Dhana ya "kusaidiana" maisha na mwanamke katika utafutaji ni ya wanaume dhaifu na wajinga sana

 
Nadhani wewe ndiye mwenye Dhana potofu....

Sasa nitoke niende kazini kila siku nimwache mtu ndani 366 days ??? Yeye anafanya nini?

Ndani nina washing machine, dishwasher, kupika ninapika, kufanya usafi ninafanya pia.....

Haiingii akilini mwangu....

mwanamke kwa mwanaume wote waende kazini kama kazi wanazo...Siku hizi kuna mahatiji mengi saana ambayo ni asilimia 1 tu ya watu wanaweza kuyapata.

-school fees
-nyumba
-gari
-shule nzuri za watoto
-nguo nzuri kwa ajili ya familia
-vacation
-chakula bora
-Good phones,TV, internet,

Mambo kibao ....sasa nijitutumue kukamilisha yote haya kama mke anaweza kufanya kazi?

Na utakuwa na mwanamke boya kama let say ni daktari analipwa mshahara mzuri halafu anakuwa selfish eti kisa ni mwanamke na watoto washindwe kuishi maisha mazuri.

Maisha siku zote yalitengenezwa kusaidiana kazi...hata bibi na babu...babu analima mama anapanda viazi.

Tatizo hutokea pale unapokutana na mwanamke mvivu tu.
 
Hakika umeongea ukweli mchungu Sana mkuu.
Siku hizi wavulana na marioo Ni wengi mtaani kuliko wanaume halisi.
 
Una ndoa? I mean umeolewa?
 
QURAN INARUHUSU HATA MWANAMKE KAMA ANAJIWEZA KUMPA MAHARI MCHUMBAWE AKAMTOLEE KWAKE.
 
Mnaomponda mleta mada endeleeni kuponda ila jamaa ameongea ukweli kwa zaidi ya 95%.
 
Eva mke wa Adam alikua mkulma ?! Aise !! Naona kuna toleo la biblia mpya huko mitaani. Huyu huyu Eva aliepewa jukumu la kuza kwa uchungu ndio alikua mkulima ?! Kumbe Mungu alimwambia Eva atakula kwa jasho na sio Adam aliyeambiwa maagizo haya.

Unazungumza baada ya wao kupewa adhabu.
Wote walikuwa Wakulima.
Stori inaeleza jinsi Eva alivyotaka kwenda kutafuta chakula yaweza kuwa cha jioni au alfajiri. Ndipo huko akakutana na vishawishi.

Stori inaonyesha kabisa kuwa ilikuwa Kawaida kwa Eva kwenda kuchukua matunda na ndio maana Wakati anamletea Adamu matunda Adamu hakushangazwa ila kitendo cha kuona tunda la ujuzi wa mema na mabaya ndio kilimshangaza
 

Kulea watoto wanaoenda shule?
Kupika inachukua dakika ngapi Mkuu?
Au unazungumzia kupika kwenye Kuni?

Mwanamke akae nyumbani kwa makubaliano lakini lazima awe mzalishaji wa mali za hapo nyumbani kama kufuga kuku, kuuza kiduka cha nyumbani, kuuza maji, kufuga ng'ombe n.k.
Na sio akae nyumbani kama kaburi
N
 
leo nimekuelewa
 
unasomesha watoto ili waje wakusaidie?, you are a fool
Hapa sijiongelei mimi mjomba, naongelea mazoea ya familia na koo nyingi za kiafrika kutokana na umaskini na ujamaa, vipi wewe wazazi, walezi, ndugu au jamaa zako wanajiweza hivyo huwasaidii siyo
 
Kwamba amtoto akizaliwa aliwa mwaka anaandikishwa shule au sio ?

na yes nakubaliana mwanamke kusimamia miradi ya familia na sio kua muajiriwa huko na mabos wake huko. Akisimamia miradi ya familia boss wake ni mume wake hakuna shida hapo.

Mimi napinga nyie mario kabla ya kuoa mnaanza kuuliza "kwanza huyu mwanamke anafanya kazi wapi ili anisaidie maisha" sijui unanielewa dogo ?!
 

Mke kijakazi
Alafu kuna mke msaidizi wa mume.

Mbona wewe mume wake umeajiriwa?
 
Baambie baambie baelewe.....

Tukitaka tunafanya ila sio lazima...so ukioa jipange kuendesha familia..is how kichwa cha Family is....

Ndo maana mnasema wanawake wana viburi kwa sbb mmeacha majukumu yenu mmewapa vichwa wao ndo waendeshe familia..yani ubaba umegeuka kwa watu wawili...

Ni ila ni baadhi ya wanaume....but wanaume wengine wanajielewa wanatufanya tujisikie tuko peponi...na ndo hiko tunataka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…