Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,009
Reaction score
2,315

Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa gari kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
 
Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuwawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.
Asee nimeiona hii habari hapa ITV. Kwamba dereva alitaka kuwagonga polisi kwa gari na baada ya wao polisi kukimbia gari ikagonga kichaka kisha dereva akashuka na kitu kama kisu kutaka kuwashambulia polisi na kuwanyang'anya bunduki ndio wakamchapa ganzi. 😂😂
 
Dereva wa lori la Dangote ameuawa na polisi baada ya kujaribu kumnyang'anya silaha askari.

Kamanda wa polisi Lindi amesema awali dereva huyo alitaka kuwagonga askari hao na lori lakini liliwakosa na kuingia porini kisha akashuka na kutoa kisu na kujeruhi askari watatu kabla hajauawa.

Source: ITV habari!
 
Body cam footage za hao polisi ziwekwe hadharani tujue ukweli ni upi.
 
Kutaka kumnyang’anya polisiccm silaha ni uongo wa hao jamaa ambao ni waongo WALIOKUBUHU.

Back
Top Bottom