Gari yako ya kwanza ulienda Kukopa, ulikopa Wapi...!? Kwa dhamana gani....!?
Ulikopa Gari then ndo ukaanza biashara yako ya kwanza kuuza Mafuta ya Taa...!
Nyie hamkua Masikini, story za aina hii hazimsaidii ama kum motivate Masikini, ambaye hawezi hata kukopesheka kwa Pikipiki....!
Mimi nataka kusikia kama hivi....!
Nilichukua Gunia 3 za mahindi ambazo nilivuna baada ya kulima kwa mkono, Gunia 2 nikaenda kuuza, Gunia moja nikasaga Unga, nikanuua Mafuta, Dagaa, Panga, Shoka n.k.
Nikaenda msituni kukata miti na kuchoma mkaa, mkaa wangu wa kwanza kuchoma nikapata Gunia 15, nikauza nikapata laki 3, nikachoma tena mkaa nikapata laki 5...! Nikaenda wilayani kununua hiki na hiki, nikaenda kuuzachuku na huku n.k
Tunataka mifano halisi kama hii....!
Sio unatuambia tu Biashara ya kwanza ya Azam ilikua Bakery ya kutengeneza Mikate.....!
Alipata wapi pesa za kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mikate hamsemi....!
Hatutaki hizo story.....! Tunataka mtiririko unaoeleweka tokea chini.