Kwanza kabisa Mimi Sina dhehebu maalumu japo nimebatizwa Rc na ndoa nikafungia huko.
Napenda kusikiliza mahubiri yoyote Yale. Tofauti tu na mahubiri ya kitapeli na ushuhuda wa uongo, hayo Sina muda wa kuyasikiliza hata kidogo.
Huwa nafurahishwa sana na aina hii ya wachungaji/watumishi wa Mungu wanaokemea dhambi bila kupepesa macho.
Siyo watu una hubiri waache dhambi halafu una wabembeleza wee kama kwamba wanachofanya ni sahihi ila kina madhara! Ni sawa na mzee wa upako kusema kunywa pombe Ni kosa ila sio dhambi.
Padri wangu aliyekuwa hapapasi dhambi ni padre Thomas kabila bilingi. Daima atabaki kuwa padre mzuri mno kuwahi kutokea.
Huyu hata kwenye ndoa kama umepaka makeup umevaa wigi alikuwa hafungi ndoa za namna hiyo.
Jamaa amenyooka tangu miaka ya 90. Uzuri huyu sio tegemezi wa sadaka. Ameshajikomboa kielimu na kuchumi.
Ukosefu wa uhuru wa kifedha ndio umewafanya wachungaji wawe machawa wa waumini wakiwaogopa. Huwa nawaangalia machoni unaona kabisa mtumishi anaona aibu kwa anachokiongea.