Sasa kwa taarifa yako, kanisa katoliki biblia siyo chanzo pekee cha imani, tunavyanzo vingine zaidi ya vitano.
Tuna kitu tunaita mang'amuzi/mguso (Godly experiences) kwa hili ijapotokea Mungu akanitendea jambo/akanigusa kwa namna ya pekee je, wewe utawezaje kuelezea mguso wa Mungu kwangu?? Hii ni chanzo experience ya watyu hasa watakatifu ambao nje ya hapo maisha yao ni ushuhuda wa imanni yao kwao na kwa watu wengine.
Tunacho chanzo kingine, haya ni mapokeo na hapa watu wengi sana mnachanganya na vitu kama mitaguso, hapa mapokeo ni mambo mengi ambayo yanafanyika kwenye kanisa lakini hayaandikwa wazi au ayakuandikwa kabisa katika biblia ila yalikuwa yanafanywa na mitume. Haya mambo mengi utayapata katika maisha ya watawa na mapadri au katika taratibu za kiibada hasa misa.
Chanzo kingine ni biblia hapa sitaki kueleza panajulikana.
Pia tuna chanzo cha mitaguso/maandiko(charters) zitokanazo na synodes/mikutano ya mama kanisa/uongozii wa kanisa. Kwasasa tuna mitaguso miwili ya kanisa wa kwanza ni ule wa mitume wa Yesu juu ya ufundishaji na uendeshai wa imani/kanisa na wa pili umefanyika miaka ya 1960s. Pia zipo mikutano mingi ya mababa wa kanisa/maaskofu/makadinali wamekaa na kupitisha inaongoza watu/wauminini hasa wakatoliki kuishi imani moja ya kanisa katoliki la mitume. Unaweza soma maandiko mengi sana, ikiwemo kateksimu (mtaala wa mafundisho ya imani katoliki).
Chanzao kingine ni Roho mtakatifu, hili fika linajulikana Yesu mwenyewe amesema kuwa tutapatiwa mwalimu mkuu wa kutufundisha mambo makuu na yeye utata juu ya Mungu sehemu, maandiko mengi yanaelezea uwepo wa Roho Mtakatifu na kazi zake.
Kufikia hapa kwangu huwa nakuona u mchanga sana hasa mtu unayetafuta kukua kiimani huku ukabaki kuamini kwamba is only the bible has and can reveal the God truths..! Huwa nakuona mchanga sana.