Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Mbingu ni mali ya Mwenyezi Mungu, ni yeye ndiye huamua nani aingie na nani asiingie.

Toba hufanywa na mhusika mwenyewe mwenye dhambi akiwa na nia ya dhati ya kuacha matendo yake machafu.

Maombi/kuombewa huja pale mtu anapokiwa amezidiwa na ulaibu wa hayo matendo kiasi cha kuwa na pazia/giza kwenye nafsi yake na kutoona ubaya wa matendo yake, hapa either Mwenyezi Mungu mwenyewe akufunilie au neema ya bwana ikushukie kwa wanaokuzunguka kukufanyia maombi.

Mara nyingi yule anayeweza kuziona dhambi zake mwenyewe na kwenda kufanya toba huyu bado bwana yuko naye, giza likiingia kwenye nafsi basi hata fikra za toba kwenye kichwa chako haziwezi kuwepo, unaweza kupona tu kwa watu wa karibu yako kukufanyia maombi au kukulazimisha kwenda ibadani hata kwa fimbo kulingana na wao kuyaona matendo yako yanayokera mbele za mwenyezi Mungu kulingana na imani yako/yenu.

Dhambi za kudhulumu wengine kama kuwaibia, kudhulumu amana zao, kutembea na wake za watu kwa kujua kabisa binafsi naamini zinahitaji msamaha wa wahusika uliowatendea na kama ni mali basi inabidi uzitoe sadaka na wewe uanze upya..(wajuzi hapa watanisaidia)..
 
Dhambi tajwa hapo juu, maelekezo ni kumshirikisha Mtumishi wa Mungu wa Kweli.

Amen
Kila Anaweza kuwa mtumishi wa mungu Wa kweli kwaiyo hakuna haja ya ushirika wa mtu mwingine
 
Si uende tu kwa ulie mzinia umuombe msamaha?
Utakacho kutana nacho uwe tayari kukipokea
Ndo ujue UZINZI ni DHAMBI mbaya sana, kuitubia ni Hadi uombe radhi Kwa uliyemibia mke,

Na Kwakuwa kwenda direct ni risk Kwa maisha Yako, ndomana Mungu anashauri utumie mtumishi wa Mungu wa Kweli Ili BUSARA itumike kupata njia Bora ya kusuluhisha Hilo.

Kutubu sirini, hujamaliza tatizo la UZINZI Bado.

Amen
 
Kama ni hivyo na hiyo sadaka apewe huyo muathirika na siyo ale mchungaji
 
Kama ni hivyo na hiyo sadaka apewe huyo muathirika na siyo ale mchungaji
Muathirika hapewi sadaka,

Mwiba mke wa mtu atalipa Mahari ndo ADHABU ya kuzini na mke wa mtu.

Mtumishi anaweza kukusaidia kuyeyusha moyo wa muibiwa mke Ili apunguze.

Sadaka ni shukrani, Wala Si malipo ya lazima.
 
Muathirika hapewi sadaka,

Mwiba mke wa mtu atalipa Mahari ndo ADHABU ya kuzini na mke wa mtu.

Mtumishi anaweza kukusaidia kuyeyusha moyo wa muibiwa mke Ili apunguze.

Sadaka ni shukrani, Wala Si malipo ya lazima.
Kwa hiyo akilipa mahali na mke anachukua?
 
Kwa hiyo akilipa mahali na mke anachukua?
Hiyo ni faini mjomba, soma Waamuzi enzi ya Muda huko.

Muibiwa mke ndo ataridhia amuache mke au amsamehe waendelee na maisha.

Binti ambaye hajaolewa, kijana aliyembikiri ndo hupigwa fine na kuamriwa kumwoa.

Hata sasa, SHERIA hizo hazijabadilika, ndomana dhambi ya UZINZI Mungu ameelekeza ashirikishe mtumishi wa Mungu wa Kweli Ili kumaliza tatizo Hilo Kwa pande zote Kwa HAKI.

Kamwe usitubu sirini ukadhani umemaliza.

Amen
 
ukiona uovu, kemea, yale mambo ya zamani kuona uovu unasema tusikemee usijekuwa sio munyu ndio imepelekea manabii wa uongo kujaza watu wanaoelekea motoni, hasa kwa kile walichokuwa wanatutishia zamani kwamba "usimseme mtumishi wa Mungu", jambo lililopelekea hata wale ambao sio watumishi wa Mungu kupitia hapo kuibia watu pesa na kutumiwa na shetani wapendavyo.

kuna imani nyingi sana zimeibuka siku hizi, zingine hata ukiona kama zina muelekeo wa kupeleka watu mbinguni nyuma ya pasia ni mpango kabisa shetani alikaa akadraft namna ya kudanganya watu, namna ya kupindua injili, namna ya kupotezea watu muda badala ya kumwona Mungu watangetange kutafuta miujiza. na shida yake, waumini walio wengi ni uneducated, masikini na wagonjwa, wanaenda pale in good faith wakijua ni mtu wa Mungu kumbe ni ajenti kabisa anareport kwa shetani.

Kuuza miujiza, kutoa kiingilio kumwona mtumishi, na mengine yote yanayofanana na hayo, ni kinyume na injili, Yesu mwenyewe alisema tumepata bure tutoe bure. and this is the reason why wanapata kiburi cha pesa kama yule wa arusha hadi anajifanya kugawa pesa kwa watu wakati waumini wa mlemle wanazitolea mate izo pesa na hawajui hata watakula nini na wengien hawana hata nauli ya kurudia nyumbani, na yeye akisimama pale anasema hizo pesa ni za kwangu, zilezile walizotoa sadaka masikini. ninyi ndio wachungaji mashetani mlioharibu injili na kuuchekea uovu.

worse enough, fanya yote lakini never undervalue/downgrade the Blood of Jesus. usije hata siku moja ukabeza uzito wa kafara la Damu ya Yesu. lina thamani kuliko vitu vyote na ndio maana lina uwezo kuokoa wanadamu wote duniani, everyone is included ni yeye tu kuamua kulipokea au la.

mtu akija na kusema uchukue sadaka nenda nayo kwa mtumishi ukatubu, hili ni fundisho linalopuuza kafara la Damu ya Yesu, kama vile halitoshi? sisi sote tulishindwa kulipa Garama ya dhambi zenu, Mungu akauliza nimtume nani akaja Yesu, yale aliyopitia, hakuna mwanadamu aliwahi kuyapitia, kafara lake lili cover kila kitu, na alitupatia bure kwa neema tu though hatukustahili. shetani sasa anakuja na kuwaambia watu wabebe sadaka wakati wa kutubu ili within time watu waone kumbe kafara la Yesu halikutosha.

kama kanisa la SILOAM lilivyokuja na doctrine kwamba Jina la Yesu na Damu ya Yesu imepungua nguvu, mashetani yamezoea ndio maana hayakimbiii (kumbe hawajui shetani hawaogopi hata wakitaja Jina la Yesu kwasababu mioyoni mwao hawana Mungu). wamefikia mahali hata wanapoomba hawatumii Jina la Yesu, na awali alipoanza mwanzilishi wao MUNUO pale mbezi makonde, alionekana mtu wa Mungu na watu walikuwa wanaonywa wasimseme, sasaivi limeshakuwa kanisa limesambaa Tanzania nzima, ni wale wanadamu wanaovaa nguo zote hadi viatu vyeupe kama ulishawahi kuwaona. anavaa kiatu cheupe, suruali nyeupe, shati jeupe (ila sura yake nyeusi)....kwahiyo tunawaasa watu, hao manabii na mitume wa kisasa wanaouza vipawa, hauna haja ya kuuliza kama ni watu wa Mungu au la, hao ni matapeli kimbia mara moja. na wewe kama ni mmoja wao ushindwe kwa Jina la Yesu Kristo.
 
Dhambi anaepaswa kutubiwa dhambi ni Mungu peke yake kwa kuwa katika agano jipya pazia la kuingia kwenye kiti cha rehema ambapo aliingia kuhani mkuu akiwa na dhabihu za waungamaji liliondolewa na dhabihu ya Yesu na kukomesha ibaada ya kikuhani ya Haruni.
Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni Kristo Yesu pekee. Kutubu kwa mtumishi ili akufanyie upatanisho ni kurudi kwenye ibaada za ukuhani wa Haruni.
Lazima tutambue tofauti ya ukuhani wa kiharuni na ukuhani wa Melchizedek.
Tulicho agizwa katika agano jipya ni kuungamania sisi kwa sisi yaani kama umemkosea ndugu yako uungame kosa lako kwake na sii umkosee Fred akaungame kwa John.
Pia lazima tutambue utofauti uliopo kati ya dhambi na makosa yafanywayo na mdhambi.
Vitu hivi viwili vinachanganywa sana. Hili husukumwa zaidi na maslahi binafsi ya makasisi( watumishi).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muathirika hapewi sadaka,

Mwiba mke wa mtu atalipa Mahari ndo ADHABU ya kuzini na mke wa mtu.

Mtumishi anaweza kukusaidia kuyeyusha moyo wa muibiwa mke Ili apunguze.

Sadaka ni shukrani, Wala Si malipo
N

Nimekusoma
Kumbe wewe ni wa Musa!mtu wa sheria ndiyo maana hatuwezi kuelewana
Mchana mwema
 
Kwani hilo andiko la Yakobo ni kipindi cha akina nani?
andiko la kwenye yakobo limesema upeleke sadaka wakati wa kutubu, kama wale wa zamani walivyokuwa wanapeleka sadaka ya wanyama wakachinjwe badala yao kufunika dhambi? Yesu kwa kipindi hiki alichinjwa kwa ajili ya wote hivyo tunasamehewa bure bila kulipa pesa.
 
Wakati unatubu zambi kwa mtumishi kwa ndani unakuta na yeye ananyonga bange ukimaliza akavute afu unakuta na tattoo ya nanga kifuani au kama ni wakike unakuta Katia kipini kwenye kisim.i[emoji1787]
 
Wapenda showoffs hao, wao kujionyesha ndio fahari yao na mara nyingi watu wa kaliba ya mleta mada hupenda kujikweza. Kuna baadhi ya watu hawaridhiki ikiwa jamii inayowazunguka haijaona / shuhudia mtu huyo kafanya jambo fulani.

Maombi ni uhuru wa bendera, ukombozi wa fikra ni uhuru wa maendeleo.
 
Asante nimepokea ushauri....
 
Yesu alitoa mwili wake, hivyo hatuhitaji sadaka za wanyama. Ila suala la kuungama liko palepale
 
N



Nimekusoma
Kumbe wewe ni wa Musa!mtu wa sheria ndiyo maana hatuwezi kuelewana
Mchana mwema
BIBLIA haijabadilika, Yesu ameboresha tu AGANO kuwa Imara zaidi.

(Mathayo 5:25)

Patana na mshitaki wako upesi, wakati upo pamoja naye njiani, yule mshitaki asije akakupeleka Kwa kadhi, na kadhi akakupeleka Kwa askari, ukatupwa gerezani.

Leo unakuta mtu ameokoka anakopa na anapiga chenga kulipa, neema Si kudhulumu au kudumu katika Dhambi,

Ukizini na mke wa mtu patana nenda Kwa mtumishi akupatanishe, usamehewe.

Amen
 
N



Nimekusoma
Kumbe wewe ni wa Musa!mtu wa sheria ndiyo maana hatuwezi kuelewana
Mchana mwema
(waebrania 12:14)

Tafuteni Kwa bidii kuwa na Amani na watu wote na huo utakatifu ambao HAPANA atakayemwona Mungu asipokuwa nao.

Dhambi ya UZINZI huwezi pata Amani ukitubu gizani mwenyewe, lazima utafute namna ya kuweka mambo sawa,

Ndomana mtumishi wa Mungu wa Kweli lazima ahusike.

Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…