Dereva Bajaji ana Maisha Mazuri Kuliko Watumishi wa Umma

Sisi ni watumishi tu hatuko kwa ajili ya mshahara sisi tuawahudumia wananchi tu katika hali yoyote
 
Maana yake watumishi wa umma maslahi yao ni madogo kiasi cha kuzidiwa kipato na wabangaizaji ?
 
Mada kama hizi za bodaboda sijui bajaji, Guta nk zitakuwa na maana kama zitaletwa na madereva husika wa hivyo vyombo; sisi wengine tusipoteze muda kuwasemea faida wanayopata kwa kutumia data za kijiwe cha kunywea kahawa. Ukipewa Bajaji uka kaa nayo wiki moja utakuja kufuta huu uzi wako...
 
kuna mabandiko Mengine yanaonyesha jinsi gani mwandishi ni mfinyu wa ufahamu. Dereva bajaji ashinde ubora wa maisha kuliko watumishi karibia wote wa serikali? kwamba ana kipato gani kwa mwezi tuanzie hapo.
nadhani kaangali wa kada ya chini
 
Ni asubuhi na mapema nitaomba unitoe kwenye hilo kundi la watumishi wanaozidiwa maisha na mwendesha bajaji .

Niko nasubiri
 
Muda huo hio bajaji humwagi oil,hufanyii service hutii mafuta,we n kuiendesha na kupeleka hesabu tu (Hii kitu nadhani unaisimulia kinadharia sana)
 
Muda huo hio bajaji humwagi oil,hufanyii service hutii mafuta,we n kuiendesha na kupeleka hesabu tu (Hii kitu nadhani unaisimulia kinadharia sana)
Hiyo ni net profit baada ya kufanya yote hayo.

Kumbuka kama mmiliki mwenyewe na dereva mwenyewe mapato ni 50,000-70,000 Kwa siku
 
Painful truth!
 
Kinachodanganya watumishi wa umma ni "ule uhakika wa maisha kwa kidogo anachopata" kazi za kujiajiri mara nyingi ni risk. Ila kama hujali risk ni kazi nzuri yenye kipato kizuri. Kwa taarifa yako hakuna tajiri ambae hajapitia risk mbalimbali.
 
Bodaboda ni bora kuliko wabunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…