comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,014
- 6,834
Adam Mohamed Bakari, dreva wa Mh. Lissu aliyasema haya katika mahojiano yake na DW kwa mara ya kwanza akiwa nchini Ubelgiji, zaidi ya mwaka mmoja na nusu tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.
===
Adam Mohamed Bakaria aliyekuwa Dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A. Lisu amehojiwa na DW nchini Ubelgiji ambapo ameelezea tukio la kupigwa risasi la aliyekuwa bosi wake.
Amesema baada ya kujua kuwa wanafuatiliwa alianza kuwa makini sana kwa kuwa wao hawakuwa watu wa kwenda maeneo ya club nk. Siku ya tukio amesema aliona gari mbili zinamfuata, ambapo alipunguza speed ili ziwapite lakini hazikuwapita. Baadae alijua gari hizo zinawafuatilia lakini hakumwambia Tundu Lissu.
Wakati huo alikuwa katika mwendo wa kawaida, baadae ikabidi aongeze speed na akaona ni kweli gari hizo zilikuwa zinawafuata. Baada ya kupita Club 84 alisimama na gari nyingine aina ya V8 iliwafuata kwa speed. Ilibidi aingie ndani walipokuwa wanakaa na kupark gari ambapo gari zilizokuwa zinawafuata zikapaki ndani.
Wakati huo akamwambia Lissu asishuke kwa kuwa kuna watu wanawafuatilia. Hapo wakakaa ndani ya gari ili kusubiri waliokuwa wanawafuatilia watoke ili wawajue, hata hivyo watu hao hawakushuka. Baada ya kukaa kwa muda mrefu watu hao waligeuza gari kuelekea walipotokea, baadae wakarudi reverse kwa speed na kuanza kushambulia.
Dereva wa Lissu amesema bosi wake alikuwa kushoto kwake, kwa hiyo wakati wa mashambulizi aliupigamlango kutoka nje, na alimvuta Lissu upande wake.
DEREVA ASEMA HAHUSIKI NA SHAMBULIO HILO
Adam Mohamed amesema amekuwa dereva wa Lissu kwa miaka 16 na anamchukulia kama ndugu yake na sio bosi wake. Amesema wanaosema kuwa yeye anahusika na shambulio hilo au kuwa alikimbia ni watu wasiojua hali halisi kwa kuwa walikaa Nairobi kwa miezi mitatu na hakuna aliyekwenda kuwahoji.
Aidha amesema yeye ndiye aliyempeleka Tundu Lissu, General Hospital Dodoma na polisi walikuwa wanakwenda na wanamuona na wala hawakumuhoji. Amesisitiza kuwa yeye hakukimbia wala hakufichwa, na alikuwa tayari kwa mahojiano.
Aidha amesema alipata mfadhaiko baada ya tukio hilo kwa kuwa yeye hakuzoea masuala ya vita.