Dereva wa basi la Mtei Express auawa na madereva wa malori kutoka Rwanda

Hasira za barabarani ni mbaya, tujifunze kudhibiti hisia zetu ma ujue kuwa kuna watu ni machizi zaidi yako ama wana hasira zaidi yako. Huwezi jua atafanya nini ukimfuata. Usishuke kwenye gari yako ukifanyiwa rafu samehe na endelea na safari yako. Hakuna aibu kupisha ugomvi
 
Madereva wa Bus nao wanacheza Rafu ile mbaya.. wakichezew wao ndio wanajifanya kushupaza shingo.

Turudi ktk mada, abiria hao ni wajinga na hawajielewi. Pia huyu jamaa alikuwa hana dereva mwingine msaidizi? Kondakta? Tusihoji reaction ya abiria instead of kuuliza hao wengine kwanza.
 
Pole kwa ndugu na jamaa zake lakini pia ni fundisho kwamba sio kila ugomvi ni wa kupigana wakati mwingine ni kujifanya mjinga siku ipite tu kwasababu alikua amesha wapita hakukua na haja ya kuwasubilia ili kufanya ugomvi.
 
Pole kwa ndugu na jamaa zake lakini pia ni fundisho kwamba sio kila ugomvi ni wa kupigana wakati mwingine ni kujifanya mjinga siku ipite tu kwasababu alikua amesha wapita hakukua na haja ya kuwasubilia ili kufanya ugomvi.
Pia ni reminder kwamba ukiwa unakufa mbele ya watanganyika wenzio watakurikodi warushe status.
 
Swala lilokuwepo hapo ni wa basi kulipita hilo truck na mbele usalama ulikuwa ni mdogo dereva wa basi ikabidi atumie nguvu kumsukuma wa lori ndipo wa ka kwanguana. Sasa marehemu alishindwa kijidhibiti hasira ndio alishuka kwenda kugombana na huto wa lori. Nae wa lori akashuka na mtalimbo tunaoutumia wakati wa kurekebishia matairi akampiga nao dereva wa basi kichwani, walijaribu kumkimbiza hospital lakini ikawa ni haki ya yeye kutangulia mbele za Mungu. hiyo lori ina number za tz lakini dereva ni mtanzania, alikamatwa yupo polisi.
 
Ni dereva wa Manning Nice bus za route ya Tanga Babati nahisi kama sijakosea.

Kuna jamaa yangu anamjua huyo driver ndiye aliyenipa taarifa hii.
Hiyo ndiyo ukweli dereva wa making ice na dereva la lori
Dereva wa maning ice tena ni msambaa...
Walichomekeana na lori...kwenye kupitana...huko mbele basi akapaki akimsubiria lori aje akampiga pini wakaanza kurushiana maneno hdi ngumi
Ndiyo tanboy wa lori akaja kumsaidia dereva wake wa lori
Kwa kumtandika jamaa wa maning ice na mchuma
Alifia wakati anashulikia masuala ya PF3
HILI Tukio nliambiwa na ndugu wa huyo dereva wa bus
Sasa hili la mtei sijui warwanda ndy naisikia sahv

Ova
 
hivi hiyo basi si ilikuwa na abria ? wakwaacha tu hao wauwaji wakauwa na kupanda magari yao wakaondoa? hiki kisa sizani kama ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…