Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

Detention Register: Jaji Tiganga yuko Majaribuni - Kiza Kinene

Kesi hii inayovutia hisia za wengi, zaidi ya weledi ilihitaji uhuru stahiki wa mhimili wa mahakama na uthubutu wa Jaji katika kutoa haki tupu na kwa mujibu wa sheria.

Pungufu ya hivyo tunakoelekea mahakama haitaweza kukwepa lawama.

Mezani tulipo kuna pingamizi ambalo kigezo chake kikuu ni kuwa mshitakiwa hakuwahi kufikishwa central police Dar.

"Detention register ya mahali ambapo mshitakiwa anadai hakuwahi kufikishwa ina thamani gani mahakamani katika hatua hii?

Katika hali kama hii, inapokelewa vipi kama ushahidi?

Katika hali kama hii inapokelewa kuthibitisha nini, kabla ya Jaji kujiridhisha kwanza ukweli halisi ni upi?

Katika hali kama hii Jaji anajiridhisha vipi nani anasema kweli kuhusu central police baina ya upande wa mashtaka na upande wa washitakiwa?

Haki ikitendeka itaonekana.

Haki ikiporwa kupitia visingizio pia itaonekana ikiporwa kama Mh. Jaji ataamua iwe hivyo.

Changamoto hizi zitufungue macho zaidi kuona tunahitaji katiba ya namna gani kwa hakika ili kuepukana nazo kabisa.
Huyu jaji aweza kuvuliwa ujaji wake , subirini .
 
Nikupe siri moja ambayo watu wengi hawaifatilii.
Wakiendelea kufanya uonevu wa kiwango hiki wanachofanyiwa akina Mbowe.
Tena kwa kiburi,na zaidi kwa kutumia na kutegemea nguvu za dola,fedha ama mabavu waliyonayo.
Naye unayemuonea akawa hana namna ya kujitetea kwa namna yoyote ile.

Nakuhakikishia kwa kiapo.HAKI YA MUNGU,Mungu mwenyewe huingilia Kati kuja kujibu kwa niaba ya wanaoonewa..
Kwa kuthibitisha hilo la mtu "kumshudia" mtu mwingine uongo,yaani kutoa ushahidi wa uongo. Kama wafanyavyo hao mawakili wa serikali,majaji,mashahidi na Mapolisi.
Mungu alitunga Sheria kali(amri) isemayo usishuhudie uongo au usiseme uongo.
Kwa kuwa Wana nguvu watajiona hawajali,lakini subiri majibu ya Mungu.

IMG_20211110_090602_953.jpg
 
thubutu! nani awape wa utetezi? Hukusikia mwanasheria wa tigo akikuambia wanafuata maagizo ya watawala!?

1. Tupo sympathizers kibao hadi 92kj ije kuwa kwenye makampuni hayo?

2. Amri ya mahakama inaweza kutumika pia.

Kwanini kuandikia mate?
 
Kuna mhimili uliojichimbia chin zaid in jiwe voice
Kesi hii inayovutia hisia za wengi, zaidi ya weledi ilihitaji uhuru stahiki wa mhimili wa mahakama na uthubutu wa Jaji katika kutoa haki tupu na kwa mujibu wa sheria.

Pungufu ya hivyo tunakoelekea mahakama haitaweza kukwepa lawama.

Mezani tulipo kuna pingamizi ambalo kigezo chake kikuu ni kuwa mshitakiwa hakuwahi kufikishwa central police Dar.

"Detention register ya mahali ambapo mshitakiwa anadai hakuwahi kufikishwa ina thamani gani mahakamani katika hatua hii?

Katika hali kama hii, inapokelewa vipi kama ushahidi?

Katika hali kama hii inapokelewa kuthibitisha nini, kabla ya Jaji kujiridhisha kwanza ukweli halisi ni upi?

Katika hali kama hii Jaji anajiridhisha vipi nani anasema kweli kuhusu central police baina ya upande wa mashtaka na upande wa washitakiwa?

Haki ikitendeka itaonekana.

Haki ikiporwa kupitia visingizio pia itaonekana ikiporwa kama Mh. Jaji ataamua iwe hivyo.

Changamoto hizi zitufungue macho zaidi kuona tunahitaji katiba ya namna gani kwa hakika ili kuepukana nazo kabisa.
 
Mkuu itoshe tu kusema kule Dodoma, wakati Tundu Lisu anamiminiwa risasi, cctv zilikuwepo na zilikuwa zinafanya kazi!

Pamoja na yote. Kwa vile hawafai haki ni muda wa kuvaana nao head-on.

Movements zao Mosh - Arusha - Moshi - Dar - Mbweni hazitawaacha salama.

CCTV central Zije zipatikane pia.

Taabu iko wapi?
 
Kuthibitisha kama alikuwepo au hakuwepo ni kazi rahisi sana, waombe cctv za wahusika wote waliokuwepo siku hiyo hapo central police, waangalie metadata za minara ya simu kama kweli hao polisi walikuwepo, walinganishe na cctv za mahali ambapo mtuhumiwa alikuwepo na mwisho waangaalie minara ya simu kuelekea mahali ambapo mtuhumiwa alipelekwa, medadata zitasema tu kweli kama hao askari walimpeleka huko central au kwingine maana radio call zao au simu zao za mikononi zitaonesha minara waliyokuwa wanapitia.
Nani atatoa hizo data,polisi haiwezi kujichunguza
 
Huyo Jaji yuko kwenye mission maalum ndiyo maana anafanya fyongo za wazi hadi yeye mwenyewe anaona aibu anaishia kutazama chini.
 
thubutu! nani awape wa utetezi? Hukusikia mwanasheria wa tigo akikuambia wanafuata maagizo ya watawala!?

Mpaka tuseme ma sympathizers tupo?

Mahakama hutoa amri pia.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kuthibitisha kama alikuwepo au hakuwepo ni kazi rahisi sana, waombe cctv za wahusika wote waliokuwepo siku hiyo hapo central police, waangalie metadata za minara ya simu kama kweli hao polisi walikuwepo, walinganishe na cctv za mahali ambapo mtuhumiwa alikuwepo na mwisho waangaalie minara ya simu kuelekea mahali ambapo mtuhumiwa alipelekwa, medadata zitasema tu kweli kama hao askari walimpeleka huko central au kwingine maana radio call zao au simu zao za mikononi zitaonesha minara waliyokuwa wanapitia.
Daaah, wewe unaufumbuzi wa tatizo wasiloweza kulikubali wahusika wote wa upande huo.
Na kwa vile wao ndio waonyesha shoo yao, huwezi kupata ushirikiano wowote juu ya kazi hiyo.
 
Daaah, wewe unaufumbuzi wa tatizo wasiloweza kulikubali wahusika wote wa upande huo.
Na kwa vile wao ndio waonyesha shoo yao, huwezi kupata ushirikiano wowote juu ya kazi hiyo.
Hili jambo litakuja ibuka tu muda si punde maana hakuna namna ya judge kujua kama walikuwepo au hawakuwepo.. movement orders za radio calls haswa kwenye servers and minara ya mawasiliano. Movement za magari yaliyotumiwa kuwasafirisha sehemu mbalimbali , cctv ambazo zinaweza onesha magari ya polisi yakienda huko cetre , maadam wametaja muda , tarehe na mwaka , ushahidi uko wazi, si lazima utoke polisi (Wanaweza kuuchakachua, lakini computer itasema kama wali edit na kuchakua- wataalam wa comouter forensic wanajua nachosema), hata watu binafsi pia wanaweza leta kama wanazo hizo videos... ni lazima sasa tushirikiane ili mapolisi watuambie ni gari gani walitumia, number plates za magari hayo na , saa ngapi , walikuwa wapi , mahala gani, sehemu gani ili tuweze kukonect dots kama wanasema ukweli au la , vinginevyo hii kesi ni isidingo tu kwa mawakili wa serikali kuchukulia uzoefu wa kazi kutoka kwa wenzao wa private practice...
 
Back
Top Bottom