La Quica
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 1,009
- 2,315
Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa gari kisha gari likaingia msituni.
Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.
Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.