwa nini. ?. Nyimbo musiojiuwa munaichezea nini?. Au ni mdundiko ndio munao furahia?.
Hivi kwani vinavyo fanyika havipo au Vipo na je impact hasi au chanya tunayopata nchini?
 
Eti “hata asipotaka”. Huyu hata akitamani, hatuwezi kusigina Katiba yetu ili kumuaccomodate mtu mmoja. Ni fedheha kufikiri mwamba kati ya Watanzania 58M+, ni Jiwe tu anayeweza kutuongoza

Lakini huu upuuzi upo hata kwenye vyama vyetu vya siasa.
Miaka yote hiyo alipatikana nani alieweza kuleta mabadiliko kama ya huyu mjomba?
 
Back
Top Bottom