Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

MBUNGE WA MAKAMBAKO AT

Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.
Naomba nimuulize swali deo kama kikwete nawengine waliomtangulia wangeongezewa muda kukaa madarani je leo angeuona huouwezo wa huyo anaetaka aongezwe muda ?
 
Ila lisu ana gundu sana,

Kaifyekelea mbali TLS na Chadema hivyo hivyo,

Kaenda kujituliza zake Belgium.

Ila mkuu CCM kama ni Chama cha mioyo ya wananchi kwa nini hata kukitetea wanatumika majasusi wa TISS
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

View attachment 1693592

Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania.
Juzi tu baada ya kupewa ubunge kule makambako akaja bungeni akashika Biblia akaapa kuilinda Katiba. Leo anatoa hoja ya kuivunja Katiba. Tumweleweje?
 
Hawa wapuuzi Wameshaongea na Mungu juu ya umri wa kuishi wa jiwe?? Mungu fundi Bwana anaweza akafanya yake hata hii mitano akashindwa kuimaliza.

Katiba inatakiwa kuheshimiwa na watu wote licha ya ubovu wake wote.
 
Sasa jamani mtu kama Deo Sanga ombeni Kwanza hata CV yake ndiyo utajua uwezo wake wa kufikiri unakoma hapo.Lakini mimi wakati mwingine upumbavu kama huu wanaulea CCM wenyewe.Mtu anaongelea pumba kama zile nikumchana tu.

Nijuavyo Mimi CCM ni chama chenye hazina kubwa sana ya viongozi ndiyo maana hata huyo JPM alipatikana huko na kufanya hayo makubwa yanayosemwa .

Sasa kama ni hivyo hakuna haja yakuanza kusema eti oooh..amalizie ...ni ujinga tu.Inamaana Tanzania nzima hii hakuna mtanzania anayeweza Fanya haya kabisa?

Mbona hii ni ajabu.

Ifike mahala tuwe tunaongeleayale tuliyotumwa na wananchi kufanya .Yaani Leo Kwanza ndiyo mwaka wa Kwanza tu wa mhula wa pili wa Rais madarakani jitu linaanza kupigia chapuo kubadili katiba.Kama haja hiyo ipo si msubiri japo hata mwaka 2024 huko?.Leo hii mapema hivi haraka ya nini?
 
Sera ya taifa kwa sasa ni Magufuli kuongezewa muda madarakani.
 
Halafu COVID-19 jamani inachukua watu wazuri tu inatuachia haya matakataka? Zee pumbavu sana hili! Halafu Magu na yeye anauchuna tu bila kuwakaripia? Hatutaruhusu upumbavu huo, yeye amalize miaka yake tu atembee tunajua imebaki miaka minne tu full stop!
Hujui unachoamini unajua!
 
MBUNGE WA MAKAMBAKO AT

Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.

Badala ya kufikira kuweka katiba nzuri endelezi tunafikira umungu mtu. Tusingangae tuna umasikini sasa mtu kama huyu kaenda bungeni kufanya nini ?. Hii tufikirie tukija kupata raisi mbaya itakuwaje kama muda ni miaka 14 au 20!!
 
Sasa jamani mtu kama Deo Sanga ombeni Kwanza hata CV yake ndiyo utajua uwezo wake wa kufikiri unakoma hapo.Lakini mimi wakati mwingine upumbavu kama huu wanaulea CCM wenyewe.Mtu anaongelea pumba kama zile nikumchana tu.
Nijuavyo Mimi CCM ni chama chenye hazina kubwa sana ya viongozi ndiyo maana hata huyo JPM alipatikana huko na kufanya hayo makubwa yanayosemwa .
Sasa kama ni hivyo hakuna haja yakuanza kusema eti oooh..amalizie ...ni ujinga tu.Inamaana Tanzania nzima hii hakuna mtanzania anayeweza Fanya haya kabisa?
Mbona hii ni ajabu.
Ifike mahala tuwe tunaongeleayale tuliyotumwa na wananchi kufanya .Yaani Leo Kwanza ndiyo mwaka wa Kwanza tu wa mhula wa pili wa Rais madarakani jitu linaanza kupigia chapuo kubadili katiba.Kama haja hiyo ipo si msubiri japo hata mwaka 2024 huko?.Leo hii mapema hivi haraka ya nini?
Nimeangalia CV yake kwenye tovuti ya bunge. Angeulizwa " wewe wasema hayo kwa nafsi yako au wengine wamekuambia hivyo?". Nadhani wabunge wasomi wako wengi sana,ingependeza kukawa kunajengwa hoja za kuongeza pato la taifa,kukuza uchumi, kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja, namna ya kujenga tax base kwa kuongeza middle income earners n.k. kifanyike kitu gani ili viwanda baadala ya kupelekwa China vije Tanzania, kifanyike maandalizi gani ili kweli kuwe na kuvutia wawekezaji wakubwa hapa kwa maana ya wafanyakazi ,kielimu,kitabia, kitamaduni, kimtazamo wa kizalendo au bora liende n.k.Je kutakuwa na tofauti kiasi gani cha bei ya umeme baada ya bwawa la umeme selous kukamilika, je SGR itakuza uchumi kwa kiasi gani na wananchi wa makambako wategemee nini. Natumaini wanalipwa kwa kuisimamia na kuishauri serikali na siyo vinginevyo. Natamani kusikia hoja za kuleta maendeleo na siyo kupeana sifa. Sifa huja baada ya kazi na siyo mwanzo.
 
Natoa wito kwa watanzania wote ikibidi tufanye maandamano yasiyo na kikomo kumlazimisha mh rais kuongeza muda..hii ni kwa maslahi mapana ya taifa..MTU ameitoa nchi matopeni kwenye lindi la rushwa,umaskini,ufisadi,ujinga,utegemezi n.k na kuipaisha hadi nchi yenye neema tele ndege,elimu bure,ajira,uwajibikaji,afya bora,miundombinu,uwazi,demokrasia na shibe harafu tumwachie eti kwa matakwa ya maandishi tu nyie mwayaita katiba..hakuna katiba iliyo juu ya maslahi ya umma...niko tayali kuandamana hata ikibidi nipigwe risasi nife kutetea maslahi ya watu..narudia ALAZIMISHWE AONGEZA WALAU MIAKA 20
Acha ujinga basi. Baadae mnaanza kulalamika tena tunamkosoa bosi wenu bila staha, sijui bla bla gani.

Kiufupi acheni kutuchokoza Watanzania. Mliyo yafanya kwenye uchaguzi uliopita, yanatosha.
 
Natoa wito kwa watanzania wote ikibidi tufanye maandamano yasiyo na kikomo kumlazimisha mh rais kuongeza muda..hii ni kwa maslahi mapana ya taifa..MTU ameitoa nchi matopeni kwenye lindi la rushwa,umaskini,ufisadi,ujinga,utegemezi n.k na kuipaisha hadi nchi yenye neema tele ndege,elimu bure,ajira,uwajibikaji,afya bora,miundombinu,uwazi,demokrasia na shibe harafu tumwachie eti kwa matakwa ya maandishi tu nyie mwayaita katiba..hakuna katiba iliyo juu ya maslahi ya umma...niko tayali kuandamana hata ikibidi nipigwe risasi nife kutetea maslahi ya watu..narudia ALAZIMISHWE AONGEZA WALAU MIAKA 20
Tufute katiba na kumfanya mfalme wa maisha na akifa mtoto wake amrithi ufalme basi tumalize ubishi kabisa, itapendeza zaidi.

Hapo vipi?
 
Back
Top Bottom