Dereva wa Daladala aliyemuua mkewe Dar kisha kukimbia, akamatiwa Lindi

Dereva wa Daladala aliyemuua mkewe Dar kisha kukimbia, akamatiwa Lindi

Kwanini Yule mchina aliyeuwa mpenzi wake Hadi Leo hajakamatwa? Nashangaa wabongo wakifanya mauaji ni siku 3 Tu ameshadakwa ina maana Yule mchina anajua jinsi ya kukwepa POLISI tofauti na wabongo
Ukiwa na pesa hata ukijificha pale karibia na central police hautoonekana, wachina ni wazuri sana wa kuhonga pesa haswa wakiwa na majanga au wakiwa na jambo lao
 
Yaani badala ya kuvuka boda aende Msumbiji eti kaishia Lindi ndo kaona kajificha🤣🤣 hapo atakaa mahabusu miaka 9 kisha kifungo cha maisha wacha akaolewe jela
 
Human experience management
Gender: Male
Status: Shit head
Hisia usiziletee mzaha
 
Ukifanya uhalifu kwa bahat mbaya, make sure unatupa cm yako, usiwasiliane na watu wote unaowajua na wanaokujua, nenda sehem ambayo haina watu ambao unaweza kukutana nao na wanakufaham, usitumie mitandao ya kijamii, badirisha jina, badirisha muonekano wako na uvaaji wako... Ndio maana mnasikia kuna watu wanatafutwa miaka na miaka hawapatikani cha ajabu wanazunguka tu...
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Maarifa Hadith Matala (45), Dereva wa daladala, mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake, Sharifa Twaha Nyamaishwa (31), Kondakta wa Daladala aliyekuwa mkazi wa Kimara Suka Golani Wilaya ya Ubungo.

Inadaiwa Maarifa alimshambulia sehemu mbalimbali za mwili mpenzi wake huyo na kusababisha kifo chake, tukio hilo limetokea tarehe 16 Agosti 2022 huko maeneo ya Kimara Suka, na mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoweka.

Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo lilianza upelelezi na ufuatiliaji wa haraka na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mkoani Lindi alipokuwa amejificha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa wapenzi hao walikuwa na migogoro inayosababishwa na wivu wa kimapenzi na kupelekea kugombana mara kwa mara, na mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha.

Uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya tuhuma hizo za kikatili uliovuka kiwango.
Mume dereva na mke ni kondakta.......huo ndio ubaya wa mke na mume kufanya kazi za sehemu moja,kudanganya huwezi
 
Yaan Aliya Jana akakimbilia Lind haraf leo kakamatwa ?? Sasa alijifichaje yaan unakamatwa mapema hivi?

Mapenz haya yatatumaliza tuspokuwa makini, hasa hasa cm znachangia Sana kugombanisha na kusababisha migogoro na vifo kwa wanandoa!!

Zaman sm hazkuwepo na ndoa zlikuwa na aman, kwa hyo wanandoa tuwen Makin na cm zetu
Kabisaaa
 
Mume dereva na mke ni kondakta.......huo ndio ubaya wa mke na mume kufanya kazi za sehemu moja,kudanganya huwezi
Hakuna sehemu taarifa inasema ni sehemu/daladala moja. Kwani haiwezekani ikawa ni route tofauti?

Mfano dereva aendeshe route ya Kimara-Posra halafu mke awe konda wa daladala la Mbagala Rangi Tatu - Mawasiliano?
 
Kwanini Yule mchina aliyeuwa mpenzi wake Hadi Leo hajakamatwa? Nashangaa wabongo wakifanya mauaji ni siku 3 Tu ameshadakwa ina maana Yule mchina anajua jinsi ya kukwepa POLISI tofauti na wabongo
Kwani hakuna watanzania waliowahi kuuwa wakakimbia mpaka Leo hawajapatikana?, wewe umeona mchina tu au vipi
 
Hapa nina mashaka mchana kutwa wanashinda wote kazini kwao wakirudi wote wamechoka au abiria kaomba namba kwa kondakta?
 
Back
Top Bottom