Dhana potofu ya kwamba kila mtu kaandikiwa kifo chake

Nipe tu elimu hapa mimi ni RC ila nimefanikiwa kusoma majarida yenu toka nikiwa darasa la pili. Pia nimeshiriki ibada zenu
Utakachopanda duniani utavuna hicho hicho,kama hukufuata maagizo na sheria za Mungu bada ww mavuno yako yatakuwa kifo baada ya hukumu (sio kuchomwa moto). Hakuna mpango wowote wa kifo unaofanywa na Mungu.
1. Tunakufa kwa sababu tumerithi dhambi ya kifo toka kwa wazazi wetu(Adam na Hawa)
2. Unaweza kufa kwa uzembe wako mwenyewe.
3. Unaweza kufa kwa sababu ya matukio yasiyotarajiwa.
 
baada ya kifo hapa duniani nitbaki katika mfumo wa roho. Je siku hiyo ya mwisho nitakua katika mfumo gani??? Roho au mwili!?
 
kwa mujibu wa mtoa mada,kama tungeendelea kukua(seli zinazozalishwa zingeendelea kuwa nyingi kuliko zinazokufa),basi kungekuwa na chance ya kuwa na maisha marefu zaidi...provided kwamba unakwepa magonjwa na ajali zinazoweza kupelekea kifo ghafla...ila kwa nadharia hyo pia mtu anaweza kufika miaka 1000 akiwa na urefu wa meter 75( hapo ni kama kila baada ya miaka 20 atakua anaongezeka urefu kwa 1.5 meters).
 
Sio kweli msome mtoa mada linganisha na ulicho andika uone tofauti
 
Ushawahi kufa au unaleta tuu story za kidini
 
Mkuu unajua kwanini jamii ya watu wa kale waliishi miaka mingi sababu kuu ilikua size ya miili yao na vyakula vya asili. Watu walikua na miili mikubwa sana. Mfano kidogo angalia jamii ya wachaga hasa wa zamani wengi waa maumbo makubwa sana ukienda moshi ndani ndani huko utakuta wazee wana miaka 100+
 
natauta more informations,narudi...nisaidie pia...maybe tukijua what was their menu,,tutajua ni vyakula gani vinachochea uzalishaji wa seli hai zaidi kwenye mwili wa mwanadamu.
 
wanasema mtoto akizaliwa huwa analia,
sababu ya kulia ni baada ya kutia saini death certificate yake..hivyo anajililia matanga yake..
hii stori ipo sana najua vinci ushawahi kuskia
Th reason mtoto analia baada ya kuzaliwa ni kuguswa na shetani isipokuwa kwa Maryam na mwanawe (yesu/issa/jesus).

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "No child is born but the devil touches him when he is born, whereupon he starts crying loudly because of having been touched by the devil, except for Maryam and her son." Abu Hurayrah then read: {And I seek refuge with You (Allah) for her and her offspring from Satan, the outcast.} [Sūrat Āl-‘Imrān: 36]
Sahih/Authentic. - [Al-Bukhari and Muslim]
 
Kwa mujibu wa hii hadithi Issa ana mamlaka makubwa zaidi ya Mo.

Kwa sababu Issa hajaguswa na shetani alipokuwa mdogo ila Mo aliguswa.
 
Nazungumzia mada yako kwa upande wa imani ya Kiislam (uislam).

Ipo hivi moja kati ya nguzo ya imani ya kiislam ni kuamini Qudra (makadirio) za Mungu.

Mungu ametufunulia kuwa ana majina 99 yanayoendana na utukufu na sifa zake. Miongoni mwa majina hayo ni Al-A'lim (mwenye Elimu) bi maana kuwa asili za elimu zote unazozijua na usizozijua ni kwake yeye na yeye ndiye mjuzi wa kila kitu ,unachokijua na usichokijua vyote anavijua.

Pia jina lingine miongoni mwa hayo majina 99 ni Al-Qadir ( mwenye kukadiria). Mungu ameumba kila kitu kwa makadirio na sababu zake na matokeo yake.

Mungu kabla hata ya kutuumba wanaadam tayari alishakadiria kuwa atayuumba ,tutakaa katika matumbo ya mama zetu kwa muda gani, kisha tutazaliwa na kuishi katika huu ulimwengu kwa muda gani, tutakula nini, tutakunywa nini n.k haya ni makadirio na ni elimu ya Mungu.Hakuna ajuae katika viumbe vyake .

Na miongoni mwa elimu zake kubwa ambazo hakuna anaejua ila yeye ni kujua lini na wapi kiumbe kitakufa.

Na yeye ndie anaejua sababu ya kifo chako ni nini?

Mwanadam kabla hujazaliwa tayari ushawekewa makadirio kuwa utaishi kwa muda gani, rizki yako itakuwa kiasi gani, utakuwa mwema au muovu, utakuga lini na wapi.
 
Kwa mujibu wa hii hadithi Issa ana mamlaka makubwa zaidi ya Mo.

Kwa sababu Issa hajaguswa na shetani alipokuwa mdogo ila Mo aliguswa.
Hadith inajieleza kuwa Isa mwana wa maryam aliombewa dua na mama yake angali bado yupo tumboni kuwa Mungu amkinge na shetani na Mungu alijibu maombi ya maryam. Issa alipozaliwa hakulia na miongoni mwa miujiza pia aliyopewa ni kuongea hali ya kuwa ni mtoto mchanga. Issa /yesu aliongea kumtetea mama yake dhidi ya tuhuma za uzinifu kuwa alizini ndio maana akampata huyo mtoto.
 
Kwa mujibu wa hii hadithi Issa ana mamlaka makubwa zaidi ya Mo.

Kwa sababu Issa hajaguswa na shetani alipokuwa mdogo ila Mo aliguswa.
Allah amefadhilisha mitume katika daraja tofauti na mbora katika mitume yote ni Muhammad (pbuh) kwasababu mitume yote iliyotangulia ilitumwa kwa kundi au taifa fulani ila Muhammad alitumwa kwa ajili ya ulimwengu mzima. Na pia yeye ndie atakaekubaliwa ombi la kuombea wanadamu wote siku ya mwisho wapate kuhukumiwa mara baada ya kuwa washakaa takribani ya miaka elfu hamsini wakisubiri hukumu ya Mungu ipite.
 
Kama haya ndio mafundisho basi mnapotoshwa sana, Ina maana Gani sasa ya mtu kuzaliwa kama Kila kitu keshapangiwa? mfano; utazaliwa maskini utakufa na utapiamlo yaani umezaliwa ya nini sasa?

Nachofahamu Mungu anajua hatma yetu lakini haimaanishi ndio kapanga iwe hivyo (Mtu kujinyonga), kuna watu wamebadili hatma zao kupitia maombi/juhudi n.k.

Hii mentality ndio inafanya watu weusi tuache kuchapa kazi au kumtafuta Mungu eti Kwa kuwa rizki umeshaandikiwa!!
 
Kuhani mkuu ni mmoja tu naye Hana baba Wala mama, anaishi milele, haha Mwanzo Wala mwisho yeah ni Melchizedek ambaye kwetu amejidhihirisha kibinadamu kama Yesu kristo. Huyu ndiye kuhani mkuu, ambaye bila kupitia kwake hakuna namna utafikia ufalme wa mbinguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…