Dhana ya kuoa mtumishi mwenzake ili wasaidiane kimaendeleo imemponza

Hamna makosa hapo, hayo ni matokeo sio makosa, ipo wazi kwamba ukishakubali kushare majukumu ya uwekezaji na mkeo basi mavuno ni ya mke na watoto wako. Ukitaka uhuru Jenga asiweke hata tofali, mwambie tu mke wangu tutakaa hapa.

Hiyo nyumba ni ya mwanamke yeye akajenge nyingine atapata amani kuliko kukimbizana naye.
 
Ngosha tayari kasha pata single room ila ule mtoto mkubwa mwenye 11yrs inabidi aondoke nae kwasasa iko shule ya bweni ila wakifunga itambidi apate mschana wakazi au aoe tena, otherwise atamshinda kulea
Mimi nisaidie hapa, mtu mwenye 51yrs, unasema mtoto wake mkubwa ni 11yrs, nini kilitokea hapo katikati, kama ni mambo ya uzazi sawa, lakini kama alioa na kuzaa akiwa almost 40yrs huyu ana matatizo makubwa,
 
Mimi nisaidie hapa, mtu mwenye 51yrs, unasema mtoto wake mkubwa ni 11yrs, nini kilitokea hapo katikati, kama ni mambo ya uzazi sawa, lakini kama alioa na kuzaa akiwa almost 40yrs huyu ana matatizo makubwa,
Ndoa ya kwanza ilikufa ila hakubatika kuzaa hiyo ndo ilikuwa ya pili, hana matatizo yoyote yule ni jama mtumishi safi limemkuta tu kama wengine.
 
Yani huko alikotoka huyo mke wa ngosha kayakanyaga unaachaje hati ziandikwe majina ya mwanamke
 
Ishu ya kushare na mke siitaki hata kidogo kuna kiwanja changu nishakianza foundation naona wife anajitiatia kwamba anichukulie mkopo bank tunyanyue yote nimemwabia ukweli kwamb sitaki hata 100 yake 😂 na nyumba yangu nikimaliza namuandikia mdogo wangu.
 
Hao ndio wanawake chako chao na chao kinabaki kuwa chao na familia ya kwao,ila ile familia mnayo ijenga ndani haimuhusu.

Sometimes huwaga na waelewa sana wanao amua kuoa wa mama wa nyumbani, halafu kesho kwenye MaTV utawasikia haki sawa,50/50.Sasa unajiuliza hii 50/50 ipo kwenye vitu gani?Hapo ndipo unapojua wanawake hata wanavyo jifanya kuvipigania hawajui nini maana yake, hizi harakati za usawa wa kijinsia sijui 50/50 ni mipango ya hizi NGO kupiga hela za wazungu.

Ila ushauri tu kwa wanaume wenzangu, husipigie budget hela ya mwanamke mara nyingi huambatana na dharau pamoja na kejeli na siku zote hela ya mwanamke ni chungu haijawahi kuwa tamu.
 
Hii kanuni yakipumbavu inayotumiwa na baadhi ya wanaume wenzangu sijui itakoma lini, unampangia majukumu mkeo? Mshahara wake? We ni mwehu? Mwanaume tumia kipato chako kuhudumia familia yako, waishi kulingana na kipato chako, acha kutaka maisha ya juu kwakutegemea pesa ya mke. Kama unapata milion na mkeo anakusanya milion 5, panga ratiba na matumizi yako kulingana na milion, mkeo achana na pesa zake, akitaka kujitolea hewala ila usimpangie na jenga kibanda kwa pesa zako, u ajengewaje? Wanaume tunazidi kupungua
 
Na wanakuwaga na uchungu na Hela zao unakuta amekuzidi mshahara lakini anakodolea sana za kwako kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…