PreGE2025 Devotha Minja: John Heche ameshindwa kuitisha kamati kuu kujadili kesi ya Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Devotha rudi nyumbani Marangu ugombee udiwani, tutakuchagua. Ila nawe Devotha mbona haujawahi kumtembelea mwenyekiti wako umjulie hali, mtamuongeleaje mkikutana huku haujui mawazo yake!
 
Kwahiyo hiyo ndio sababu yakujiondoa CDM.
hahaha aisee, naona hiyo sasa ni option B ya kupiga hela za CCM baada ya Ile ya kupewa majimbo kupitia CDM kugoma.
 
Akiongea na wanahabari mkoani Morogoro ambapo yeye na wanachama wengine wamejivua uanachama wa CHADEMA, Devotha Minja amesema kuwa Makamu Mwenyekiti ameshindwa kuitisha kikao cha kamati kuu ili kwa pamoja wakae na kujadili madhila ambayo chama kinapitia kwa sasa ikiwa ni pamoja na kesi inayomkabili Tundu Lissu, lakini pia wanachadema kukamatwa

"Siyo jambo la kawaida tangu uchaguzi umeisha tukapata viongozi wapya, Kamati Kuu pekee iliyoitishwa ni ile iliyofanya usajihili wa wagombea wa uchaguzi wa kanda mbili ambazo ni kanda za Zanzibar, ambazo zilikuwa zimebakia kabla ya Mkutano Mkuu ili kupata viongozi wapya."

"Lakini chama kimepata madhila makubwa sana kwa mwenyekiti wetu (Tundu Lissu) kukamatwa na kusafirishwa usiku kucha na hatimaye kupewa kesi kubwa na mbaya, kesi ngumu ya uhaini lakini Makamu Mwenyekiti (John Heche) ambaye anajinasibu kuzuia uchaguzi ameshindwa kuitisha Kamati Kuu ili tujadili kwa pamoja ikiwa ni namna gani ya kupata ushauri wa wanasheria juu ya upi mwelekeo kwenye kukabiliana huko mahakamani ingawa Makamu Mwenyekiti anaonekana huko Dar es Salaam, anaonekana akiendelea na mikutano lakini ameshindwa kuitisha Kamati Kuu tujadili kwa pamoja namna ya kuhakikisha Mwenyekiti wetu anatoka gerezani." Devotha Minja

View attachment 3334695
Kwahiyo ndo sababu yawewe devotha Minja kuondoka cyo
 
Mnaomwita kibaraka kesho lissu naye mtamwita kibaraka kama mrema,cheyo,lipumba nk.
Fijana fya hofyo kabsaaa
Huyo ni kibaraka na ameshaonekana dhahiri. Hata Lissu akionekana ni kibaraka basi jina hilo litamfaa. Mbowe alikuwa kibaraka wa Fisiemu. Period
 
Akiongea na wanahabari mkoani Morogoro ambapo yeye na wanachama wengine wamejivua uanachama wa CHADEMA, Devotha Minja amesema kuwa Makamu Mwenyekiti ameshindwa kuitisha kikao cha kamati kuu ili kwa pamoja wakae na kujadili madhila ambayo chama kinapitia kwa sasa ikiwa ni pamoja na kesi inayomkabili Tundu Lissu, lakini pia wanachadema kukamatwa

"Siyo jambo la kawaida tangu uchaguzi umeisha tukapata viongozi wapya, Kamati Kuu pekee iliyoitishwa ni ile iliyofanya usajihili wa wagombea wa uchaguzi wa kanda mbili ambazo ni kanda za Zanzibar, ambazo zilikuwa zimebakia kabla ya Mkutano Mkuu ili kupata viongozi wapya."

"Lakini chama kimepata madhila makubwa sana kwa mwenyekiti wetu (Tundu Lissu) kukamatwa na kusafirishwa usiku kucha na hatimaye kupewa kesi kubwa na mbaya, kesi ngumu ya uhaini lakini Makamu Mwenyekiti (John Heche) ambaye anajinasibu kuzuia uchaguzi ameshindwa kuitisha Kamati Kuu ili tujadili kwa pamoja ikiwa ni namna gani ya kupata ushauri wa wanasheria juu ya upi mwelekeo kwenye kukabiliana huko mahakamani ingawa Makamu Mwenyekiti anaonekana huko Dar es Salaam, anaonekana akiendelea na mikutano lakini ameshindwa kuitisha Kamati Kuu tujadili kwa pamoja namna ya kuhakikisha Mwenyekiti wetu anatoka gerezani." Devotha Minja

View attachment 3334695
Tuangalie tuu jamii forum isijekuwa kama Inst na Facebook
 
Naiona hoja. Yaani hata Kamati Kuu ya dharura wakati kiongozi wenu mkuu ana kesi ya tuhuma za kuweza kunyongwa hadi kufa? CHADEMA imetufanya watanzania tuufute kabisa upinzani vichwani mwetu. Kwa hali hii, CCM itatawala sana.🙏🙏🙏
Nchi kuwa na watu kama wewe hata chama tawala kikifutwa kichwani mwako ni sawa tu. Huna tofauti na Bashite
 
Back
Top Bottom