Dereva Bajaji ana Maisha Mazuri Kuliko Watumishi wa Umma

Motivation speaker hamna tofauti na mafarisayo.

Mnaongea nadharia sana kuliko uhalisia.

Hii mijadala ya kazi fulanikuwa bora kuliko kazi nyingune ni utoto tu. Hakuna hitimisho lenye ukweli ndani yake.

Katika hii dunia kuna kazi za kila aina na kila kazi ina kipato chake kulingana na mazingira
 
Watu mnaopenda kuwalinganisha watumishi wa umma na hao bodaboda wenu, na waendesha bajaj huwa nawashangaa sana.

Kitendo tucha kuitwa mtumishi wa umma, ni heshima tosha. Hata ikatokea ukapelekwa polisi; mtumishi wa umma anaweza kujidhamini mwenyewe! Ila bodaboda na huyo dereva wa bajaj, hawezi kufanya hivyo.

Na mwisho kabisa, bado maisha ya dereva wa bajaj, kamwe hayawezi kulingana na yale ya mtumishi wa umma.

Hata hizo hela zenyewe ulizoandika hapa, ni za kufikirika tu. Vipi akiumwa, akipata ajali, chombo kuharibika, nk.
 
Ukiona mwenye bajaji anajeuri sana ujue hayajui maisha, sisi baba na mama, kaka, dada zao kama watumishi na wapambanaji ndio tumewapa msingi, na watumishi wamechukua mikopo wakawaajiri hao dereva boda na bajaji maisha ni daraja, ushoga ushaingia tafuteni pesa tafuteni pesa jeuri pesa
 
Mtumishi wa umma, angalia mshahara wako kiasi kinachobaki baada ya makato yote, gawanya kwa siku 30 ili ujue unaingiza ngapi kwa siku. Linganisha na kipato cha bodaboda kwa siku.(bodaboda anaefanya kazi kwa kujituma).
 
Inasemekana wamiliki wa hizo bajaji ni watumishi waliyochukua mikopo...
 
[emoji22]
 
Itakuwa unauza bajaji Sasa unatafuta mteja ambae kimsingi awe mtumishi
Biashara ya bajaji ni ngumu na njaa sana Bora hiyo 8500000 uwekeze kwenye vifaa vya simu au vipodozi na sio bajaji
 
Acha kujidanganya wewe, mtumishi wa Halmashauri anawezaje kumshinda Dereva Bajaj?

Heshima ni pesa sio kuajiriwa.
 
Haijui kabisa biashara ya bajaji na hajawahi hata kuifanya,angejua kuipata 10000 baada ya kuweka mafuta ni kipengele asingeongea
Ana masihara sana, unakuta kijiwe kina bajaji 50+ wanapakia Kwa foleni kupata 20 tu ni mtiti.
 
Kujifariji mko vizuri
 
Acha kujidanganya wewe, mtumishi wa Halmashauri anawezaje kumshinda Dereva Bajaj?

Heshima ni pesa sio kuajiriwa.

Mimi ni muumini wa kujiajiri. Ila siyo katika biashara ya kuendesha bodaboda, bajaj, daladala,nk. Kujiajiri kuzuri ni kule kwa kukaa kwenye ofisi yako, halafu wateja wanakuja ili uwahudumie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…