Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Maarifa Hadith Matala (45), Dereva wa daladala, mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake, Sharifa Twaha Nyamaishwa (31), Kondakta wa Daladala aliyekuwa mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo.
Inadaiwa Maarifa alimshambulia sehemu mbalimbali za mwili mpenzi wake huyo na kusababisha kifo chake, tukio hilo limetokea tarehe 16 Agosti 2022 huko maeneo ya Kimara Suka, na mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoweka.
Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo lilianza upelelezi na ufuatiliaji wa haraka na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mkoani Lindi alipokuwa amejificha.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa wapenzi hao walikuwa na migogoro inayosababishwa na wivu wa kimapenzi na kupelekea kugombana mara kwa mara, na mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha.
Uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya tuhuma hizo za kikatili uliovuka kiwango.