Dhambi inatakiwa ikemewe namna hii. Sio kubembeleza

Dhambi inatakiwa ikemewe namna hii. Sio kubembeleza

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Kwanza kabisa Mimi Sina dhehebu maalumu japo nimebatizwa Rc na ndoa nikafungia huko.

Napenda kusikiliza mahubiri yoyote Yale. Tofauti tu na mahubiri ya kitapeli na ushuhuda wa uongo, hayo Sina muda wa kuyasikiliza hata kidogo.

Huwa nafurahishwa sana na aina hii ya wachungaji/watumishi wa Mungu wanaokemea dhambi bila kupepesa macho.

Siyo watu una hubiri waache dhambi halafu una wabembeleza wee kama kwamba wanachofanya ni sahihi ila kina madhara! Ni sawa na mzee wa upako kusema kunywa pombe Ni kosa ila sio dhambi.

Padri wangu aliyekuwa hapapasi dhambi ni padre Thomas kabila bilingi. Daima atabaki kuwa padre mzuri mno kuwahi kutokea.

Huyu hata kwenye ndoa kama umepaka makeup umevaa wigi alikuwa hafungi ndoa za namna hiyo.

Nilimkubali sana.


Nisiwachoshe.






 

Attachments

  • 288e1437bcc4ccd2b74a559e97512613.mp4
    7 MB
  • a9b41369ef32fc4a537a6af58cfbc454.mp4
    5.5 MB
Toka mmeanza kukemea hizo mnazoita dhambi mbona kila siku ndio zinazidi?

Tena siku hizi hao wachungaji wenu ndio wanafanya matukio ya ajabu kama hawana ubongo vile🤔
 
Jamaa amenyooka tangu miaka ya 90. Uzuri huyu sio tegemezi wa sadaka. Ameshajikomboa kielimu na kuchumi.

Ukosefu wa uhuru wa kifedha ndio umewafanya wachungaji wawe machawa wa waumini wakiwaogopa. Huwa nawaangalia machoni unaona kabisa mtumishi anaona aibu kwa anachokiongea.
Uhakika jamaa anapita mle mle hakuna kuzunguka zunguka
 
Back
Top Bottom